Kuwajibika maana yake nini? Neno hili linatoholewa kutoka kwenye misingi utawala bora. Heche anaposema "tusipowajibishana wenyewe kwa wenyewe ana maanisha tusipofukuzana wenyewe kwa wenyewe, jambo ambalo ni upotofu wa dhana ya utawala bora. Lakini pia mtu anapotoa majibu kwa matendo/ makosa yake si lazima afukuzwe chama au kazi ili chama kionekane mbele ya jamii kuwa kinataka mabadiliko. Sidhani kama kona adhabu moja kwa kila kosa. Tukifanya hivyo tutakuwa wavivu wa kufikiri kwa kutoa jibu moja kwa kila swali.