Mwanamke aliyefahamika kwa Jina la Maselina Mtewele (50), ambaye ni Mkazi wa Mijiji cha Lwangu Halmashauri ya Mji wa Njombe, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumuua Mume wake Gwido Kigaya (59), kwa kumkata na panga eneo la kichwani.
Majirani akiwemo Magnus Mayemba na Albentina Mayemba ambao wanasema tukio hilo limetokea Machi, 18 2026, majira ya saa saba usiku, ambapo inadaiwa Mtuhumiwa alimkata kwa kutumia panga baada ya ugomvi uliokuwa ukiendelea wakati wakigombania jembe.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Johnbosco Kigae amesema mpaka kufikia mauaji, wanandoa hao walikuwa wakigombana mara kwa mara ambapo Maselina alishawahi kufanya jaribio la kumuua kwa shoka mumewe na kushindikana.
"Lakini pia kumekuwa na malumbano ya hapa na pale na wametengana muda mrefu Mke akilala peke yake na Mume peke yake na wanasema pia hata huduma ya Mume na Mke ilikuwa haipo"amesema Johnbosco Kigae.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga akiongea kwa njia ya simu na AyoTV, amethibitisha kutokea mauaji hayo na Mtuhumiwa tayari amekamatwa na upelelezi unaendelea.