samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Miezi ya mwishoni mwa mwaka 2010 kampuni ya simu za mkoni ya vodacom ilianzisha huduma ya kupiga simu voda kwenda voda kwa nusu shilingi kwa sekunde katika mikoa ya Dsm, Morogoro na mikoa mingine ya jirani.
Siku za hivi karibuni makato hayo yamekuwa tofauti. Kwa mfano leo niliweka vocha ya sh. 500 nikiwa Dsm na kumpigia mteja mwingine wa vodacon.
Kilichonishangaza ni vocha hiyo kumalizika ndani ya dakika nne. Nililazimika kupiga simu huduma kwa wateja ili kujua kama huduma ya nusu shilingi kwa mkoa wa Dsm na mikoa jirani bado inaendelea au imesitishwa.
Muhudumu alinihakikishia kwamba huduma hiyo bado ipo isipokuwa katika mikoa mingine ndo wanapiga voda- voda kwa sh moja na nusu pamoja na VAT.
Nilipomuuliza kulikoni sh. 500 ikaisha ndani ya dakika nne aliniambia nimpigie baada ya masaa mawili atakuwa ameniangalizia nini tatizo. Kwa kuwa ilikuwa sa sita kasoro dakika 2 usiku nilishindwa kuvumilia hadi sa nane usiku. Nawaomba vodacom watuweke wazi kama nusu shilingi bado ipo au wameshaiondoa..