NMB kupata faida inayovunja rekodi zote ya TZS 775 bilioni ni matokeo ya Sera chanya na rafiki za kibiashara za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Yes Mama Samia na Ruth Zaipuna ni kama mapacha kwa performance nzuri wanazoonesha
 
Ukienda kupekua Financial Statement yao
utakuta interest za mikopo ipo juu way of accepted risk tolerance, unnecessary service charges kwa wateja for banking with them (dhulumati tu). But that’s not the pudding on the cake.

Faida kubwa utakuta mambo yote aliyokuwa anapingana nayo Magufuli yamerudi. Hela za mashirika zilizokuwa zinaenda hadhina sasa utakuta zimerudi bank. Hela zake yenyewe ndio serikali inakopeshwa through short term loans with high interest, hela hizo hizo za serikali bank inanunulia government securities na kuvuna interest ya faida na kuna ongezeko la hayo manunuzi.

Wakitoka hapo wanakwambia mama anaupiga mwingi uchumi umekuwa, angalia sasa mikopo ya kibiashara (ambayo ndio inakuza uchumi) utakuta ni sehemu ndogo ya faida yao. Hela ipo serikalini tu huko ndio watu wanapenda kufanya biashara.

Ni watu wa hovyo tu ndio walishindwa kumwelewa Magufuli, nchi inachezewa sana.
 
Ms Ruth Zaipuna mama wa mihela

Tunapomsifu Rais kwa Sera rafiki tusiache kusifu pia juhudi kubwa na nzuri za huyu Mama kama Mkurugenzi Mkuu,

Huyu Mama anafanya juhudi kubwa sana kuhakikisha Benki inakuwa katika uelekeo sahihi,

Hongera Rais Samia hongera NMB ya Ruth Zaipuna
 
Kuna kitu naona hukijui,

Akaunti nyingi za serikali ziko hazina,
 
Mabenki yanatuibia sana
 
Kuna kitu naona hukijui,

Akaunti nyingi za serikali ziko hazina,
Haya tupe breakdown ya amana za wateja wao zilizo bank kati ya individual, businesses and government institutions. Kuona nani ana hela nyingi huko.

Breakdown ya faida inayotokana na interest kati ya mikopo kibiashara, government ‘loans and security’ na interest nyingine (tuone ipi ina mchango mkubwa kwenye faida yao).

Ni hivi ukiangalia sehemu kubwa ya faida yao utakuta ni watu ambao wana-balance budget zao za maisha kulipa ada, rent na other living expenses (hawa awazalishi kwenye uchumi),.Wengine wanaowapa faida ni kufanya biashara na serikali.

Lakini mchango wao katika sector ya viwanda ni mdogo sana, prove me wrong.

Source nyingine ya hela zao ni charges za hovyo kwa wateja (ambazo zinatakiwa kuongelewa) na foreign exchange (zama za kutakatisha hela za ngada). Lakini si kusema kuna ubunifu wowote wa huyo mama kwenye hiyo faida.
 
Mimi sio staff wa Benki yoyote lakini ninazo kumbukumbu kuwa akaunti zoteza Serikali ziko BOT,

Huku kwenye mabenki wamebaki na operational money.


NMB nadhani wanastahili pongezi better wapongezwe tu
 
Mimi sio staff wa Benki yoyote lakini ninazo kumbukumbu kuwa akaunti zoteza Serikali ziko BOT,

Huku kwenye mabenki wamebaki na operational money.


NMB nadhani wanastahili pongezi better wapongezwe tu
Kuna faida ndio atukatai

Hila kama msingi wenyewe wa faida ni monopoly ya kupokea mishahara halafu kukopesha hao watu at rates ambazo unchallenged na wafanyakazi hawana option ya ku-shop around for better deals on the banking market. Sasa hapo unapongeza nini.

Serikali uweke hela ununue bond zao, uvune interest kama sehemu ya faida unapongeza nini, au hela hizo hizo uwakopeshe short term loans with high interest unasifia nini.

Info zote hizo zipo kwenye ‘income statement’ yao na break down ya hizo income sources on notes.

Hakuna ubunifu wowote kuna market monopoly tu inayowapa faida na government savings za kuzungusha. Na faida yao aina impact kubwa kwenye kukuza uzalishaji wa sector binafsi.

Sasa mtu ana hitimisha vipi uchumi umekuwa kutokana na faida za MNB hawa ndio watu wanaomuongopea raisi kwa maslahi yao.
 
Bank kupata faida kubwa ni ishara ya ukuaji wa uchumi kuwa ni WA kuridhísha
 
Wewe zione tu Ni nyingi. Gawio la serikali mafisadi wanalisubiri wawape wake zao wakanunue chupi Dubai.
Tatizo pale hazina pakacha linavuja, sio kwamba hela hauingii.
 
Rais siamtoe Mwigulu pale aende huyu dada wa NMB inchi ipae kiuchumi?!
 
Huyu dada anagonga vichwa vya wengi kwakweli kwakasi kubwa ya ukuaji wa bank ya NMB
 
Acha wivu hata kabla ya Mwenda zake wafanyakazi wengi walikuwa NMB Sema mwendazake aliwatimua Wazungu akaweka wabongo kwenye top management
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…