jamaa mmoja,Nshomile aliwakuta rafiki zake wawili wahaya wakiwa katika mazungumzo ya kawaida. mmoja wao alikuwa ana mtoto anaitwa Gosbert ambaye alisoma shule ya msingi na huyu nshomile. mazungumzo yakawa hivi:-
Nshomile: Ndugu yangu za siku, mwanao hajambo?
Baba Gosbert: Salama, mwanao pia vipi?
Nshomile:..aah Livingstone anaendelea vizuri, baada ya primary kalifaulu kwenda Mzumbe, kule kakaperform vizuri sana. High school alikwenda Ilboru akatoka na pointi tatu. wakamchagua Muhimbili, he did wonders akagraduate as a best student, akasomea shahada ya uzamili makerere, sasa ni surgeon, daktari bingwa wa upasuaji. Vipi ka Gosbert, kako wapi siku hizi?
baba Gosbert🙁kwa kujiamini) Aah Gosbert pia alifanya vizuri sana, kwa sasa anashughulikia wagonjwa walioshindikana na mabingwa!
Nshomile:haya kwaherini, (akaaga akiwa mnyonge, aliamini kuwa mwanae Livingstone ana mafanikio zaidi ya Gosbert)
Baada ya kuondoka, yule jamaa watatu akamuuliza baba Gosbert; Hivi kumbe ka Gosbert kamesoma eeh!
Baba Gosbert:...ah, kapumbavu sana kasome wapi? Kameishia kuchimba makaburi tu!