Nombeni ushauri wa kiutalaam wana JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nombeni ushauri wa kiutalaam wana JF

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Ras, Jul 14, 2010.

 1. Ras

  Ras Senior Member

  #1
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina laptop yangu Toshiba m50 Window 7 premier. Nilikuwa nikiiwasha inaleta black screen kwa muda na maandishi mengimengi hivi then inawaka, lakini leo imeleta hiyo screen nyeusi na kuandika CD-ROM BOOT PRIORITY ...........NO MEDIUM halafu haijaendelea kuwaka nifanyaje Wakuu?? Je ni nini tatizo hasa?? Naomba ushauri wenu Wakuu.:frusty:
   
 2. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Nitaaanza kwa kujaribu kufafanua kwanza hilo neno CD ROM BOOT PRIORITY....

  Kwa kawaida Computer huwa ina kitu kinaitwa BOOTING SEQUENCE PRIORITY(inaweza ikatumika lugha nyingine ya kitaalam zaidi) ila kwa maana nyepesi ni kuwa Unapoiwasha computer yako mtiririko mzima wa system kuweza kuwaka mpaka mahali ambako user wa kaiwada anaweza kuanza kutumia (tunaita Booting systeam) ni huwa wa namna hii....

  1. kwanza Computer inapowaka kitu cha kwanza inachofanya ni kudisplay details za mfumo mzima wa computer na uwezo wake ulivyo.....(ndio yale maandishi unayoyaona yanayotokea kwenye black screen(tunaweza kusema inaitwa booting procedure) yale maandishi yanaweza kukuonyesha uwezo na speed ya computer yako vilevile na version y BIOS system yako na Booting procedure hii inatanguliwa na kitu kinachoitwa POST(power on self test)kama kuna failure yoyote ya attached device(mouse keybord,harddisk, RAM,cd rom na hata CMOS battery) basi hapo ndipo utakapokujulisha kuona tatizo liko wapi (mara nyingi ni kwa lugha ya kiufundi zaidi kwa hiyo unaweza usielewa kama sio mtaalam wa maswala hayo hasa kwa kesi ya RAM na HDD)...

  ikiwa mashine yako iko sawa basi unaweza ukasikia single beep ...sometimes double beeps(sio kwa computer zote zingine hazitoi Beep) kuashiria everything is OK na computer inaendelea KU load OS(operating system)

  BOOTING PROCEDURE NA OS LOADING......
  Hints:
  OS(operating system) - E.g Windows XP, windows 7, Ubuntu(linux)
  Hard disk/hard drive(HDD) - ni kifaa cha kutunzia files na programs zote zinazopatikana kwenye computer.. kwa lugha nyepesi ndio (container) au tumbo la computer... kila unachofanya kinahifadhiwa humo unit yake ni kwa KB,MB,GB,TERA

  RAM - Random Access memory - Hapa tunaweza kusema ndio play ground ya kila activities ya computer.. kwa mfano rahisi tunaweza kusema ndio ndio mahali pa kufanyia kazi kwa programs zako (maelezo zaidi chini) unit ni MB

  CPU( central proccessing Unit) a.k.CPU clocks a.k.a proccessor - Hiki kifaa ndio BRAIN OF COMPUTER...... idea na mhimili mzima wa computer uko hapa..na ndio sifa ya computer ilipolalia( kama vile kwa ubongo au brain ya mwanadam) pasipo hii computer is consider to be useless(typical dead) NB: ingawa computer ni muuonganiko wa vifaa vinavyotegemeana) hiki ndio kifaa kinachoprocess activities(request) zote zinazoingizwa na ku zidisplay kupitia screen kwa usahihi na kwa wakati muafaka (acuracy and speed) unit ni kuanzia Mhz , Ghz na kuendelea

  BIOS (basic input/output system) - it is a set of instruction that tells computer how to start

  HOW COMPUTER START UP AND GETTING READY TO USE...

  Bila kujali ni aina gani ya OS inatumika ... unapobonyeza kitufe cha ON katika computer yako ... itaanza kufanya POST kuangalia kama kuna missing au defected device yoyote ambayo itaathiri utendaji wake... baada ya kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa pamoja na setup nzima ya BIOS hapo computer kwa kutumia some integrated programs itaload OS kutoka kwenye HDD na kuipeleka kwenye RAM tayari kwa matumizi(mind u RAM its a play ground)... na hili linafanyika kwa kila program unayofungua... ni lazima iwe loaded kwenye RAM ili uweze kuitumia ... na unapoizima inarudishwa kweney HDD na kuwa saved hapo.. ndio maana hatuzimi Computer kama RADIO au TV kwani kufanya hivyo ni kusababisha LOADED programs zisiwe retained kwenye HDD na kuwa saved hapo(ingawa baadhi ya computer za kisasa zinauwezo wa kurecover demaged files incase power fault occur)

  Sasa ikiwa basi computer itagoma kuendelea ku load OS mara baada ya POST kuna sababu mbalimbali iznazoweza kusababisha

  1. OS NOT FOUND( had disk fault au imekufa au haipo kabisa au OS haijawa installed)
  2. RAM MISSING ( RAM imekufa au haipo kabisa)
  3. SYSTEM FILE corrupted ( Files za OS zimekuwa corrupted na zinahitaji kuwa re installed)
  4. BIOS SETUP MISCONFIGURED (BIOUS setup zimekuwa misconfigured au corrupted)
  na sababu nyingine nyingine nyingi.......................

  Hitimisho

  kwa kesi ya laptop yako inaonekana kuwa computer imeshindwa kuiona Booting system files za OS yako kutoka kwenye HDD yako... hii inaweza ikasababishwa na kuwa HHD hajatambulika kwenye mashine yako.. (labda laptop ilipata mushlkeli kidogo na kusababisha hadrware error mfano kuigonga au kuanguka au power fault) kwani kwa kawaida ilitakiwa iende kwenye option ya pili (HDD) kutoka kwenye ya kwanza (CD ROM)

  kwa kaiwada booting sequence ya computer huanzia 1.CD ROM ---> 2.HDD - 3.NETWORK 4. EXTERNAL MEDIA (sequence hii sio kwa computer zote) ila hizo mbili za kwanza (1. CD ROM ----> HDD) kwamaana ya kuwa computer itaboot kupitia CD ROM ikiwa tu kama kuna BOOTING MEDIA ndani ya CD ROM (kwa mfano WINDOWS XP OS CD, WINDOWS VISTA OS CD) na kama haipo computer itakwenda kwenye option ya pili yaani HDD ... hapo sasa kwa kuwa tayari HDD yako inakuwa installed na OS basi computer ita boot kupitia hapo ( NB: booting kupitia CD ROM ni kwa ajli ya Technical issues tu ndio maana ikawa ya kwanza unaweza ukachange iwe ya pili au ya mwisho... ili computer yako ianzie kwenye HDD moja kwa moja..

  CHA KUFANYA

  mara nyingi computer inakupa option wakati inawaka (pale kwenye black screen) mfano.. press f1 or f2, or del, or ALT-DEL or SHIFT-F2 or f12 or f10 orCTRL-ALT to enter (BIOS) setup ...(angalia ya kwako imekupa opt ya key ipi ipi kati ya hizo keys) then ukishaingia kwenye BIOS setup tafuta BOOTING sequence then unaweza ukare arange kufuatana na maelekezo ukimaliza save and exit (fuata maelekezo) then computer ita restart.. kama bado rudi kwenye SETUP nenda kajaribu kuload DEFAULT CONFIGURATION" (fuata maelekezo utaona ilipo "default config" kwani BIOS zinatofautiana siwezi sema yako ikoje


  NB: wakati mwinginebaadhi ya computer inakataa kuendelea kuload systm files ikiwa kama umeiwasha wakati kuna CD ndani ambayo sio ya Bootable CD... mathalani cd ya music, video na e.t.c... mfano kwa kesi kama yako angalia kama hujasahau cd ambayo sio bootable ndani ya cd rom/ dvd rom....

  naaamini nimejaribu kwa mapana yangu...... all the best  Computer ufanyaji kazi wake kwa lugha rahisi tunaweza tukaufananisha na mwili wa binaadam kwa maana ya kuwa viuongo vya mwili vina umuhimu sawa kinapopungua kimoja au kuwa na hitilafu basi madhara ni ya kiasi kilekile...
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Ras naona Fredwash amemaliza; fuata maelekezo ukishindwa rudi jamvini
   
 4. Ras

  Ras Senior Member

  #4
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu NASHUKURU SANA. Ngoja nifanye kama ulivoagiza. BIG UP Man!:peace:
   
 5. Ras

  Ras Senior Member

  #5
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poa Man. Guidance.
   
 6. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Maelezo mengi na mazuri........! Simply mwambie aende kwa fundi au m-chat one to one wakati anaiwasha uweze kumwelekeza stepwise kulingana na yanayojiri.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hiyo Inaa maana oshiba yako inashidwa kuona Boot Sector iliyokuwepo kwenye HHD. Jibu rahisi kwa haraka haraka tatizo itakuwa

  • Either OS yako ya windows7 imekuwa corrupt.- reason kama vile virus ,uproper shut down, etc
  • Au HDD( Hard Disk Drive) yako imekufa au ina bad sector kwenye boot sector- imewahi kudondoka chini ?
  solution

  1. Kama unayo CD ya Window 7 ingiza kwenye DVD/CD rom drive jaribu kufanya repair ya window 7 yako
  2. Hakikisha HDD iko detected unavyowasha mashine press nadhani F2- kama una utundu soma soma maelekezo uone kama HDD iko detected na sequnce ya kuboot iko sawa.- Kuna mtaalamu kakueleza
  3. Go to toshiba website an check kama kuna FAQ ya tatizo lako na solutiona yeke kwenyekitengo cha support.
  4. Nitafute nikussuport online katika charge ya ya shilingi 500 kwa saa.teh teh teh
  5. find a PC doctor

  Good luck
   
 8. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60

  Yeah kaka i thought about it..... lakini nikagundua na hizi kazi zetu za kutafuta uji wa watoto zilivyo...inaweza ikawa shida kupata convinience time kati yangu na yeye... ila la kwenda kwa fundi ni kweli nilitakiwa niongeze kuwa akishindwa apeleke kwa wenye ujuzi wao...

  NB: niliweka maelezo yote hayo on purpose coz nilijua someday somebody else anawea akafanya references flani flani ... hata pa kuanzia... kwani kama alilileta jamvni basi walau hata majibu pia yaonekane jamvini kwa faida ya wanajamvi

  thnx anyway for ushauri... well noticed
   
 9. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  charge ya 500 kwa saa.....teheteheteeeee haya bwana mjasiriamali... at least bei zako ni za walalahoi hahahahhhhhhhh
   
 10. Ras

  Ras Senior Member

  #10
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa ushauri mkuu, ningekuwa Bongo ningekutafuta mzee walau nikupe kitu kikubwa zaidi ya hiyo 500 hahahaa. Bahati mbaya nipo mbali mwana but hope one day YES tutaonana. Hii pC niliinunua huku Asia unajua tena pc zao zinakuwa kwa lugha yao so nilibadili nikainstal Window 7 ambayo unajua tena niliipata kijanja kwa kudownload vile original cd yake ilikuwa kwa lugha ya huko. May be pia ndiyo tatizo. PLEASE NAOMBA KAMA WAWEZA KUWA NA WINDOW 7 NISAIDE HAPA MZEE KWANI HUKU NILIPO NI VIGUMU KUPATA ENGLISH VERSION. Guidance Man.
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Umejaribu kutumia google translator kutafsiri hiyo lugha. kama alivyokuambia fredwash washa mashine bonyeza f2 au f12 kama sikose kwa toshina sina uhakika. Lugha yeyote iyakotokea itafisri na uafuate maelekezo aliyokupa jamaa. ukiona usumbufu basi anza moja

  Kutoka ka ugumu wa mazingira uliyopo nakushauri tumia WIndows XP. inawezekana katika kufanya update online Microsoft waligundugua hiyo ni pirated version na sometime kuna update nyingine sio update as such kwenye window7 ni file za ku verify na validate OS.

  Kwa windows XP na hata ikiwa pirated u will receive all online update without a problem. Kama una sehemu una network nzuri unaweza kupara image na CD ya windows kwenye site inatwa piratebay.org Binafsi nitaanz akutumi widnows7 next year wachina na warusi wakishakua na njia salama zaidi ya kuinstall Window7

  Kama unataka Window XP- Windows XP Professional SP3 Activated [2010] - [GuruFuel] (download torrent) - TPB

  kama unataka kuendelea na window 7english - Windows7 Ultimate x86 with working activators and Office2007 (download torrent) - TPB

  NB: Kuna link zaidi ya hizi kama una muda na umewahi kutimia torrent site au file sharing site utajua namaanisha nini. Nimeweka hizo mbili kukupa mwanga but unaweza kuapatalink zaidi ya hizo.

  Assumptions

  • Kudownlod hizo file kutoka hiyo site inabidie pc utayotumia iwe installed na application za kudowloand kama Uttorent au Bittorent au nyingine
  • uwe na internet connection wich you have ndo maana umeweza kupost problem
  • File utakazodowload zitakuwa kwenye image/ISO. Assumption ni kuwa unajua procedure za kuchoma image file to CD na una una kompyuta ambayo DVD rom yake inakuruhusu kufanya burning.
  • Kama unakwenda kwa ption ya kuinstall window7 stage ya kuistall window7 ikiisha itabidi utafute kitu inaitwa window7 loader/activator ya kuondoa alert na warning validity ya hiyo OS.

  Namna gani vipi shusha email yako ya yahoo unaweza kufanya voice call au interactive chat seesion
   
 12. Ras

  Ras Senior Member

  #12
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAWASHUKURU SANA WANAJF zaidi zaidi Mkuu pale Mtazamaji na Fredwash ushauri wenu wa kitaalamu umeniwezesha kutatua tatizo. Big up Wakuu twahitaji vichwa kama ninyi Bongo. Tatizo lilikuwa kama mlivyosema ilikuwa ikiboost kupitia CD-ROM sasa nimebadilisha inakwenda safi kabisa. Peace a Love Men :peace:
   
 13. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60


  well noticed bro...... this is wat keep JF alive and kicking despite all those shortcoming..... hongera kwa kutatua tatizo.........
   
Loading...