Nusu mwaka bila aliyekuwa msaidizi wa mwenyekiti wa CHADEMA taifa Ben saanane, hatua 7 ngumu

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
NUSU MWAKA BILA BEN SAANANE: Hatua 7 ngumu
SAKATA la kupotea kwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) taifa, Ben Focus Saanane, litatimiza nusu mwaka wiki ijayo, Mei 18, mwaka huu, huku mchakato wa kumtafuta ukiwa umepitia hatua takriban nane bila mafanikio.

Saanane ambaye alikuwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alitoweka Novemba 18 mwaka jana hadi sasa hakuna taarifa zozote rasmi kutoka mamlaka za kiserikali kuhusu mwanasiasa huyo kijana.

Pamoja na kuendesha harakati za kisiasa Saanane pia alikuwa katibu wa taasisi inayoitwa Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Nchini (UTG) ambayo imesajiliwa rasmi hapa nchini. Hatua saba kubwa zilizokwishafanyika bila mafanikio ni kupekua kumbukumbu zake Idara ya Uhamiaji (kama yupo nje ya nchi), kukagua hospitali mbalimbali, kukagua mahabusu na magereza, vyumba vya kuhifadhia maiti kwa nyakati tofauti.

Hatua nyingine ni kutoa shinikizo kwa Chadema na serikali kuhusu kutafutwa kwa mwanasiasa huyo, kujaribu bila mafanikio kukagua miili iliyookotwa mto Ruvu na kuzikwa kinyemela na kuanzisha kampeni maalumu ya kuhamasisha mwanasiasa huyo apatikane akiwa hai.

Mwishoni mwa wiki Raia Mwema lilizungumza na ndugu, marafiki na baadhi ya viongozi wa Chadema kuhusu kupotea kwa Ben Saanane, na wameelezea masikitiko yao kuhusu kile walichodai ni uzembe wa vyombo dola kushughulikia suala hilo.

Mmoja wa viongozi wa UTG, Godlisten Malisa aliliambia Raia Mwema kuwa walitoa taarifa ya kupotea kwa katibu wao Ben Saanane makao makuu ya Jeshi la Polisi na katika kituo cha Tabata, Desemba 5, 2016 na kupewa RB namba TBT/RB/8150/2016.

“Jumatatu hiyo hiyo ya tarehe Desemba 5 mwaka 2016 UTG tulianza rasmi kumtafuta Ben maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo katika hospitali mbalimbali ambapo tulitembelea hospitali za Amana, Temeke, Mwananyamala na Hospitali yaTaifa Muhimbili lakini kote tuliambulia patupu,” alieleza Malisa na kuongeza, “Kote huko tulipewa ushirikiano wa kutosha na tulikagua vyumba vya wagonjwa mahututi, na orodha ya wagonjwa waliolazwa hospitalini humo wasiotambulika (unknown cases) na katika vyumba vya kuhifadhia maiti lakini hatukumpata.”

Alieleza zaidi kuwa kati ya Desemba 6 na 7 mwaka 2016, UTG walipita mahabusu katika vituo vyote vikubwa vya polisi jijini Dar es Salaam na magereza yanayotunza mahabusu ya Keko na Segerea lakini Ben Saanane hakuwemo katika orodha ya mahabusu waliowahi kufikishwa katika magereza hayo.

UTG walifuatilia taarifa za Ben pia katika Idara ya Uhamiaji ili kujua kama Ben amesafiri nje ya nchi, ambapo idara hiyo ilitoa taarifa kuwa Ben hajasafiri nje ya nchi kwa kipindi cha mwezi Novemba na Desemba kama ilivyodhaniwa awali.

Kiongozi huyo wa UTG alieleza zaidi kuwa Desemba 8 mwaka huo wa 2016 walisafiri kwenda Bagamoyo kujiridhisha kama miili iliyookotwa huko mto Ruvu inahusiana na Ben kwa namna moja au nyingine, lakini walipofika walikuta miili yote imekwishazikwa bila kuacha kielelezo chochote cha utambuzi.

“UTG tulitoa saa 72 kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na taasisi za serikali kuchukua hatua juu ya sakata la Ben na miilii iliyozikwa Bagamoyo na Desemba 14, Chadema iliitikia wito wetu ambapo Mnadhimu Mkuu wa Chama, Tundu Lissu, alifanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa Chadema kuhusu suala hilo,” aliongeza Malisa.

Alisema Desemba 13 (ndani ya saa 72 za UTG) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kuwabaini waliohusika na mauaji ya watu saba ambao miili yao iliokotwa pembezoni mwa mto Ruvu wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ikiwa kwenye mifuko ya sandarusi, ili hatua kali kwa waliohusika na mauaji hayo.

Kwa mujibu wa Malisa, UTG pia wameanzisha kampeni mpya ya “Bring Back Ben Alive” kama moja ya njia ya kuhamasisha juhudi za kumtafuta Ben kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Kwa upande wake ndugu wa Ben Saanane aliyetambulisha kwa jina la Erasto, akizungumzia sakata hilo alidai kuwa kampuni ya simu ambayo Ben alikuwa akitumia huduma zake, iliwasilisha taarifa ya mawasiliano ya Ben kwa Jeshi la Polisi, Desemba 14, mwaka 2016.

“Taarifa ya mawasiliano ya simu ya Ben ilikuwa na upungufu mwingi hasa taarifa ya mawasiliano ya mwisho. Mawasiliano yaliyowasilishwa Jeshi la Polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao (cyber-crime) yanaonesha kuwa Ben aliwasiliana mara ya mwisho kupitia simu yake tarehe 16/11/2016, lakini Ben aliondoka nyumbani kwake tarehe 18/11/2016 tunatilia shaka kwamba huenda mawasiliano ya Ben ya siku mbili za mwisho (tarehe 17 na 18) yamefichwa kwa sababu maalumu,” alidai.

Mshauri wa kisheria wa UTG, Bob Wangwe, alisema wamewasilisha malalamiko rasmi (ya maandishi) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ambayo kikatiba ina mamlaka ya kusikiliza mashauri au malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu kwa mujibu wa ibara ya 130 na 131 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tume hiyo ina mamlaka ya kumwita na kumhoji mtu yeyote katika Jamhuri ya Muungano isipokuwa Rais wa nchi, Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar.

“Kwa mamlaka yake tume inaweza kuwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini na kuwahoji juu ya matukio ya kuogofya yanayoendelea nchini ya watu kupotea na wengine kuripotiwa kuteswa au miili yao kuokotwa wakiwa wamekufa,” alifafanua Wangwe.

Alisema, kupitia UTG, wanaiomba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imuagize Mkemia Mkuu wa Serikali (GC) kwa kushirikiana na mamlaka nyingine wafukue miili ya watu saba waliozikwa kando ya mto Ruvu wilayani Bagamoyo ili ifanyiwe vipimo vya vinasaba (DNA test).

Wangwe alisema pia wamefanya mazungumzo na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kukiomba kupeleka malalamiko rasmi Umoja wa Mataifa (UN) juu ya matukio ya Watanzania kutoweka katika mazingira tata, akiwemo Ben Saanane.

“Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba tayari LHRC wamekwishaandika barua hiyo Umoja wa Mataifa kuwaomba kuleta wataalamu watakaokuja kuchunguza matukio haya ya watu kupotea, kutekwa na kuuawa,” alisema Wangwe.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema chama hicho kimechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuhakikisha mawaziri wote vivuli bungeni wanagusia suala la Ben Saanane katika hotuba zao wanazowasilisha bungeni.

"Ni Tanzania pekee duniani ambapo mtu anaweza ‘akayeyuka hewani’ na vyombo vya dola vikashindwa kumpata na kutoa maelezo yanayoweza kuridhisha umma," alidai Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.

Hivi karibuni Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliishauri serikali kuomba wataalamu wa uchunguzi kutoka Uingereza (Scottland Yard) kuja kuchunguza suala la kupotea kwa Ben Saanane.

Hata hivyo serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Majaliwa ilipinga mpango huo kwa madai kuwa vyombo vyetu vya usalama havijashindwa kufanya kazi hiyo..
tmp_30363-IMG_20170512_154800654493847.jpg
 
-Ni Tanzania pekee duniani ambapo mtu anaweza ‘akayeyuka hewani’ na vyombo vya dola vikashindwa kumpata na kutoa maelezo yanayoweza kuridhisha umma," alidai Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.
 
Watu wako busy kutafuta mkate wa kila siku kwaajili ya familia zao, tumechoka na porojo zenu za mtu anaejulikana mitandaoni tu. Watu wangapi wanatangazwa kila siku misikitini wamepotea na hakuna anaeuliza.
 
Hata hivyo serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Majaliwa ilipinga mpango huo kwa madai kuwa vyombo vyetu vya usalama havijashindwa kufanya kazi hiyo..View attachment 508252

Kamuulize mbowe anajua alipo huyo saa saba....bado tuna uchungu wa kufiwa na watoto wetu kule arusha na sasa tuna janga la mafuriko...kama huna hoja tupishe
 
-Ni Tanzania pekee duniani ambapo mtu anaweza ‘akayeyuka hewani’ na vyombo vya dola vikashindwa kumpata na kutoa maelezo yanayoweza kuridhisha umma," alidai Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.
Nchi ya viwanda, ingekuwa amepotea hata tembo angetafutwa mpaka apatikane.
 
Ben Saa8 anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa jijini DSM according to Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ubungo Mhe. SAID KUBENEA.
 
Kama mbowe ndiyo alimficha inamaana plan ya kumfichua hakua nayo na huyu kijana kweli na elimu yake ya PhD inamaana kweli alikubali kucheza mchezo wa hatari kama huo?

Na kama ni serkali kwanini wasinge mng'oa kucha na meno kama absolom kibanda na ulimboka na kumuachia huru hadi wamfiche muda wrote huo?
 
If we desire a society of peace, then we
cannot achieve such a society through
violence. If we desire a society without
discrimination, then we must not
discriminate against anyone in the
process of building this society. If we
desire a society that is democratic, then
democracy must become a means as
well as an end.
 
mi sielewi kwanini mpaka sasa kubenea hajaojiwa kuhusu ben kuonekana kwa marafiki zake na kwenye vijiwe vya kahawa
 
Back
Top Bottom