NSSF wananidhulumu, nifanyeje?

BrazakakaBura

Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
88
Reaction score
104
Naombeni ushauri wenu wakuu tangu niache kazi mwaka jana mwezi wa kumi kwenye kampuni ya kichina nilikokuwa nafanya kazi ya kumwaga zege na kuamua kujiendeleza kimasomo.

Nilifata hatua zote nilizoambiwa lakini kila nikienda sioni ata dalili za kupewa wananiambia tu niandike barua nyingine kila nikienda. Nifanyaje wakuu

Shida ni kwamba sisi maskini kusikilizwa si rahisi kabisa hata nikisema niende kwa mkuu wa wilaya kufika si leo yaani saizi niko radhi hata nusu nipewe nusu ibaki kwa ataenisaidia huko.

Mawazo yenu wakuu
 
Kama wamegoma kukupa kwa amani ,tumia mabavu au tafuta wazee wa chumaulete
 
Tafuta mtu mmoja hapo nssf, mpe ahadi tamu endapo atafanikisha hilo. Wiki haishii, This is Africa (TIA)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…