Teknolojia
Itifaki
Makala kuu ya: Internet Protocol Suite
Ugumu wa miundombinu ya mawasiliano ya Intanet unahusisha vipengele vya vifaa vyake na sehemu za mfumo wa progamu inayodhibiti tabaka mbalimbali za usanifu. Ingawa vifaa vinaweza kutumika kusaidia mifumo mingine ya programu, ni urasimu na mifumo ya sheria za
usanifu wa programu zinazoainisha Intanet na hutoa msingi wa ukubwa wake na mafanikio yake. Wajibu wa urasimu wa usanifu wa mifumo ya programu za Intanet umepewa tume ya uhandis wa Intanet (IETF). [SUP][8][/SUP] IETF huongoza makundi ya kuweka sheria, wazi kwa
mtu yeyote, kuhusu masuala mbalimbali ya usanifu wa Intanet. Majadiliano yanayotokea na amri za mwisho huchapishwa katika mfululizo wa machapisho, iitwayo Kuomba kwa Maoni (RFC),ipatikanayo bure kwenye tovuti ya IETF . Mbinu muhimu za utengenezaji wa mitandao zinazowezesha Intanet ziko katika RFC teule yenye sheria za Intanet.
Sheria hizi hueleza msingi unaojulikana kama Itifaki ya Intanet. Hii ni kielelezo cha usanifu unaogawanya huduma kuwa visehemu katika itifaki ya mfumo(RFC 1122
, RFC 1123
). Visehemu hivi vina uhusiano na mazingira au upeo ambao huduma zao hufanya kazi. Sehemu ya juu ni
Sehemu ya zana, nafasi iliyotengwa kwasababu ya mbinu za utenegnezaji mitandao zinazotumika katika zana za programu, mfano, kivinjari. Chini ya sehemu hii ya juu, kuna sehemu ya
Usafiri iunganishayo zana katika
kompyuta tofautikupitia mtandao
(mfano,
client-server) na mbinu sahihi za kubadilishana takwimu . Chini ya sehemu hizi ndipo kulipo na msingi wa teknolojia ya mitandao, linalojumuisha sehemu mbili.
Sehemu ya Intanet inayowezesha kompyuta kutambuana kupitia
anwani za Itifaki ya internet(IP), na huziwezesha kuungana pamoja kwa kutumia mitandao zilizo karibu. Mwisho, chini ya usanifu huu, ni sehemu ya programu , na
sehemu ya uunganishaji, ambayo huwezesha kuungana kwa kompyuta
zilizo katika kiunganishi sawa wa mtandao ya mtaa , kama vile mtandao wa eneo
(LAN) au
uunganishi wa kupiga. Mfano huu, ujulikanao pia kama
TCP / IP, ni iliyoundwa isitegemee vifaa inavyotumia, kwa hivyo mfano huu hauna haja ya kujishughulisha na maelezo yoyote. Mifano mingine vimeundwa, kama vile
mfano wa mifumo ya kiunganishi
kilichofunguka (OSI) , lakini si sawa katika maelezo ya ufafanuzi, wala utekelezaji, lakini kufanana kupo n itifaki ya TCP / IP hujumuishwa katika majadiliano ya mitandao ya OSI .
Sehemu maarufu zaidi ya picha simamizi ya Intanet ni Itifaki ya Intanet (IP) ambayo hushughulikia upeanaji wa (anwani za IP) kwa kompyuta zilizo katika Intanet. IP inawezeshaushikanishaji wa mitandao na
kimsingi hujenga Intanet yenyewe. Toleo ya 4 ya IP (IPv4) ni toleo lililotumiwa katika kizazi cha kwanza cha Intanet ya leo na bado yatumika vikubwa. Iliundwa kushughulikia hadi watumiaji billioni~ 4,3 (10 [SUP]9[/SUP]) wa intanet. Hata hivyo, kulipuka kwa ukuaji wa Intanet
umesababisha kuisha kwa anwani za IPv4 ambayo inakadiriwa kuingia hatua yake ya mwisho katika takriban mwaka wa 2011. [SUP][9][/SUP] Toleo ya itifaki mpya, IPv6, iliundwa katikati ya mwongo wa 1990. Toleo hili linauwezo mkubwa wa kupeana anwani na mbinu bora zaidi ya uelekezaji wa trafiki ya Intanet. IPv6 kwa sasa ipo katika awamu ya kuachiliwa kibiashara duniani mashirika ya kuweka anwani za
intanet(RIR)yameanza kuwahimiza mameneja wote wa rasilimali kupanga uchukuzi na uongofu wa haraka. [SUP][10][/SUP]
IPv6 haishirikiani kikazi na IPv4. Kimsingi toleo la IPv6 hutengeneza toleo "sambamba" la Intanet ambalo halipatikani moja kwa moja na IPv4. Hii ina maanisha uboreshaji wa Programu au vifaa vya ukalimani ni muhimu kwa kila kifaa cha mtandao ambacho linahitaji
kuwasiliana kupitia Intanet ya IPv6. Mifumo ya kuendesha kompyuta ya kompyta za kisasa tayari vimebadilishwa ili vifanye kazi na toleo zote za itifaki ya Intanet. Miundombinu ya mtandao , hata hivyo, bado yamebaki nyuma katika maendeleo hayo. Mbali na tata za viungo
vinavyotengeneza miundombinu yake, Intanet imewezeshwa na mikataba ya kibiashara (mfano, mkataba wa kujitakia), na kwa ufundi maalum au itifaki zinazoeleza jinsi ya kubadilishana data kwa kupitia mtandao. Hakika Intanet ina ainishwa na viungo vyake na sheria za uelekezaji.