North Korea yarusha kombora

ze kokuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
7,476
Reaction score
9,654
Korea kusini imeeleza kwamba Korea kaskazini imerusha makombora kadhaa ya masafa mafupi,hayo yanajiri baada ya mazungumzo ya kuondoa silaha za kinyuklia na Marekani kuvunjika.

Makombora hayo inaelezwa kwamba yaliruka umbali wa 70km hadi 200 kabla hayajaanguka baharini katikati ya Korea kaskazini na Japan.

Marekani imeeleza kwamba inafahamu kuhusu tukio hilo huku waziri wa Mambo ya nje wa Marekani akizungumza na simu na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Korea kusini na Japan.

Jaribio hili la kombora litakua ni la kwanza kwa Korea kazkazini tangu mwaka 2017 ambapo ilikua Mara ya mwisho nchi hiyo kurusha makombora.

https://www.google.com/amp/s/www.nytimes.com/2019/05/03/world/asia/north-korea-missile.amp.html
 
Marekani kishaona bwana kiduku ameshakaa kwenye 18 ndio maana anamzingua kwenye mazungumzo na bwana kiduku anarusha makombora kumkomvisi tramp warudi waongee lakini wap amechelewa.... Vikwazo vimeshataiti..... Waziri wa ulinzi aliyejiudhuru Bwana JAMES MATTIS Alimwambia kama unataka ushuhudie moto ambao haujawahi kushuhudiwa toka dunia kuumbwa arushe hata jiwe kwenye kisiwa chenye kambi kubwa ya marekani cha GUAM bwana kiduku mpaka leo anambwela....
 
Uko sahihi Mkuu....watu wake wanakufa njaa huko anarusha viroketi kusudi ili aonekane na Marekani apate nafuu ya vikwazo lakini Marekani wamemkazia
 
Uko sahihi Mkuu....watu wake wanakufa njaa huko anarusha viroketi kusudi ili aonekane na Marekani apate nafuu ya vikwazo lakini Marekani wamemkazia
Usisahau pale Marekani alipopeleka machumachuma yake kwenye rasi ya Korea. Na akaanza kutoa vitisho vingi tuu.
Lakini kiduku akamwambia arushe tu japo jiwe aone cha moto...
Marekani akaondoa machuma yake na akasingizia kwamba yalikuwa yanapita tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…