Referendum ni kama uchaguzi mkuu maana unahusisha watu wote nani atasimamia hiyo referendum kama ni hii hii ZEC au NEC na kama watatumia daftari la wapiga kura hili lililo na mgogoro ni dhahiri matokeo yatapingwa na upande mwingine mifano ipo mingi refer matokeo ya chaguzi zote tatu au wataita AU au UN wasimamie, kama ni serikali yetu bado serikali ni sehemu ya tatizo badala ya kutibu itazidisha tatizo.
Ninachoiomba CCM iheshimu maamuzi yeyote ya Wawakilishi kwa sababu wako pale kwa mujibu wa sheria na wanawakilisha watu vinginevyo watatufanya tuanze kuamini kuwa chombo cha wawakilishi ni kama bendera tu na kipo pale kutimiza malengo ya CCM na si ya wazanzibari.
Nani atatuhakikishia kuwa matokeo ya referendum hayatakuwa-tempered ku favor upande mmoja. Nia ya unity government ni kuondokana na ukiritimba wa ZEC na vyombo vyote vinavyosimamia chaguzi mbali mbali ambavyo haviaminiwi na CUF kama CCM bara wanaona ni lazima kuwe na referendum basi atafutwe msimamizi ambaye atakubalika na pande zote ili matokeo yawe fair kwa wote.
Kama wataogopa referendum kwa sababu TU, ya kutoamini usimamizi wa matokeo ya referendum hiyo, maana yake hata uchaguzi utakaotoa mshindi na mshindwa ili waungane kuunda serikali ya mseto hautafanyika kwa amani sababu ya kuogopa matokeo kuwa tampered.
Serikali ya mseto siamini itasababisha aliyetangazwa kushindwa hata kama anaamini kashinda atakubali kujiunga na serikali kwa sababu tu ya mseto huo? Siyo kweli hata kidogo bado atataka yeye ndo aongoze serikali hiyo.
Si ajabu pamoja na sheria hiyo kuundwa serikali ikashindikana sababu ya mambo hayo, kama ilivyowahi kutokea wajumbe wa baraza la wawakilishi wa CUF walivyogoma kushiriki vikao sababu ya madai fulani fulani licha ya kuwa walikuwa washindi katika majimbo yao.
Katika hayo lazima kuamini katika usimamizi, uwe wa referendum au uchaguzi kama itaamuliwa hivyo, au vyovyote vile itakavykubalika kuamini USIMAMIZI HAKUKWEPEKI, vinginevyo hamna lolote.
Asalaam Aley-kum. Niko ndani ya Ukumbi wa Baraza La Wakilishi hapa Zanzibar kwenye Mkutano wa Kumi na Nane, Kikao cha Saba.Niko kusikiliza mjadala juu ya Uanzishwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Mhe. Aboubakar Khamis Bakari tayari ameshaiwasilisha mezani. Ataisoma na itafuatiwa na majadilino.
Nitawaletea ile michango tuu yenye nguvu za hoja, na ili kubalance, hata michango ya hoja za nguvu, pia nitawaletea
Hivi sasa ndio Mhe anashuka na hoja yenyewe.
.
that is why I'm saying.. we can not govern by referendums! What if the people of Kilimanjaro would like to have a referendum to create their own little republic? What about the people of Mtwara who would like to have a referendum to decide if they want to be part Tanzania or to be part of Mozambique? What about people in Kagera who would also want to have a referendum?
Kama tunawakubalia Zanzibar kufanya referendum ya kubadilisha mfumo wa utawala kwa sababu ya kura ya wengi wape, kwanini tuwatakalie watu wa mikoa hiyo wakija na hoja zao?
Itakuwaje kama suala la Kadhi nalo likataka liamuliwe kwa referendum? why not?
Itakuwaje kama CCM watakuja na wazo la referendum kuamua (kama walivyofanya kwa makosa) kama Watanzania wanataka kuendelea na mfumo wa vyama vingi au kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja? Itakuwaje kama referendum hiyo ikapita kwa asilimia 80? should we then go back to single party state?
It is a stupid idea and I'm sorry to be the first one to call it as such!
If we agree on a principle that politically divisive issues need to be resolved by referendums then we should carry that principle to its eventual logical conclusion.
Aisee hii ni very poor argument ndugu!
Huwezi kulinganisha mtwara, iringa kilimanjaro na Zanzibar
Zanzibar ni Nchi uliyounganishwa na Tanganyika..sitegemee watu wa kilimanajro watake referundum agh!
Hii colonial thinking kwamba zanzibar ni sawa na mkoa ndio maana nawaunga mkono wazenj wajitenge na bara, maana sipendi kukaa kwenye nchi inayo colonize nchi nyingine kwasababu ya powers zake!
Nakala ninayo, kuscan hapa ZnZ ni issue. Maalim hayupo ukumbini, ila wageni ni wengi, wakiwemo wazungu wazungu ambao nadhani ni wanabalozi.asante pasco kwa habari hizi na umekuwa msaada mkubwa kwa JF kuhusiana na habari kama hizi. Kazi yako nini wewe maana mikutano yote unatuletea mambo live. Dodoma hujaenda?
Pata nakala ya hiyo hoja ili tuscan basi.
Maalim Seif yupo ukumbini kufuatilia hoja au msaidizi wake Jussa?