Njooni tuelezane jinsi ulivyokosea kutuma meseji

knows

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,403
2,006
Habar wakuu
Naimani mkopowa wote haya njoeni tusimuliane.

nikikumbukaga nacheka sana kipindi niko chuo hiyo siku nilikosea kutuma text nilikuwa nachati na mubebe unajua zile text za malavdav sio powa sasa bhana katika kuchati nilikuwa nachati na watu wawili katika kutuma sasa si ndio nikakosea kuja kushtuka text nimeituma kwa Mama bwaaana weee asikwambie mtu babu nilitamani kama ningekuwa nina uwezo wa kuikimbiza ile message niikimbize kama SuperMan niikamate isiende lakini wapi ndio kwanza ngoma inarudisha delivered yaani kwa kunihakikishia ulichotuma kimefika.

Hapohapo nikazima na simu wenge kama lote akili ishavurugika Usifanye masihara nikasema kivumbi leoo kuwasha simu naona sio kweli nikakaa baadae nikaona haina maana ni bora niwashe tu simu eebhana ile nawasha tu ngoma inaita kucheki Mama daah ila niliyamaliza yakaisha japo haikuwa rahsi nilikomaa kiume.

Nakumbuka tena kuna siku nipo na jamaa yangu sana na yeye alikuwa anachati siku moja tumekaa katika kuchati kwake kumbe alikuwa anachati na mwanamke wake hapohapo pia anachati na mchepuko bhaana si akajichanganya message ya mchepuko akatuma kwa mwanamke wake nilicheka sana sikuiona jamaa ujanja wote mfukoni maana kilinuka balaa lake lilikuwa zito jamaa alitamani kulia ilibidi nimsaidie kiume kesi nikabeba mimi mpaka tunalimaliza lile valangati mwamba yuko makini siopowa.

Tupe na wewe ya kwako ilikuaje msala wako wa kukosea message.
 
'sio kila mwanaume anayeweka mikono mfukoni anahesabu hela, wengine wanarekebisha mapumbu yao'.

Mwanamke wangu mmoja alikosea hiyo message badala ya rafiki yake, akamtumia baba yake. Ule usiku hata K hamu ya kunipa ikawa hana. Nilimuhurumia lakini niliishia kucheka sana.
 
😂😂😆😆😆
 
Kuna kiasi cha pesa nilimtumia mchepuko sasa baada ya kutuma nika muandikia meseji kama ameona hiyo pesa kuja kushtuka delivery ripot imetua kwa wife na nilikuwa nimeandika "nimekutumia my umeona " fasta akili kubwa ikacheza nika mtumia muamala mwingine wife ili kuzuga na nika mwandikia sms nyingine kwamba kuna fundi atakuja home mta mpatia iyo pesa..
ikawa imepita hivyo ila nilikuwa naumbuka siku hiyo.
 
Hapa kama aliingia kingi MKuu huyo manzi niwakuweka ndani fasta Maana ni kiazi enough to be into da marriage
 
Back
Top Bottom