Nuclear detterence Doctrine

Nuclear detterence Doctrine

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,312
Reaction score
12,194
"If India builds the bomb, we will eat grass and leaves for a thousand years, even go hungry, but we will get one of our own. The Christians have the bomb, the Jews have the bomb and now the Hindus have the bomb. Why not the Muslims too have the bomb?.."
Zulfikar Ali Bhutto; waziri mambo ya nje Pakistan-1965
As long as the world is constituted as it is, every country will have to devise and use the latest devices for its protection. I have no doubt India will develop her scientific researches and I hope Indian scientists will use the atomic force for constructive purposes. But if India is threatened, she will inevitably try to defend herself by all means at her disposal.".
Waziri mkuu wa India-1999
"Israel must be like a mad dog, too dangerous to bother. We have the capacity to take the world down with us. And I can assure you that that will happen before Israel goes under".
General Moshe Dayan-IDF
Hayo ni maneno ya baadhi ya wababe waliopata tokea katika dunia tunayoishi. Hii walikuwa wakionyesha kwanini ili uwe mbabe katika dunia yetu basi inakulazimisha umiliki Nuclear weapons au weapons of mass destruction-WMD.

mf_deadhand3_f.jpg


THE CHAIN-STORE PARADOX
Hii ni concept inayojaribu kumfikirisha mtu katika mchezo na kihalisia inafanyiwa kazi katika maamuzi juu ya jambo fulani lenye uhitaji wa haraka na maamuzi magumu.

Una maamuzi mawili katika mchezo Ubaki mchezoni au Ukubali kushindwa na kumbuka kubaki mchezoni kunahusisha maamuzi laini ya kukubali kula ukiwa na matarajio ya kula baadae au kutoka mchezo kukiwa na maamuzi ya kutumia nguvu kuhakikisha mnakosa wote mchezo!.

Hapo nimetumia lugha rahisi kwa mtu wa kawaida kuielewa concept hii ingawa ni ngumu kidogo kuielewa bila kuufikirisha ubongo wako!.

Katika kukabiliana na mchezo/concept hii Reinhard Selten alikuja na njia za kukabiliana nayo. Selten alisema mtu hukabiliwa na machaguo matatu (3) katik kufanya maamuzi nayo ni: Routine(ratiba), Imagination (mawazo fikirishi) na Reasoning (fikra). kwa kutumia njia hizo tunapata,
  • Routine (ratiba). Hapa mtu atatumia ujuzi alioupitia kipindi cha nyuma katika kufanya maamuzi yake kuhusu yajayo, ingawa maamuzi yanaweza kutokuwa sawa kwa sababu fulani.
  • Imagination (mawazo fikirishi). Mtu atajaribu kufikiri njia mbalimbali na matokeo ya maamuzi kutokana na njia atakazo zifikiri kuamua jambo hilo. Hatua hii kwa namna moja lazima itahusisha ratiba yake.
  • Reasoning (fikra). Mtu atatumia mawazo ya zamani pamoja na kuangalia matokeo ya njia zote atakazo amua kuzitumia kufikia maamuzi yake!.
KWANINI THE CHAIN-STORE PARADOX?
Ilibidi tuanze kuangalia hapo juu sababu katika hizi nchi babe duniani kila moja ina system yake ya kujilinda katika kipindi ambacho itakuwa vitani na mbabe mwenzie na ikiwa inaelekea shindwa vita basi watatumia mfumo huo kuamua njia gani wamalize vita.

Kupitia mifumo hii tunaweza jifunza wenzetu wana maamuzi gani pale watakapoona wanaenda shindwa vita, yani kuliko kuingia utumwani ni bora wafanye maamuzi magumu. Hebu cheki mifumo hii.

1. Mertvaya Ruka au The Dead Hand/ Perimetr system - RUSSIA.

mf_deadhand_f.jpg


Hii system ilianza kipindi cha vita baridi kati ya USSR na USA lakini badae imeendelea kuwepo hadi leo huko Urussi ingawa USSR ilivunjika. Mfumo wa hii system ni kuhakikisha hata kama hakutakuwa na command post yeyote au mtu yeyote Moscow kipindi itakapokuwa urussi imepigwa mabomu basi yenyewe itaruhusu zana zote zilizopo zaidi Intercontinental Balistic Missile (ICBM) kuruka kwenda kumpiga adui.

Ingawa idea kubwa ya mfumo huu ulikua ni kujilinda dhidi ya mmarekani lakini iwapo atatokea adui mwingine basi bado kipigo chake kipo palepale.

Ina maana leo ikitokea adui kaipiga kwa mabomu moscow akijua kashinda vita kupitia first strike basi ajue kuna system iliyopo inayotumia mtetemeko wa ardhi, mwanga, kiwango cha mionzi na sensa zingine zilizofungwa ambazo zikihisi hali tofauti Moscow basi zitaruhusu mabomu yake kulipuka kumfata popote alipo.

Mfumo huu huwa unazimwa kipindi cha amani na kuwashwa kipindi cha hali tete ya vita hivyo kuondoa bahati mbaya zinazoweza jitokeza. mwaka 2015 urusi waligundulika wanatengeneza mfumo mwingine wa kutumia kipindi cha mwisho (last resort) unajulikana kama the Status-6 Ocean Multipurpose System au “Kanyon” hili bomu litatumika kutengeneza tsunami ya baharini ukubwa wa mpaka mita 500 kwenda juu ina maana likipigwa bandarini ni eneo kubwa sana la ardhi litafurika maji kuharibu vifaa vya adui.

"We've since asked the Russians if it's still on and they've assured us, with complete confidence, that we should mind our own business."
Nichols- mwandishi The National Interest​

2. Military Strategic And Tactical Relay(MILSTAR) - USA.

141119-F-IO108-006.JPG


Muunganiko wa satelite kadhaa zinazotumik kurahisisha mawasiliano ya kijeshi marekani, mawasiliano haya hayawezi kuingiliwa kwa njia yeyote na adui (anti-jamming) na ndio yanayotumika kipindi cha vita au marekani itakapokuwa imepigwa kiasi cha kushindwa kabisa kuwa na uongozi.

Ina maana USA itakapokuwa imeshindwa vita basi The Emergency Rocket Communications System ( ERCS ) itatoa muongozo wa vikosi vilivyo maeneo mengine nini vifanye. Ingawa makadirio makubwa yamewekwa inawezekana mfumo huo ukatoa maelezo ya kuilipua marekani au adui kwa kutumia Blue Scout rocket au bomu la Minuteman II; intercontinental ballistic missile (ICBM). Alipoingia raisi George H.W. Bush alitoa maelezo uzimwe lakini hatua yake jeshi imelifanya taratibu hivyo bado upo hewani.

3. The Letters Of Last Resort - UK

download.jpg


Hizi ni barua 4 zinazofanana maneno yake ambazo kila waziri mkuu wa Uingereza anapoingia huwa anaziandika kuelezea jeshi litafanya nini kipindi uingereza itakapokuwa imeshindwa vita. Barua hizi hutumwa kwenye submarine zinazokuwa baharini huko baltic sea.

Hakuna mtu anaruhusiwa zifungua mpaka kipindi kutakapo tokea tukio hilo na kama mpaka waziri anamaliza uongozi wake hakujatokea vita kubwa kwa uingereza kushindwa basi baada ya kuondoka Waziri barua zake huchomwa moto bila kusoma alitoa maamuzi gani na waziri anayefata naye hutakiwa andika maamuzi yake.

Wadadisi wanasema yawezekana akawa waziri amtoa maelezo ya jeshi kuungana na marafiki zao ikiwa UK itafutwa au hata kujilipua wakose wote au kila jenerala ataishi kulingana na maamuzi yake, ila hakuna aliyewahi soma nini kila waziri amekuwa akikiandika. Kutimiza lengo submarine at least moja huwa inakuwa mbali na nyumbani kwao.

4. The Samson Option - ISRAEL

B5CD0eqCEAEp5px.jpeg


Kwa kupitia maamuzi kama aliyofanya samson wa kwenye biblia (waamuzi 16:30) hawa jamaa wakaja na mbinu yao hii. Wao pale itakapotokea Israel imeshindwa vita basi bora wakose wote wanajilipua kwa mabomu yao ya nyuklia. Kama mnakumbuka samson aliposhindwa na mateso aliamua kujiua pamoja na watesaji wake basi jamaa ndio wameifata system hiyo na wao.

Kipindi wanapigana na warabu kwenye The six day war baada ya kipindi cha kwanza kuzidiwa mashambulizi waziri mkuu wao alitoa oda iwapo wataendelea kushindwa zaidi basi mabomu walokuwa wameyaandaa wangeyalipua kuonyesha wapo tayari kukosa wote eneo!.

Unaweza shangaa lakini hawa jamaa hadi leo hawajawasahau wajerumani kw kipigo walichowapa wakati wa vita ya 2 ya dunia. Na ikitokea vita watarudi kulipa kisasi.

twenty, thirty atomic bombs on Berlin, Munich, Hamburg, Nuremberg, Cologne, Frankfurt, Stuttgart, Dresden, Dortmund and so on to assure the job gets done. And the land will be quiet for 1000 years".​

5. No First Use Rule - CHINA
Hawa jamaa wenyewe hawana tatizo na mtu kwahiyo kwenye sera yao wanajitambulisha kwamba hawatatumia mabomu ya nyuklia kwa nchi ambayo haina mabomu hayo ina maana kwa nchi yenye nyuklia watakaposhindwa vita kuyatumia kama njia ya mwisho itakuwa kawaida.

Taarifa nyingi juu ya uwezo wao ni siri maana hata sehemu za kuhifadhi ni siri yao kubwa sana ingawa wamejenga barabara za chini ya ardhi kusafirisha zana zao inaitwa The great underground wall of China.

6. The Minimum Credible Deterrence (N-deterrence) - PAKISTAN.

Agni-1024x684.jpg


Hawa jamaa hasira yao kubwa ipo kwa india zaidi hata ya ugomvi wao na israel. Ingawa walisha apa kutomvamia mtu yeyote lakini wakatoa onyo siku watakayovamiwa hawatasita kutumia njia yeyote ya silaha walizonazo kujilinda. Sera yao haina utofauti na ile ya Mutually Assured Destruction (MAD).

Jamaa wenyewe wanachotaka ni watambulike wamo lakini hawataki kumchokoza mtu wala kuchokozwa, Pakistan ni moja ya mataifa pekee kutumia wanasayansi wake kufanya maendeleo ya kiteknolojia ya nyuklia ingawa kinamna fulani waliiba michoro ya shughuli yote kwa muingereza ila yote ikiwa kujilinda na India tu.

7. No First Use Rule - INDIA.

India-WMD.jpeg


Hawa jamaa nao hawana ugomvi na mtu hadi kutishia kumnuke mtu lakini bado haiwapi chance ya kutomlipua mtu ikiwa watakayepigana naye atakuwa anauwezo wa kumiliki mabomu ya nyuklia. Katika sera yao wanasema hawatakuwa wa kwanza kutumia nyuklia lakimi iwapo kuna mtu atajaribu itumia kuwapiga basi watamlipa kiwango alichowapigia.

Adui yao mkubwa ni Pakistan kutokana na ugomvi wa majimbo fulani mpakani mwao. Ingawa wana ugomvi lakini walishampa uhakika hawatatumia nyuklia mpaka atakapoanza pakistan kuitumia.

8. The Force de Frappe (strike force) - UFARANSA

sna_saphir_0.jpg


Hawa wenyewe wanaamini hata kama utapigwa vipi usiogope kurudisha maumivu yako kwa aliyekupiga hata kama haitaamua ushindi lakini umepelekea kuonekana hujapigwa kivivu.

Ina maana ukipigwa we rudisha kwa kupiga kwa nguvu zako zote sehemu unazoona adui ataumia hata kama mashambulio yatakuwa kidogo lakini umeiridhisha nchi yako, du faible au fort ( Weak-to-strong deterrence ). Kama alivyowahi sema raisi wa ufaransa de Gaulle:

"Within ten years, we shall have the means to kill 80 million Russians. I truly believe that one does not light-heartedly attack people who are able to kill 80 million Russians, even if one can kill 800 million French, that is if there were 800 million French."
Ina maana kwao hata kama raia millioni 800 wa ufaransa wakifa mradi wameua raia million 80 wa urussi basi ni sherehe kwao!. Hawa jamaa muda mwingine hawaeleweki sera zao juu ya Mrusi zipoje hadi hutofautiana na EU kimaamuzi. Au cheki hapa alivyosema Jenerali wa jeshi lao Pierre Marie Gallois,

"Making the most pessimistic assumptions, the French nuclear bombers could destroy ten Russian cities; and France is not a prize worthy of ten Russian cities."
Kuhakikisha hili linafanikiwa huwa wanahakikisha submarine moja inakuwa mbali na nchi yao ili iwapo watashambuliwa basi ile submarine itapeleka maumivu kwa adui. Ufaransa ni moja ya nchi zilizotengeneza mabomu yake kutokana na tafiti zake wenyewe bila msaada wa nchi zingine ni moja ya nchi zenye tafiti kubwa kuhusu mabomu ya nyuklia na adui yao mkubwa wakimuona ni Mrussi.

Itaendelea!...

Cc Da'Vinci, Malcom Lumumba, Elungata, kimsboy, Hussein Melkiory, ze kokuyo, Donatila, zitto junior, infantry soldier dudus Girl Next-door
 
Brother wick thanks kwa madaa hii mujarabuu..
Nipo bize kidogo soon nitarudi tuichambue mwanzo mwisho...

Cc mngony @Infatry soldier
 
Mkuu wick ,kudos!
This is just deep, too deep.
Nimesoma huku niko na tabasamu kubwa sana usoni mwangu.

Japo umeandika maada ngumu kidogo,
Ambayo hutakiwi uisome kichwa kichwa tu kwasababu tu siyo matukio ya kihostoria pekee.
The analysis you have just made is what i call "Putting some life into history"

NB: Kwasababu umesema utaendelea,
For the time being I reserve my comments.

Tuko pamoja mkuu!
 
Japo umeandika maada ngumu kidogo,
Ambayo hutakiwi uisome kichwa kichwa tu kwasababu tu siyo matukio ya kihostoria pekee.
The analysis you have just made is what i call "Putting some life into history"

NB: Kwasababu umesema utaendelea,
For the time being I reserve my comments.

Tuko pamoja mkuu!
Tukiangalia hapo ni kwamba wenzetu imefikia kipindi ambacho Chaguo la kutawalika kwao halipo ni either Ushindi au Mkose wote hii inatuweka wapi sisi ambao mpaka leo tunatumiwa vikosi vya makuruta kuja kututuliza!..
 
mkuu asante kwa hizi nondo .nasubiri yajayo
 
Tukiangalia hapo ni kwamba wenzetu imefikia kipindi ambacho Chaguo la kutawalika kwao halipo ni either Ushindi au Mkose wote hii inatuweka wapi sisi ambao mpaka leo tunatumiwa vikosi vya makuruta kuja kututuliza!..
hahaa hatari mnoo hii...na kuja kututuliza huwa ni Janja Janja tu ..wakija wanabeba na vitakavyo wanufaisha zaidi
 
hahaa hatari mnoo hii...na kuja kututuliza huwa ni Janja Janja tu ..wakija wanabeba na vitakavyo wanufaisha zaidi
Ndio unaposhangaa mwingine anakwambia bora tutawaliwe tena, wakati kuna mwingine anasema ukitaka nishinda najilipua tufe wote!!..
 
You have done your research proper.

Hiyo ya israel ,Samson option ina maana pindi taifa la israel linapozidiwa na kuonekana liko hatarini,watafyatua makombora ya nuclear kupiga miji mbalimbali ya ulaya,Russia ili kwa wanavyosema ,TUFE WOTE.

Jamaa hawataki kabisa kushindwa tena na kumezwa na mataifa mengine kama kipindi cha falme za babel na asyria,
ndo maana dakika zote submarine mbili za israel zinakuwa zimejificha sehemu,hazijulikani zilipo,japo warusi wanadai wanajua zilipo mda wote.

Mwaka 1973 wakati wa vita vya yomma kappur waisrael walipoteza vifaru na ndege nyingi vitani na wakaona wako hatarini,
wakaanza kuandaa makombora ya nyuklia peupe kabisa wakijua satelite za mmarekani zinaona kila kitu,kipindi hicho israel hana nuclear submarine,
so walianza kuandaa makombora ya nuclear kuipiga syria na misri,
marekani kuona hivyo ,Rais wao Nixon akatoa amri haraka israel apelekewe silaha haraka sana,
ndo ikaanza operation kubwa ya kumkimbizia silaha israel ambapo nasikia hadi commercial airliner zilitumika kubeba silaha usiku na mchana kuwahisha israel ndo waisrael wakaweza kuyarudisha nyuma majeshi ya misri na syria.

Na marekani kufanya juu chini kufanikisha mkataba wa amani kati ya israel na misri kwa ahadi kuwa marekani itakuwa ikitoa misaada ya kijeshi kwa misri na israel kwa miaka yote,provided hizo nchi zinamaliza uhasama,
mkataba uliitwa CAMP DAVID
 
Na marekani kufanya juu chini kufanikisha mkataba wa amani kati ya israel na misri kwa ahadi kuwa marekani itakuwa ikitoa misaada ya kijeshi kwa misri na israel kwa miaka yote,provided hizo nchi zinamaliza uhasama,
mkataba uliitwa CAMP DAVID
Kwanini marekani anamsaidia sana Israel angeweza kufanya kumpiga pini asiyarushe!..Na hili la Israel kuweka ahadi ya kumrudia mjerumani ww3 ikitokea nazani wajerumani wajiandae!.
Kuna sehemu nilisoma baadhi ya member wa EU wanataka Ujerumani aanze kumiliki Silaha za nyuklia ili kujiandaa iwapo USA atajitoa kuwasaidia maana UK nae ndio hivyo kajitoa EU!.
 
Back
Top Bottom