Njombe: RC Christopher Ole Sendeka ang'aka akitaka kujua milioni 44 zimetumika kufanya nini?

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amemuagiza Internal Auditor wa mkoa pamoja na Mhandisi wa mkoa wa Njombe kuanzia leo kukusanya taarifa za ujenzi wa jengo la shule ya msingi ya Msimbazi ya mfano iliyoko wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe na kutumia kiasi cha shilingi milioni 44 wakati jengo hilo likijengwa chini ya kiwango.

DSC_4943.jpeg


"Naagiza kuanzia leo internal auditor wa mkoa na mhandisi wa mkoa anzeni kazi ya kukusanya taarifa ya jengo hili nisaidiwe kujua milioni 44 zimetumika kufanya nini, kununua nini na ndani ya awamu hii bado kuna watu wanajenga kienyeji kwa namna hii? Hawana kumbukumbu za ujenzi, hawafanyi kazi kwa kiwango na wala kumbukumbu hawaziweki" Olesendeka alisema.

Wananchi wa kijiji cha Msimbazi wameonesha kuunga mkono agizo la Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutoridhishwa na ujenzi uliofanywa na mkandarasi huyo na kuiomba Serikali kuchukua hatua stahiki dhidi ya waliofanya udanganyifu. "Sisi kama wanakiji kwa kweli haturidhiki kwa kazi hii kama mkuu wa mkoa ambavyo hajapendezewa kwa hiyo ni bora tu hatua zichukuliwe mapema" alisema mmoja wa wananchi.

Afisa Ufuatiliaji wa Mradi wa TASAF katika Halmashauri za Makambako, Wanging’ombe na Mbarali mkoa wa Mbeya, Edwin Mlowe amewataka wataalam wa Halmashauri wanaofanya kazi ya kusimamia miradi ya TASAF kama jengo hilo kuacha kukaa maofisini na badala yake ni vyema wakajiridhisha na ujenzi wa miradi inayoibuliwa na wananchi.

"Ni muhimu sasa wataalamu wa Halmashauri kujiongeza kwa maana ya kusimamia na kufuatilia ujenzi maana yake mafundi wakiwa site lazima hawa wataalamu waweze kufika eneo la ujenzi" alisema Edwin Mlowe.
 
Back
Top Bottom