Nusura Dr. Slaa chapwe bakora

Nusura Dr. Slaa chapwe bakora

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,676
1003379_10151795697679339_1309594835_n.jpg
 
Walisharuhusiwa siku nyingi tuu mkuu... ikitokea tutajua tuu ni mwendelezo wa ile Slogan ya mheshimiwa!
 
[h=2]USAHIHI; Polisi 'kumdhibiti' Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa[/h]
Ndugu wana JF

Tangu mapema sana asubuhi, tumepokea simu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, watu tofauti, wakionesha concerns zao juu ya taarifa kuwa ofisa mmoja wa Jeshi la Polisi ameonekana kwenye picha 'akimdhibiti' Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willbroad Slaa.

Picha na maelezo yake (caption) yameonekana kuwasononesha na kuwatisha watu wengi.

Ili kusaidia jamii na kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea, iwapo usahihi wa tukio hilo hautaelezwa, tumeona ni vyema kwa nafasi yetu kuweka kumbukumbu sawa.

USAHIHI; Kama ilivyo ada ya misafara ya CHADEMA, hasa inapohusisha viongozi wakuu, viongozi (watendaji waandamizi) wengine wa kitaifa, wabunge na viongozi wengine wa chama katika maeneo husika, huwa ina hamasa, shamrashamra na mapokezi makubwa kila mahali kunapofanyika mikutano au shughuli ya kichama.

Katibu Mkuu, Dkt. Slaa na timu yake walipotua Mpwapwa kwa helkopta siku ya Agosti 18, mwaka huu, alilakiwa na umati mkubwa wa watu, wakitaka kumsalimia na kumkumbatia. Wakifurahia ujio wa mmoja wa viongozi wakuu wa chama katika eneo lao, kwa ajili ya kuendesha Mabaraza Huru ya Rasimu ya Katiba Mpya, katike eneo hilo.

Katika hali kama hiyo, walinzi, wakiwemo askari polisi, walikuwa 'concerned' na hali ya usalama, maana 'lolote' laweza kutokea. Ofisa wa Polisi anayeonekana kwenye picha, alikuwa akiwaelekeza watu wasogee pembeni kwanza, akimwambia Daktari asubiri kidogo watengeneze njia 'vizuri' apite, maana watu wote wale kumfuata na kumkumbatia ingeweza kuwa hatari.

Kama anavyoonekana, Dkt. Slaa naye alikuwa akijaribu kumwambia yule askari kuwa awasaidie wale watu bila kuharibu utaratibu wa yeye kusalimiana na wananchi wake, ambao hujaa kumlaki kwa nia njema, bila kukodiwa wala kusombwa.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Hakukuwa na 'kudhibitiana', bali kulikuwa na kuongozana.

Timu ya Katibu Mkuu, kama ilivyo kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe, kwa kutumia usafiri wa chopa, inaendelea na ratiba ya kuendesha Mabaraza Huru ya Rasimu ya Katiba Mpya, ambapo muda huu timu ya Mwenyekiti imeshaingia Mkoa wa Katavi, kutokea Tabora na timu ya Dkt. Slaa iko Morogoro!

Maelfu ya Watanzania wanaendelea kupata fursa ya kushiriki moja kwa moja, kutoa maoni yao kwenye mabaraza hayo, yanayoendeshwa kwa njia ya wazi kwenye mikutano ya hadhara.

Nawe unaweza kuendelea kutoa maoni yako ya katiba, kwenye Mabaraza Huru ya Rasimu ya Katiba Mpya, kupitia ujumbe mfupi kwenye namba 0789 248224 au email; chademamaoni@gmail.com

Asanteni.

Makene

0752 691569​
 
Nakwambia tangulia kituoni mwenyewe kabla "chopa 😛lane:" haijakunyakua juu juu kama ponda .
 
...nukuu "Ofisa wa Polisi anayeonekana kwenye picha, alikuwa akiwaelekeza watu wasogee pembeni kwanza, akimwambia Daktari asubiri kidogo watengeneze njia 'vizuri' apite, maana watu wote wale kumfuata na kumkumbatia ingeweza kuwa hatari.
Kama anavyoonekana, Dkt. Slaa naye alikuwa akijaribu kumwambia yule askari kuwa awasaidie wale watu bila kuharibu utaratibu wa yeye kusalimiana na wananchi wake, ambao hujaa kumlaki kwa nia njema, bila kukodiwa wala kusombwa."
mwisho wa kunukuu.

...ukiangalia bila ya kusoma hayo maelezo ya ufafanuzi' kweli unaweza fikri alikuwa anachapwa!
 
phweeeh!!!!!!!!! pumzi imeshushwa!!!! maana daah bila huo ufafanuzi....:boink::boink::boink::boink::boink::boink::boink::boink::boink:
 
...nukuu "Ofisa wa Polisi anayeonekana kwenye picha, alikuwa akiwaelekeza watu wasogee pembeni kwanza, akimwambia Daktari asubiri kidogo watengeneze njia 'vizuri' apite, maana watu wote wale kumfuata na kumkumbatia ingeweza kuwa hatari.
Kama anavyoonekana, Dkt. Slaa naye alikuwa akijaribu kumwambia yule askari kuwa awasaidie wale watu bila kuharibu utaratibu wa yeye kusalimiana na wananchi wake, ambao hujaa kumlaki kwa nia njema, bila kukodiwa wala kusombwa."
mwisho wa kunukuu.

...ukiangalia bila ya kusoma hayo maelezo ya ufafanuzi' kweli unaweza fikri alikuwa anachapwa!
Usomaji wa picha inaonekana ni tatizo siku hizi. Kwa namna yoyote ile katika picha hiyo, hata kama polisi angekuwa alitaka kumchapa mtu, basi angekuwa ni huyo mwenye t-shirt nyekundu. Kwanza muone namna alivyosimama kwa hofu, kana kwamba ni mtu anayesubiri kula kipigo, lakini pia angalia Dr. Slaa ambavyo yupo katika hali ya kawaida. Zaidi ya yote, Dr. Slaa anaonekana kuwa mbali zaidi kuliko huyo mwenye t-shirt nyekundu. Kama ni kupigwa basi hiyo fimbo ingeanza kwanza kumfikia huyo jamaa kabla ya Dr. Slaa.
 
Umenena vema mkuu,nilipoiona tu picha kabla ya kusoma maelezo ya wadau nikatambua ni uzushi kama sio kichekesho.Dr Slaa yupo mbali mno na fimbo.
 
Hivi kwa nini Gazeti la MWANANCHI LISIFUNGIWE kwa uongo na uchochezi wa waziwazi kwa watanzania. Yaani Mwananchi walitaka kamba moja nyembamba sana ya uhusiano wa watanzania na jeshi la polisi iliyobaki ?

Narudia mwananchi ni wachochezi wa vurugu baina ya watanzania na jeshi la polisi...LIFUNGIWE tena MIEZI SITA, ili iwefundisho kwa magazeti mengine yenye mwelekeo huo.
 
nahisi nikukosa nidhamu kulipo pitiliza...! huwa njaiuliza ikitokea sisiemu wakishindwa uchaguzi na hatamu ikashiwa na chama kikingine labda UDP ya mzee cheo! hawa jamaa zetu watakuwaje?
 
hapo ndipo utatambua ufahamu wa mabavicha ni wa kiwango gani...soma lugha ya picha kabla ya kukurupuka...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom