no title

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,759
2,000
habari zenu wadau wote wa jukwaa la ajira!

mi napenda kushare nanyi mawili matatu katika utafutaji wa ajira. ni kweli ajira zimekuwa shida sana nchini ukizingatia mfumo wetu wa elimu unatuandaa kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri. maisha ni magumu na sometimes yanakatisha tamaa lakini hatupaswi kuyachukia, kuna msemo unasema ukiyapenda maisha na yenyewe yatakupenda.

kwenye kutafuta ajira kuna changamoto nyingi nafikiri kila mtu anazifahamu. hizo changamoto tuzichukulie kama ni fundisho kuwa tukipata kazi tuheshimu, kuijali na kufanya vile inapaswa.
kila mtu ana matamanio ya kazi aipendayo ingawa mara nyingi soko la ajira hutupeleka kwenye kazi ambazo wengi hawakuwahi hata kuzifikiria kwa sababu yaweza kuwa tofauti na taaluma tulizosomea au zaweza kuwa chni ya matarajio tuliyokuwa nayo kabla.

hapa napenda kuwahusia kufocus ile kazi unataka. jaribu kutuma maombi kwa kazi ambayo una elimu nayo. kama umesomea mambo ya masoko tafuta kazi zinazoendana na hiyo taaluma, usipoteze njozi zako za awali za career uliyokuwa waitaka, usiifanye miaka yako uliyotumia chuo kusomea fani fulani ikawa si kitu tena. tujitahidi kutuma maombi kwa kazi ambazo tuna taaluma nazo. ukiwa ni mtu wa kutuma maombi kwa kazi yoyote na mwisho wa siku utajikuta una stress, utawaza mbona ulituma barua 50 za kazi lakini hakuna hata ulipojibiwa kumbe kati ya hizo barua 50 ni moja kazi moja tu ndio ilikuwa yaendana na fani uliyosomea.

pili usikate tamaa wala usichoke. kadri unavyosikia wenzio wamepigiwa simu kwa ajili ya interview wewe watakiwa kuongeza juhudi zaidi ya kutafuta sehemu nyingine. kutopata nafasi ya kuwa interviewed haimaanishi kwamba hujafika kiwango sababu mwisho wa siku lazma wachaguliwe idadi inayotakiwa hata kama wote mnafikia vigezo. kuwa imara na endelea kupambana.

kukaa bila kazi ni kazi kuliko kuwa na kazi. hapa namaanisha tujishughulishe, tafuta shughuli ndogo ndogo ya kuweza kukuingizia kipato kutegemea na mazingira unayoishi (hapa tunaweza jadiliana na kushauriana kama utahitaji msaada zaidi). kama unaona huwezi kabisa kujishughulisha kwa kipato tafuta hata vitabu au majarida ambayo yatakuwa yanakujenga zaidi kiakili huku waendelea na job hunting.

waswahili wanasema atafutae hachoki akichoka kashapata. ni kweli hatutakiwi kuchoka wala kukata tamaa katika utafutaji, kadri unavyoshindwa jaribu tena kwa njia tofauti. mfano, ulikuwa unatuma maombi kwa njia ya posta na hujawahi pigiwa simu,basi badilisha mfumo wa kutuma maombi. kadri unavyopata vizingiti iambie nafsi yako kwa sauti kuwa "sichoki sikati tamaa".

pia tukumbuke kumshirikisha mungu katika utafutaji wetu, kwa wale ambao bado mpo vyuoni anzeni kutengeneza network na watu waliopo makazini. kwa wale mliopo makazini msiwavunje moyo wasaka ajira.
nina mengi ya kuongea ila tu niishie hapa na niwatakie kila la heri. tukumbuke kauli mbiu "sichoki sikati tamaa"

ahsante kwa kunisoma.
husninyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Similar Discussions

Top Bottom