NSSF Pengo lisilozibika linapozibwa

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,183
1,083
Ni taasisi kubwa sana Tanzania..Ni taasisi iliokuwa na ukaribu mkubwa na waandamizi wa chama tawala..Ni taasisi ilioikopesha sana serikari ya awamu ya nne..Ni taasisi yenye miradi mingi ya mabilioni ya tzs..Ni taasisi yenye viongozi wanaoamini kuondoka kwao pengo haliwezi kuzibika..Ni taasisi iliofanya baadhi ya mazuri mengi kwa watanzania na wastaafu...Ni taasisi yenye tuhuma lukuki kuisimamizi...

Sishangai attention kubwa sana kwenye suala lolote linalohusu NSSF..Wafaidika wa mfumo wa kifalme ulioangushwa ama uliokuwepo wapo ktk juhudi kubwa kukosoa,kuvuruga teuzi,kukosoa teuzi,kukejeli wafanya uteuzi si kwa maslahi mapana ya taifa bali maslahi ya minara yao inayokwenda kuangushwa na utawala mpya unaokwenda kutamalaki muda si mrefu.

Ni rai yangu kwa mteuliwa yeyote ajae kumwomba Mwenyezi Mungu sana juu ya uzima wake,usalama wake,afya yake ya usalama lakini pia kuchukua tahadhari kubwa sana katika utendaji wake wa kila siku ili kuishinda mitego,mishale,fitina na uadui ulio mbeleni.

Ni kiu kubwa kwa wafaidika wa mfumo uliokuwapo kufanya kila wawezalo kuhakikisha mteuliwa yeyote anafail ktk delivery of premium duties,responsibilities,tasks,assignments and etc ili kumprove wrong JPM kwa namna moja au nyingine.Mabadiriko yalioimbwa ndio haya yanatekelezwa kwa kasi kubwa na kwa faida ya wengi na si wachache..wakosoaji hawana budi kuwepo kwa wingi sana ili kuwavunja moyo wapambanaji ,wachapakazi,watenda haki...

Angalizo hekima kubwa sana yatakiwa katika utekelezaji wa majukumu yenye maslahi mapana kwa taifa na wananchi wote kwa ujumla..mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...

Viva Serikari ya JPM...viva Tanzania,Viva Africa
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako wenye wingi wa upendo..
Nitajifunza kiswahili lugha maridhawa na adhimu ili niweze kunyambulisha na kukokotoa vema fikra nilizojaaliwa na maanani..
Ninayo matumaini makubwa ujumbe umekufikia popote ulipo mpendwa Mtanzania....
 
Hii sinema inavutia
Dau alisifika kuijenga NSSF ingawa maadui zake wanasema 'dini yake' anaipenda sana
Waziri Mhagama anaetoka 'Peramiho' kwenye jimbo kubwa la RC church nae anaonekana 'dini yake'
anaipenda sana...anamteua mtu kumbe sio raia...

Magufuli anaonekana kushindwa kufanya maamuzi
Dau kamteua balozi huku hajampeleka 'huko ubalozini'
huku NSSF bado ndo kwanza anatafutwa 'kaimu'

Nini kiliharakisha kumtoa Dau?
 
Dau ameshaondoka, nashangaa anahangaika nini na NSSF. Atulize Boli!. There is life after NSSF

kuwekwe sheria ya kikomo cha kuwa mkurugenzi wa mashirika makubwa isizidi miaka kumi katika mikataba ya miaka mitatu mitatu
 
Hii sinema inavutia
Dau alisifika kuijenga NSSF ingawa maadui zake wanasema 'dini yake' anaipenda sana
Waziri Mhagama anaetoka 'Peramiho' kwenye jimbo kubwa la RC church nae anaonekana 'dini yake'
anaipenda sana...anamteua mtu kumbe sio raia...

Magufuli anaonekana kushindwa kufanya maamuzi
Dau kamteua balozi huku hajampeleka 'huko ubalozini'
huku NSSF bado ndo kwanza anatafutwa 'kaimu'

Nini kiliharakisha kumtoa Dau?

Jibu liko hapa:

News Alert: - Siri ya Ombeni Sefue na Erick Shitindi kuvunja bodi ya NSSF Kinyemela yavuja
 
kuwekwe sheria ya kikomo cha kuwa mkurugenzi wa mashirika makubwa isizidi miaka kumi katika mikataba ya miaka mitatu mitatu

Mkuu niliwahi kupendekeza kitu kama hicho, baadhi ya members walikuja juu wakidai namlenga CEO wa NSSF - majibu hayo yalinishangaza sana!!!
 
The boss nchi hii ina udini sana hasa kundi fulani liliamini nchi hii ni ya kwao na wengine ambao walishiriki kikamilifu ktk kutafuta uhuru wa nchi hii ambao kimsingi na kwa kiasi kikubwa ilishindikana kufaidi matunda ya nchi hii lkn baada ya ujio wa jk amewa proove wrong ktk assumption zao za kijinga baada ya kuwateua watu km kina Dau,othman chande etc na wamefanya kz na zinaonekana sasa hawa jamaa wa upande wa pili imebaki chuki,fitna za kijinga kuwaona waislam km ni maadui ktk nchi hii na kusahau yote waliyoyafanya kwa mustakbali mwema wa nchi hii,tunajua kiukweli hali ya nssf ilivyokuwa na sasa ilivyo,mwacheni dr Dau nyie nyumbuz
 
Hii sinema inavutia
Dau alisifika kuijenga NSSF ingawa maadui zake wanasema 'dini yake' anaipenda sana
Waziri Mhagama anaetoka 'Peramiho' kwenye jimbo kubwa la RC church nae anaonekana 'dini yake'
anaipenda sana...anamteua mtu kumbe sio raia...

Magufuli anaonekana kushindwa kufanya maamuzi
Dau kamteua balozi huku hajampeleka 'huko ubalozini'
huku NSSF bado ndo kwanza anatafutwa 'kaimu'

Nini kiliharakisha kumtoa Dau?
Dr. Dau hajaondoka nssf hadi leo, anaattend ofisini kama kawaida. Labda akipatikana huyo kaimu ndo ataondoka. Nenda hata kesho utamkuta ofisini.
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako wenye wingi wa upendo..
Nitajifunza kiswahili lugha maridhawa na adhimu ili niweze kunyambulisha na kukokotoa vema fikra nilizojaaliwa na maanani..
Ninayo matumaini makubwa ujumbe umekufikia popote ulipo mpendwa Mtanzania....

Mkuu nakupongeza sana sana kwa uchambuzi/maoni yako yaliyo kwenda shule, najua kila binadamu ameumbwa kivyake kwa hiyo usife moyo ukikutana na watu ambao hawachangii chochote cha maana zaidi kuangahika kutafuta tafuta typing errors - badala ya kukosoa kistaarabu wanatumbukiza keje....!
 
Word Up..!

Swali kwa Mh Rais magufuli alikuwa na haraka gani ya kumwondoa Dr Dau Nssf hadi hiv leo na kushindwa kumpangia hiyo nafas ya ubalozi?

Kama kweli kwake yeye Dr Dau alikua ni jipu alishindwa nin kumtumbua?

Kuna nin kimejificha hapo?

Haoni aibu sasa aibu inayowakumbuka wasaidizi wake?

Jenista Mhagama..Omben sefue na Shitindi wako uchi sasa.
Hii sinema inavutia
Dau alisifika kuijenga NSSF ingawa maadui zake wanasema 'dini yake' anaipenda sana
Waziri Mhagama anaetoka 'Peramiho' kwenye jimbo kubwa la RC church nae anaonekana 'dini yake'
anaipenda sana...anamteua mtu kumbe sio raia...

Magufuli anaonekana kushindwa kufanya maamuzi
Dau kamteua balozi huku hajampeleka 'huko ubalozini'
huku NSSF bado ndo kwanza anatafutwa 'kaimu'

Nini kiliharakisha kumtoa Dau?
 
Dr. Dau hajaondoka nssf hadi leo, anaattend ofisini kama kawaida. Labda akipatikana huyo kaimu ndo ataondoka. Nenda hata kesho utamkuta ofisini.

Si kweli tangu ateuliwe kuwa Ambasador kafika mara moja kuchukua his personal belongings, anaendelea na shughuli binafsi kwny ofisi yake binafsi ni Director wa Taasisi mbalimbali binafsi ikiwa ni pamoja na kazi maalum aliyopewa ya kutengeneza Strategic plan ya kuhuisha Stock exchange Market.
 
Mkuu nakupongeza sana sana kwa uchambuzi/maoni yako yaliyo kwenda shule, najua kila binadamu ameumbwa kivyake kwa hiyo usife moyo ukikutana na watu ambao hawachangii chochote cha maana zaidi kuangahika kutafuta tafuta typing errors - badala ya kukosoa kistaarabu wanatumbukiza keje....!
Mungu ni mwema ndugu yangu..asante kwa maneno ya hekima.
 
Hii sinema inavutia
Dau alisifika kuijenga NSSF ingawa maadui zake wanasema 'dini yake' anaipenda sana
Waziri Mhagama anaetoka 'Peramiho' kwenye jimbo kubwa la RC church nae anaonekana 'dini yake'
anaipenda sana...anamteua mtu kumbe sio raia...

Magufuli anaonekana kushindwa kufanya maamuzi
Dau kamteua balozi huku hajampeleka 'huko ubalozini'
huku NSSF bado ndo kwanza anatafutwa 'kaimu'

Nini kiliharakisha kumtoa Dau?

Ili asiharibu zaidi

Kuna fununu jamaa mmoja kutoka jumba jeupe atapelekwa pale kwa kukaimu kwa muda wakati bado anatafutwa mtu sahihi
 
Ifike mahali wananchi tukubali mabadiliko ili kuleta tija mahalia.Kama ndugu Rais alimwona Ndugu Dau haendani na kasi yake katika nssf, ni bora kukubaliana na alivyofanya.
 
Mie simjui Director General wa PPF, LAPF,PSPF wala GEPF wala siyajui mazuri na udhaifu wa hiyo Mifuko na sijui kitu gani kimenifanya nisijue.
hiyo mifuko ni Tabu,michango yetu wanakula tu,mbaya zaidi hata kuwalipa wastaafu ni shida kwelikweli,ila wana wakurugenzi wasomi sana ndio fanikio lao kubwa pekee
 
Sidhani kama mambo ya dini yanatija kuhusu huyu dau. Mbona wengi wameondoka tu hakuna mtu aliyewatetea kuna tu humu
 
Back
Top Bottom