Nundu Amzodoa Chenge : another Cinema in the make!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nundu Amzodoa Chenge : another Cinema in the make!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyumbu-, Feb 23, 2011.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Waziri aanika uozo, madudu mkataba Reli Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 21:07 0diggsdigg

  Ramdhan Semtawa
  NI nadra kwa viongozi wa serikali kukiri madudu, lakini safari hii hali ni tofauti baada ya Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, kuamua kusasambua madudu ya mkataba wa Kampuni ya Reli mbele ya Kamati Bunge ya Miudombinu, akisema ni wa ovyo na hana lugha ya kuwaita.

  Hii ni kauli ya kwanza kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya reli baada ya kelele za muda mrefu za wananchi kulalamikia mkataba huo, uliosainiwa Oktoba Mosi, 2007, wakati Andrew Chenge, akiwa Waziri wa Miundombinu.

  Akiwasilisha Taarifa ya Utendaji wa Kampuni ya Reli nchini kwenye kamati hiyo, jijini Dar es Salaam jana, Nundu alisema mkataba huo, umeathiri uendeshaji reli kwa kiasi kikubwa."Hisa za TRL ni hasi na serikali haitakuwa na gharama ya kununua hisa za Rites," alisisitiza Nundu.

  Nundu alisema Rites walipewa mamlaka makubwa, ikiwamo kuingiza watu watatu kati ya watano kwenye bodi, kuendesha menejimenti pia ikiwa na hisa asilimia 51."Sisi watu wawili na usiombe itokee mmoja akiwa hayupo tumekwenda na maji," alisema.

  Kwa mujibu wa waziri Nundu ambaye anaonekana kuweka mikakati madhubuti kufufua reli hiyo. Kitendo hicho cha kukabidhi mamlaka makubwa kwa Rites, kimeliweka shirika hilo, kwenye hali ya hatari na limedhoofika kwa kiasi kikubwa.

  Alisema kitendo hicho, kimelifanya shirika la reli kujiendesha kwa hasara kipindi chote cha miaka mitatu tangu kuwa chini ya menejimenti ya kukodi.
  "Hili la mkataba tusiseme ni CCM hao...hapa tunazungumza kama Watanzania, kwani kwenye taasisi (zinazohusika na mikataba) kuna watu kutoka Chadema, CUF na CCM.

  "Hili sio jambo la CCM na naamini hata hapa (ndani ya kamati) mpo kwa ajili ya Tanzania. Ninyi ni Watanzania ambao mnaangalia maslahi ya nchi, kwa hiyo nitaeleza kila kitu kwa uwazi hakuna siasa hapa."

  Akionyesha athari za madudu hayo, Nundu alisema licha ya usafirishaji mizigo na abiria kuwa mwezi wakati Rites, ikichukua kampuni hiyo, kiwango hicho kimeendelea kushuka kila mwaka.

  Akitoa takwimu, Waziri Nundu alisema mwaka 2007, zilisafirishwa tani 570,000 za mizigo, mwaka 2008 tani 475,485, mwaka 2009 tani 450,000 na mwaka 2010 tani 253,000 na kufafanua kwamba pia idadi ya abiria waliosafirishwa ilishuka mwaka hadi mwaka.

  "Kwa mfano, mwaka 2007 walisafirishwa abiria 585,310, mwaka 2008 abiria 458,819 na mwaka 2009 abiria 543,001. Hali ya sasa ya TRL sio ya kuridhisha na kutokana na hali hiyo, kuna safari mbili za treni ya abiria kwenda Kigoma pekee na hakuna treni ya kwenda Mwanza ikilinganishwa na mahitaji ya treni tano kwa wiki zinazokwenda Mwanza na Kigoma,"alisema.


  Kuhusu Menejimenti ya Kampuni

  Nundu alifafanua kwamba, tathmini iliyofanywa na mtaalamu mshauri, imebainisha kuwa, thamani za hisa za TRL ni hasi, hivyo hazina thamani na kuweka bayana kuwa, gharama itakazoingia serikali baada ya kuchukua kampuni hiyo kwa asilimia 100, itakuwa ni kulipa dola 23.1 milioni za Marekani (karibu Sh24 bilioni) kwa ajili ya kulipia madeni.

  Alisema uamuzi huo, ni makubaliano ya pamoja kati ya Rites na serikali, ambayo tayari pia imetangaza muundo wa menejimenti mpya ya wazalendo itakayokuwa na wajumbe wa bodi watano kama ilivyo sasa.

  Katika muundo huo, wa menejimenti ya mpito, Waziri Nundu alisema tangu Julai 8, mwaka jana, tayari ameteuliwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye atafanya kazi na Rites kwa lengo la kurahisisha makabidhiano ya uendeshaji TRL wakati menejimenti hiyo ya India itakapoondoka.
  Alisema katika muundo huo, kuna Mkurugenzi mtendaji anayesaidiwa na manaibu wawili; mmoja atashughulikia uendeshaji na mwingine huduma na watasimamia idara tisa.

  Kuvunja mkataba
  Waziri Nundu alisema tayari wizara imekamilisha taratibu mbalimbali, ikiwamo kuwasilisha maombi Wizara ya Fedha na Uchumi kwa ajili ya malipo ya awali ya Rites kwa lengo la kuvunja mkataba wa wanahisa wa Kampuni ya Reli na kuwasilisha nyaraka za kuvunja mkataba huo (Deed of Settlement) na Rites ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya upekuzi (Vetting).

  "Baada ya hapo taarifa itawasilishwa Rites na hatimaye kusainiwa na pande zote mbili za wanahisa, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumevunja rasmi mkataba na menejimenti ya Rites ndani ya TRL kuondoka," alisema.


  Kuboresha Reli
  Kipindi cha miezi mitatu, Waziri Nundu alisema mpango ni kufanyia matengenezo na kuimarisha reli, kununua mashine ya kuokolea (Crane) wakati wa ajali, kukarabati injini na mabehewa ya mizigo na abiria na kuweka fedha za uendeshaji wa kampuni na kwamba, kazi hizo zinahitaji Sh27.45 bilioni.

  Kuhusu kipindi cha mkakati wa miezi sita, alisema malengo ni kutengeneza kiwanda cha kuzalisha kokoto kilichopo eneo la Tura, kutengeneza mfumo wa mawasiliano kati ya Dar es Salaam na Ngerengere na kununua injini za mabehewa.

  Nyingine ni kutengeneza vituo vya magenge, kununua mashine za kushindilia kokoto kwenye tuta la reli na kuendelea kuweka fedha za uendeshaji, kazi ambazo zote zitahitaji Sh63 bilioni.

  Awali, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alitaka wajumbe kujadili mambo hayo kwa uwazi ili kupata mwafaka.
   
 2. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Najaribu kujiuliza kama Peter Serukamba alimaanisha kweli anataka mjadala wa wazi......
   
 3. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokana na taarifa hii jumla ya fedha zinazohitajika kufufua huduma za reli Shs 90.45 billion. Hizi ni chini kidogo ya Shs 94 billion, ambazo William Ngeleja alisema serikali inatakiwa kulipa Dawons haraka.

  Sasa kwa kuwa kabla ya wananchi kuitaka serikali kutolipa hizo hela kwa Dowans kulikuwa na dalili zilionyesha kuwa serikali ilikuwa tayari kulipa DOWANS, sasa hela zile zile ambazo serikali ilitaka kuilipa Dowans haraka haraka zilipelekwe kwenye hiyo reli.

  Kikwete akumbuke wananchi wa Kigoma hawaitaji kiwanja cha Kimataifa cha ndege kule Kigoma. Hawana hela ya kulipia nauli ya ndege. Wao wanataka kupanda treni wakauze dagaa na chumvi kwenye mikoa mingine.

  Peleka hizo hela reli.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Naona mambo si mabaya sana. Hawa viongozi wakweli ni wazanzibari
   
 5. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
   
 6. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyu ni nani? Ni Nundu, RITES owner, Chenge, Al Adawi au Jaji Mkuu. Tafadhali tujuze!
   
 7. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ila badoo lawama hazisaidiii..tunahitajii reli yenye ufanisii..Nundu aonge na utekelezajii wa hiyo mikakatii..
   
 8. T

  Tsidekenu Senior Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Anaitwa Sir Any Chande - ana role kubwa sana kwenye maamuzi makubwa katika nchi hii
   
 9. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mmmh huyu siye aliyetajwa hapa jamvini kuwa ni mmojawapo wa vigogo wa freemasons? kumbe ana role kubwa sana lol kwshinei...shetani ndiye anatawala dola lol
  mix with yours
   
 10. j

  julius Senior Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  OK.Hapo napata matumaini kidogo :decision:na waziri na Nudu,ameweza kuweka mambo sawa ingawa bado kunachangamoto nyingi juu ya uendeshaji wa reli hiyo.kwakweli sijui hii nchi imepata wapi viongozi kama chenge,my GOd??? ameifikisha hapo hyo reli,huyu jamaa nadhani akustaili hata huo ubunge MORAL AUTHORITY yake nayeye pia angekua na kesi za kuujumu uchumi kama wakina mramba na wenzake.
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Sir AC

  Rustom ni Mwanafunzi wake!

  Huyu ndiye anayetawala TANZANIA
   
 12. Bigjahman

  Bigjahman JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Kiongoz mkuu wa mashetan Tanzania naamin ndo anayeongoza hii nchi saiv ndo maana wa2 mnatakiwa sana kusali
   
 13. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo yeye ndiyo Mtawala halisi wa Bongo wengine ni photo copy?

  -Yaani Freemanson live na viongozi wa dini wana muangalia hivi hivi tu bila kumkemea?
  -Ila anaonekana kama ********* vile? Ahhha..! Ndo maana tunaona wanavyomiliki uchumi wa nchi! Nimeelewa sasa!
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwa kiasi kikubwa nimefuatilia utendaji kazi wa waziri Omar Nundu taratibu naanza kumkubali lakini naomba Jf tusaidiane katika hili. Ni mara nyingi sana anapoongelea masula ya kitaifa hana mchezo na anakazia sana maamuzi yake. sikuwahi kumfahamu huko nyuma na sijui kabla ya hapo alikuwa wapi. Huyu ni miongoni mwa mawaziri ninaowatupia macho kwa maana kwamba ameanza kazi yake kwa kunifurahisha.
   
Loading...