Jikatae mapema sana dogo kabla hayajakukuta makubwa. Mademu wengine wakiwa na kaelimu kidogo alafu wewe ni wa kitaa tu wanakuona sio taipu yao ila anakusaidia tu ipo siku atakuonesha laivu aliye taipu yake so jiondoe mwenyewe kabla hujakwangua viakiba vyote. Kuna rafiki yangu yamemkuta hayo kaangaika kuiba visenti vya baba yake mpaka kafirisi ofisi demu alikuwa anasoma mipango Dom jamaa kila wkend anampandia mwisho wa siku katambulishwa rasmi 'mwenye mali' ukouko Dom karudi mpoleee, kwa sasa jamaa kachanganyikiwa kabisa na mdingi kamtimua ofisini anazugazuga tu mitaani.