Njia (route) zaidi ya 60 za daladala Dar kusitishwa...

Njia (route) zaidi ya 60 za daladala Dar kusitishwa...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
MONDAY, 31 MARCH 2014

Njia 64 za magari ya daladala jijini Dar es Salaam zitakoma kutumika kutokana na kuanza kwa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART).

Kwa kuanzia matayarisho ya kupisha mradi huo, Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (DART) umetaka wamiliki wote wa mabasi ya daladala yanayopita katika Barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo, kufika katika ofisi zake kujiandikisha.

Mhandisi wa Wakala , John Shauri aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa wamiliki hao wanatakiwa kufika katika ofisi za DART zilizoko jengo la Ubungo Plaza barabara ya Morogoro kuanzia leo hadi Aprili 21 mwaka huu kwa ajili ya kujiandikisha kama moja ya matayarisho ya kupisha mradi huo.

DART iko kwenye mchakato wa kuwezesha upatikanaji wa watoa huduma kwenye mfumo mpya wa mabasi yaendayo haraka awamu ya kwanza ambayo inajumuisha barabara ya Morogoro, Kawawa na Mtaa wa Msimbazi kwa njia kuu na nyingine za kiungo.

Alisema kulingana na mpango wa uendeshaji wa mfumo wa DART, barabara zinazohusika zitapaswa kutumiwa na mabasi ya mfumo huo pekee.

Shauri alitaja baadhi ya njia zitakazoguswa na ni pamoja na Mbagala Rangi 3 kwenda Masaki, Vingunguti kwenda Makumbusho, Kunduchi Kwenda Mwenge, na Msata kwenda Ubungo.

Njia nyingine ni Kariakoo kwenda Makumbusho, Buguruni kwenda Kawe, Kivukoni kwenda Mburahati, Mbagala Kuu kwenda Mwenge, na Mkata kwenda Ubungo. Njia nyingine ni Mburahati kwenda Muhimbili, Segerea kwenda Mwenge, Vingunguti kwenda Kawe, Vingunguti kwenda Mbezi, Kunduchi kwenda Posta, na Kunduchi kwenda Makumbusho.

Pia alitaja Temeke kwenda Masaki, Kivukoni kwenda Mabibo, Muhimbili kwenda Mabibo, Posta kwenda Ubungo, Posta kwenda Mabibo, Kawe kwenda Kimara, Kivukoni kwenda Mbezi, Mwenge kwenda Mbezi, Posta kwenda Mbezi, Mbezi kwenda Tegeta na Bunju kwenda Makumbusho.

source: Kandili Yetu!!!
 
hakika dhambi ya mnafiki ni kubwa mno,unataka ikifika asubuhiwatu wajadili hili ili iweje,hii sio siku ya wajinga bali ni ya
WANAFIKI kama wewe.
LEO NI SIKUKUU YA WANAFIKI kazi yao kutunga mambo na kuwafanya watu wajinga kumbe wajinga ni wao na ndio maana inaishia saa nne asubuhi tu
 
mleta thread tafadhali ilete hi thread kesho jioni kama ni kweli ili kuondoa hili dukuduku la siku ya wajinga.
japokuwa kama sikosei nimemuona mtu akiongea kwenye tz mida ya saa 2 usiku. ni hayo tu.
 
Hii news ni kweli ilotoka ktk tv juzi ... wenye madaladala wanaotumia njia mpya wakarepoti ili wapangiwe kwengine
 
hakika dhambi ya mnafiki ni kubwa mno,unataka ikifika asubuhiwatu wajadili hili ili iweje,hii sio siku ya wajinga bali ni ya
WANAFIKI kama wewe.
LEO NI SIKUKUU YA WANAFIKI kazi yao kutunga mambo na kuwafanya watu wajinga kumbe wajinga ni wao na ndio maana inaishia saa nne asubuhi tu
Weka akiba ya maneno!!!!
 
Hapana, hii ilitoka jana kwenye gazeti la Daily News/ Mwananchi, kanunue la jana 31.03.2014, ni habari ya kweli kabisa. By the way kwa mtu serious hii iitwayo Fools sijui Foolish Day huwa anaipotezea.
 
Hii habari ilitoka kuanzia ijumaa ya tarehe 28/03/2014 kwa hiyo ni habari ya kweli kabisa haina uhusiano na sikukuu ya wajinga..
 
Jana pia niliisikia kwa Adrian Hilary Stepp wakati wa kipindi cha HOT MIX saa kumi na moja jioni,nilmsikia Mwenyekiti wa Madaladala kama sikosei anaitwa Sabri wakiongea nae kwenye simu juu ya mchakato huo.
Pia waligusia suala la kununua hisa kwa watanzania kwenye Kampuni itakayosimamia mradi huo.
 
Hii news ni kweli ilotoka ktk tv juzi ... wenye madaladala wanaotumia njia mpya wakarepoti ili wapangiwe kwengine

Nawashangaa watu wa Dar wanaogopa kujenga vibanda nje ya mji kwa kisingizio cha usafiri

Wanadhani yote yataenda mkoani.no.yatahamia route za huko ndani ndani.mabosi wako Dar wanataka wawakabe madereva
 
Back
Top Bottom