Nukuu ya salamu za pongezi kutoka kwa Ajibu kwenda kwa Samatta

magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
7,429
13,172
“Hakuna kinachoshindikana ukiamua katika soka, alipambana na kuzipambania timu alizopita kitu kilichofanya aonekane zaidi. Nampongeza ‘Popa’ naamini ametufungulia njia; sasa kila mmoja atapambana kwa nafasi yake kusaka nafasi ya kucheza huko,” anasema Ajibu aliyekataa kujiunga na TP Mazembe mwanzoni mwa msimu huu.

Ajibu.png
 
Kwani mtu akifanikiwa kwa kumtoa kafara mama yake ni lazima nawe umtoe kafara wa kwako ili ufanikiwe? Kuna njia nyingi sana za kufika kilele cha mafanikio Eliud na Messi wako kule tayari unafikiri watafanikiwa kama Samagoal?
 
Mtu ana miaka 38 anasema kafunguliwa njia sijui ya kwenda wapi huyo

Hayo ni maneno ya kina Kelvin John

Sent using Jamii Forums mobile app
Looooooooooool hata kama una chuki dhidi yake hii ni too much, Samata kaenda EPL akiwa na miaka 27 ana miaka miwili tu ya kucheza soka kwa kiwango cha daraja la dunia (juu) baada ya hapo tegemea kumuona akicheza ligi ndogondogo za ulaya ama akirudi Bongo.

Ajib bado ana nafasi ya kucheza hata Czech kwa misimu miwili sio mbaya
 
Kwani mtu akifanikiwa kwa kumtoa kafara mama yake ni lazima nawe umtoe kafara wa kwako ili ufanikiwe? Kuna njia nyingi sana za kufika kilele cha mafanikio Eliud na Messi wako kule tayari unafikiri watafanikiwa kama Samagoal?
Kanda wa mikiani si alicheza na Sumatra TP Mazembe
 
Mtu ana miaka 38 anasema kafunguliwa njia sijui ya kwenda wapi huyo

Hayo ni maneno ya kina Kelvin John.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kafunguliwa njia ya kwenda Tandale kwa Mtogole maana ndio aina ya viwanja avipendavyo. Yaani huyu jamaa hajitambui anafikiri kucheza mpira ulaya unaomba kwa kutumia passport. Hata Simba wenyewe watamtema maana mpira anaocheza sasa haueleweki.
 
Kitendo cha ajibu migomba kuikataa TP mazembe kimewakera wadau wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba mwenye ushahidi wa Ajib kukataa kwenda Mazembe kama ule ulioletwa kuhusu Ngassa kukataa kwenda Sudan. Aulete
 
Naomba mwenye ushahidi wa Ajib kukataa kwenda Mazembe kama ule ulioletwa kuhusu Ngassa kukataa kwenda Sudan. Aulete
Tulete ushahidi upi wakati TP Mazembe walimsaka kila kona hapo Kariakoo yeye alikuwa anawapiga ahadi za kidemu. Mpaka wakaamua ku surrender na kumchukua Singano aliyekuwa wa Azam. Yaani huyu mtu wako ataendelea kuwagongea buku buku akina Samata na Msuva. Ajue maisha ya uchezaji mpira ni mafupi sana. Akitemwa na Simba itabidi aende Boma FC ya Mwakaleli ili aendelee kujikimu kimaisha.
 
Back
Top Bottom