Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,969
- 51,130
Kwanza kwenye kila uhalifu wahalifu wote huacha alama (Clue) tatizo huwa ni katika kuzitambua hizo alama. Lakini kuna watu ambao wamesomea kuunganisha mfuatano wa matukio (Connecting the dots) na kupata nadharia ya nini chanzo cha uhalifu husika.
Lakini pia wapo watu ambao huweza kuchanganua na kutengeneza nadharia (Profile) ya tabia ya mhalifu. Pia kuna watu ambao wanao weledi wa kuchanganua taarifa mbali mbali zilizokusanywa na kutengeneza mwelekeo (Lead) wa nini kilichosababisha uhalifu na nani alihusika na uhalifu huo! Kwa mtizamo huo kama na nyanja zingine zitashirikishwa bila shaka uchunguzi wa waliomshambulia Lissu utakuwa rahisi.
Njia ya kwanza rahisi ambayo kutokana na matumizi ya Teknolojia ya kimawasiliano inafaa kutumiwa, ni kufanya uchambuzi wa simu zote zilizopigwa kwa kutumia minara yote yenye kushika simu zinazopigwa eneo lililotumika kumshambulia Lissu. Kuna watu wana weledi wa kufanya uchambuzi huo.
Iangaliwe kama kati ya simu zilizopigwa hapo siku hiyo kuna simu ambazo hupigwa pia toka kwenye minara inayoshika mawasiliano ya simu kwenye nyumba anayoishi Lissu Dar es salaam. Ama ziangaliwe pia kama zinahusiana na simu zilizotumika mahali Lissu aliposema anafutiliwa na gari yenye Namba T 460 CQV.
Siku ya tukio si kwamba eneo zima la "Area "D" kulikuwa hakuna watu. Watu wa eneo hilo mtaa kwa mtaa wahojiwe kama wakati wa tukio waliona kuna gari linapita maeneo yao kwa kasi na watoe angalau maelezo kama gari hilo lilielekea wapi. Hii itasaidia kujua kama gari lile lilitoka eneo la tukio ama lilifichwa kwenye nyumba za jirani.
Kama Polisi wataweka njia salama ya kutoa taarifa nadhani kuna watu watatoa taarifa sahihi kuhusu gari hilo kwani kama inasemwa lilianza kumfuatilia tokea bungeni bila ya shaka kuna watu walioliona gari hilo likiwa limeegeshwa mahali kabla ya kuanza kumfuatilia Lissu.
Polisi wanaweza pia kutumia kurassa za Instagram, tweeter na Facebook za Mheshimiwa Lissu kufuatilia watu ambao ni wafuatiliaji wa kurasa hizo lakini wana nyendo zenye kutia shaka kwenye kufuatilia huko. Jee wiki moja kabla ya tukio kutokea kulikuwa na nini kwenye kurasa za Lissu za mitandao ya kijamii?
Jee eneo zima la mtaa anaoishi Lissu hakuna nyumba ambazo zina CCTV ambazo zinaweza kwa namna moja ama nyingine kusaidia kupata taarifa ya nini kilitokea kwenye mtaa ule? Yaani mtaa wanaoishi viongozi wetu hauna hata nyumba moja ambayo ina CCTV inayoelekea barabarani? Hii pia na kwenye maeneo yote karibu na bunge CCTV zake zitumike kukusanya taarifa.
Nawasilisha!!