Wa Mjengoni
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 480
- 128
Nadhani si mimi tu lakini Wana CHADEMA wengi na UKAWA kwa ujumla tupo njia panda kwenye kura za Urais, ingawa za ubunge majibu tunayo. Kwa washauri wa Mh. Lowassa akiwemo Mh. Mbowe, Prof. Lipumba na timu yote ya viongozi UKAWA tunaomba wamshauri Laigwanani arekebishe mapungufu yake kama ifuatavyo:-
1) Aongeze uwezo wa kujieleza na kwa sauti kubwa sio kunong'ona wakati anahutubia. Watu tunaomsikiliza tunapata mvuto maneno yakiwa kwenye sauti kubwa inayosikika na ya msisitizo. Hata kama pointi zimepangiliwa lakini how do you present? Hata kama anasoma basi asome bila kubabaika kuwe na mvuto kumsikiliza na ayasisitize anayoyasoma kutoka kichwani mwake
2) Wahakikishe Mh. EL amejiandaa kikamilifu kuisoma na kuitangaza ilani ya CHADEMA mara zikianza kampeni. Dr. slaa alishakuwa mzoefu wa kampeni angeingia safari hii, yeye mara ya kwanza awe makini.
Wakati wa kampeni akumbuke wazi wana CHADEMA wengi wana shauku ya kujua hatima ya kipenzi chao Dr. Slaa atakuwa na nafasi gani ya kuijenga nchi yetu kama Kiongozi. UKAWA bila Dr. Slaa naiona haiwezekani. Nashauri katika kampeni atangaze wazi kuwa akishinda, Dr. Slaa atakuwa Waziri Mkuu baada ya kumteuwa kuwa Mbunge. Nadhani Katiba inaruhusu. Hapo mioyo ya watu itatulia. Mlisema Lowassa anakuja na mtaji wake lakini kumbukeni pia Dr. Slaa naye ana mtaji mkubwa CHADEMA ambao unaweza kubadili matokeo ya Urais hata kwa kuharibu kura kwa hasira tu.
3) Ashauriwe kuwa Mh. Magufuli lazima atakuwa anataja madhaifu yake kwenye kampeni hivyo ajiandae pia pamoja na kumwaga sera za ilani lakini pia lazima awe anajibu mashambulizi na kushambulia kwa kutaja madhaifu ya uongozi Mh. John Pombe.
Naamini yakifanyika hayo CHADEMA tutazidi kuwa wamoja.