Nukuu ya msemakweli Chakubanga

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
NUKUU YA MSEMAKWELI CHAKUBANGA.

Nikiwa kama mbobezi katika fani ya Uongozi, Master of Leadership and Management, Labda niwaeleweshe tu, hakuna mwanasiasa mwenye kuzingatia sheria, haki wala utawala bora hapa duniani,iko hivyo ukiwa Mwanasiasa chini yako yatafanyika mambo ya ajabu hadi utashangaa na unaweza usihoji kwa sababu upo kwenye siasa, ndio maana mwendazake kavikwa kila aina ya shutuma ilhali hizo shutuma hata yeye mwenyewe alikuwa akizisikia katika siasa aliyokuwemo, Mwanasiasa yeyote yule duniani lengo lake kuu kuridhisha kundi kubwa la kumuunga mkono kushughulikia jambo fulani linalowagusa na kuwakwamisha wananchi iwe kwa haki au kwa shari,ikiwezekana kuwabana Matajiri ili masikini wapate furaha na aweze kuwateka kisiasa.

Pili kutenda kuendana na mvumo wa upepo wa mahitaji ya kisiasa kwa wakati husika. Sasa safisha inayotumika ndiyo itakayochafua na kusisafishike uko mbeleni na watu watatamani mrejeo kwenye uchafu walioutoa lakini haitawezekana kwa kuwa uchafu utabadilika kuwa sumu kali dhidi yao, I'm not a Jewish prophet ila nimewaza kwa elimu yangu tu ya ubobezi katika Uongozi. Wakati aliyejuu akibanwa kisiasa na walio chini wako tayari kumfurahisha aliyejuu. Sasa hapa katikati ndio kunatokea mgongani pindi aliyejuu atashindwa kuwaelewa waliochini na walio chini watashindwa kumuelewa aliyejuu, nini kitatokea!?

Siku hizi hamna mwenye hofu ya Mungu katika kutaka ndoto zake kuzitimiza kwenda juu kwenye uongozi,mtu yuko radhi kufanya jambo analojua lipo kinyume kabisa na haki hata mbele ya mwenyezi Mungu ili tu lifurahishe Chama au mtu katika siasa ama katika kukubarika kwake kwenye uteuzi, tujitahidi kusimamia haki, duniani tunapita tu na dalili zinaonesha tunaelekea mwisho kabisa ambapo mtawala wa fimbo ya Chuma atakwenda kutawala kwa miaka 7 na kusababisha vita vya Armageddon ndipo Bwana Yesu atakaposhuka duniani kuja kuitawala dunia kwa miaka 1,000 katika utawala ambapo Simba atacheza na swala na chui atakaa pamoja na mwanakondoo kwa undugu na upendo mkubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom