Ni kweli njaaa kwani haiwezi kukutoa sehemu moja kwenda nyingine. Sema kama unaakili unaweza kukupa starter ya kutafuta kikubwa tofauti na umemaliza chuo wazazi wameuza kila kitu usome na wewe ndo tegemeo kubwa halafu na wewe ndo unaishi kwa hiyo laki 5.5
Ukipata hiyo kazi unaingia mkopo unaanza kufanya biashara.
Kuna kijana mmoja alipata ajira ya ualimu alifanya Kazi miaka 3. Tu baada ya kuthibitishwa kazini akaingia mkopo wa milioni 8 kama sikosei akatokomea mazima baada ya hapo wakamwamdikia utoro wakamfukuza Kazi.Akaenda kuwekeza kwenye mbao huko.Sasa hivi ni anahela hatari.
Sema tu changamoto ajira inalemaza akili wengi wanaona bora kidogo kuliko kutake risk