Njia pekee kuinusuru UKAWA

Njia pekee kuinusuru UKAWA

Mrbwire

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Posts
200
Reaction score
53
1. Ni ubinafsi kwa CHADEMA kutaka majimbo yote ambayo upinzani una nguvu na wakati huo huo kumtoa mgombea uraisi kwa niaba ya UKAWA.

Katika muungano wowote lazima pawe na kupata na kupoteza. Kuna baadhi ya maeneo muungano utaongeza nguvu zako na kuna baadhi ya maeneo utaku-limit. Hili haliepukiki na ni practice kote duniani. (Hata muungano wetu na Zanzibar ukiuchunguza utaliona hilo dhahiri). Lazima CHADEMA wakubali kupoteza pia.

2. Mgombea Uraisi ndani ya UKAWA

Ni dhahiri kuwa kwa sasa mtihani mzito ndani ya UKAWA ni kumpata Mgombe nafasi ya uraisi....Mgombea ambaye hayupo kushiriki tuu!. Kwa sehemu kubwa ninaamini changamoto hii ni "matokeo ya mapungufu ya kiuongozi ndani ya vyama vya upinzani". Haiingii akilini kuwa ndani ya chama kama CHADEMA, na CUF bado kete pekee ni Dr. Slaa na Mbowe na Prof. Lipumba tuu!.

Tukubali ukweli kuwa viongozi "huibuliwa" na "hukuzwa" na vyama. Kama hatujatoa nafasi kwa vijana na wasomi kuonesha uwezo wao wa kiungozi na uwezo huo ukakua kufikia kujenga ushawishi si ndani ya chama tuu bali kwa jamii nzima, upinzani hautakwepa kuupitia wakati huu mgumu! Matokeo yake kila uchaguzi watakuwa watu walewale tuu hata ambapo uwezo wao wa ushawishi katika jamii umepungua. (Uwezo huu haupo katika utendaji tuu, bali unaweza kupunguzwa kwa vigezo vingine ikiwemo umri)

USHAURI WANGU:

Kutoka na CHADEMA kuwa na nguvu kubwa kwenye jamii (Katika umoja huu)kikubali kubaki kuwa CHAMA chenye wabunge wengi. Na target iwe kuwa na majimbo mengi kuliko CCM. Hiyo itawezekana tuu kwa kupata support ya vyama vinavyounda UKAWA.

Nafasi ya Mgombe uraisi inapaswa kubaki kwa CUF. Changamoto ni kuwa hayupo mgombea ndani ya CUF mwenye ushawishi wa kutosha kumwondoa Magufuli kwa sasa. Professor Lipumba ni mzuri (Tena sana) lakini nachelea kusema kuwa bado hatoshi! Hivyo basi njia pekee ya kuokoa jahazi ni kumchukua Mheshimiwa Edward Lowassa (If at all patakuwa na huo uwezekano) ajiunge CUF na asimame kama mgombea wa uraisi kwa niaba ya UKAWA.

Kumbuka EL anazijua siri nyingi za watakaokuwa wapinzani wake. Mbali ya doa alilonalo (Ambalo linaweza kufifishwa na dhamira yake ya "kuwajibika" na ushawishi mkubwa alionao kwenye jamii) - Tukubali EL anakubalika! Ni mtu sahihi kuiwezesha CUF kushika dola kwa niaba ya wana-UKAWA. Hakuna uwezekano wa CCM kushinda kama utachukua kura za wanaukawa wote plus za CCM wanaom-support EL! Lazima Ukawa watashinda!

Kwa kufanya hivyo Mheshimiwa Lowassa atatekeleza ilani ya CUF kama chama kilichoshika dola lakini pia CHADEMA kama chama chenye idadi kubwa ya wabunge ndani ya Bunge la JMT. Huo ni mgawanyo sahihi wa uongozi. Wakati hilo linafanyika makubaliano yanapaswa kutambua uwepo wa vyama vya NCCR mageuzi na NLD.

Tanzania mpya inawezekana, lakini ni pale tutakapoweka pembeni maslahi ya vyama na kuweka mbelea maslahi ya watanzania!

ANGALIZO: UKAWA ikivunjika litakuwa pigo kubwa kwa vyama vyote vya upinzani na Demokrasia nchini. Kila chama cha upinzani kitashuka ukilinganisha na nafasi kilichopo sasa. Na CCM itakuwa kwa zaidi ya asilimia 25% ukilinganisha na nafasi yake kwa sasa. NIAMININI!
 
Kwa hiyo unamaanisha cuf washike nafasi ya uraisi Zanzibar na bara so! Huo utakuwa UKAWA au CUF
 
wakati huu tunapokaribia uchaguzi kila jambo linalofanywa na ngome yeyote katika kujiandaa na uchaguzi huu lina mchango mkubwa katika uchaguzi wa oktoba.

ukawa mlikaa chini mkakubaliana kuunganisha nguvu zenu, sasa watanzania wengi wamekuwa wakisubiri kusikia katika muungano wenu mnamsimamisha nani kubeba bendera ya umoja wenu.

swala la uwezekano wa ninyi kisambaratika lilikwisha ongelewa na watu wengi kwani mzee yusufu makamba aliwahi kuwaambia kama utani kuwa muungano wenu ni wa kuunganisha mikia ya paka na panya akikatiza mbele yenu mtakatika mikia kila mmoja akitaka panya awe wake.

wengi wamesema, lakini mimi binafsi juzi nilisema tafuteni mtu anayekubalika nje ya viongozi wa vyama vyenu, anayekubalika na anayeendana na hoja zenu ambazo mmekuwa nazo siku zote abebe bendera yenu.

sijui maneno ambayo watu wanawaambia ingawa sio moja kwa moja huwa mnayazingatia?

kimsingi mtakuwa watoto katika siasa kama umoja wenu utavunjika mapema hivi.

jambo kubwa linaloweza kuvunja umoja wenu ni uroho na ubinafsi. kila mmoja wenu akitaka yeye ndiye afaidi na umoja huu kuliko wengine. ni lazima kila mmoja ategemee kupata na kila mmoja ategemee kutoa.

ujinga wa baadhi ya wenzenu kutaka kutumia umoja huu kama ndio njia ya kupata unaweza kufanya ukawa nzima ikose.

kwenye ubunge ni bora msigawane majimbo bali kila chama kitoe mgombea alafu mtafute njia ya kujua ni mgombea yupi anakubalika katika jimbo ndio asimame mpaka mwisho na wengine wamuunge mkono.

kwenye uraisi mkivutana na kuwa na tamaa ya kila chama kutaka chenyewe ndio kitoe mgombea bila kuangalia kwenye jamii mambo yakoje hamtapata faida za muungano wenu. lakini lazima mjue kusimama mgombea wa chama kimoja ambaye ni kiongozi wa chama anaweza kukiinua chama chake na vingine kushuka na hivyo vyama vingine kuhofu hilo na kujitoa.

kama mmekomaa kisiasa mtajua kutengana wakati huu kunawadhalilisha nyote na hakuna anayeweza kuwaza kumpa uongozi wa nchi mmoja wenu kwa kipindi cha karibuni.

jionyesheni ninyi ni wakomavu wa kisiasa kwa kuibuka na mpango ambao hata kama hamtaingia ikulu lakini nyote mtakua ndani ya ukawa kwa pengine kuongeza kukubalika kwenu kwa wananchi.

lazima mtambue kila mnachokifanya kinachangia katika vyama vyenu kukubalika kwa wananchi hivyo anayewaza leo hii kuibuka na mpango wa kujinusuru yeye binafsi ni mtoto kisiasa asiyejua anachokifanya na maisha yake yote atabaki hapa alipo hawezi kufikia hatua ya kuongoza nchi.
 
Kwa hiyo unamaanisha cuf washike nafasi ya uraisi Zanzibar na bara so! Huo utakuwa UKAWA au CUF

Mkuu kasara; kuna kitu kinaitwa "competitive advantage" huwezi kukwepa CUF kupewa nafasi ya kuwania uraisi zanzibar, kama ambavyo huwezi kukwepa kukipa CHADEMA nafasi ya kuwa na wabunge wengi bara kuliko chama kingine chochote! Ushauri huu umezingatia kuwa na balance katika umoja. Sumu kubwa ya muungano wowote huwa ni ubinafsi.

Kumbuka pia kuwa mchango wa CHADEMA kufanikisha CUF kushinda nafasi ya uraisi Zanzibar ni ndogo kuliko unaoweza kuwa mchango wa CUF kuiwezesha CHADEMA kuwa chama chenye wingi wa wabunge wengi zaidi Ndani ya bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia hatuwezi kuchukulia uamuzi huu kama usio na tija. Endapo wazo hilo litafanyiwa kazi:

1) Itakuwa nafasi ya pekee kubadilisha mfumo wa uongozi wa nchi hii kwa UKAWA kuchukua uongozi wa nchini hii. - ACHANA NA U-CHADEMA na U-CUF!
2) Huwezi ukasema CHADEMA haikunufauka na umoja huo endapo chama kitakuwa na uwingi wa wabunge kuliko chama chochote... (Including a CCM) Kumbuka bunge (likisimama kwenye nafasi yake) ndilo hulisimamia serikali.

Tukumbuke pia kuwa siasa inapaswa kuendeshwa ki sayansi.... - Si muda wa kuingia kwenye uchaguzi ukiwa unategemea miujiza!
 
Last edited by a moderator:
1. Ni ubinafsi kwa CHADEMA kutaka majimbo yote ambayo upinzani una nguvu na wakati huo huo kumtoa mgombea uraisi kwa niaba ya UKAWA.

Katika muungano wowote lazima pawe na kupata na kupoteza. Kuna baadhi ya maeneo muungano utaongeza nguvu zako na kuna baadhi ya maeneo utaku-limit. Hili haliepukiki na ni practice kote duniani. (Hata muungano wetu na Zanzibar ukiuchunguza utaliona hilo dhahiri). Lazima CHADEMA wakubali kupoteza pia.

2. Mgombea Uraisi ndani ya UKAWA

Ni dhahiri kuwa kwa sasa mtihani mzito ndani ya UKAWA ni kumpata Mgombe nafasi ya uraisi....Mgombea ambaye hayupo kushiriki tuu!. Kwa sehemu kubwa ninaamini changamoto hii ni "matokeo ya mapungufu ya kiuongozi ndani ya vyama vya upinzani". Haiingii akilini kuwa ndani ya chama kama CHADEMA, na CUF bado kete pekee ni Dr. Slaa na Mbowe na Prof. Lipumba tuu!.

Tukubali ukweli kuwa viongozi "huibuliwa" na "hukuzwa" na vyama. Kama hatujatoa nafasi kwa vijana na wasomi kuonesha uwezo wao wa kiungozi na uwezo huo ukakua kufikia kujenga ushawishi si ndani ya chama tuu bali kwa jamii nzima, upinzani hautakwepa kuupitia wakati huu mgumu! Matokeo yake kila uchaguzi watakuwa watu walewale tuu hata ambapo uwezo wao wa ushawishi katika jamii umepungua. (Uwezo huu haupo katika utendaji tuu, bali unaweza kupunguzwa kwa vigezo vingine ikiwemo umri)

USHAURI WANGU:

Kutoka na CHADEMA kuwa na nguvu kubwa kwenye jamii (Katika umoja huu)kikubali kubaki kuwa CHAMA chenye wabunge wengi. Na target iwe kuwa na majimbo mengi kuliko CCM. Hiyo itawezekana tuu kwa kupata support ya vyama vinavyounda UKAWA.

Nafasi ya Mgombe uraisi inapaswa kubaki kwa CUF. Changamoto ni kuwa hayupo mgombea ndani ya CUF mwenye ushawishi wa kutosha kumwondoa Magufuli kwa sasa. Professor Lipumba ni mzuri (Tena sana) lakini nachelea kusema kuwa bado hatoshi! Hivyo basi njia pekee ya kuokoa jahazi ni kumchukua Mheshimiwa Edward Lowassa (If at all patakuwa na huo uwezekano) ajiunge CUF na asimame kama mgombea wa uraisi kwa niaba ya UKAWA.

Kumbuka EL anazijua siri nyingi za watakaokuwa wapinzani wake. Mbali ya doa alilonalo (Ambalo linaweza kufifishwa na dhamira yake ya "kuwajibika" na ushawishi mkubwa alionao kwenye jamii) - Tukubali EL anakubalika! Ni mtu sahihi kuiwezesha CUF kushika dola kwa niaba ya wana-UKAWA. Hakuna uwezekano wa CCM kushinda kama utachukua kura za wanaukawa wote plus za CCM wanaom-support EL! Lazima Ukawa watashinda!

Kwa kufanya hivyo Mheshimiwa Lowassa atatekeleza ilani ya CUF kama chama kilichoshika dola lakini pia CHADEMA kama chama chenye idadi kubwa ya wabunge ndani ya Bunge la JMT. Huo ni mgawanyo sahihi wa uongozi. Wakati hilo linafanyika makubaliano yanapaswa kutambua uwepo wa vyama vya NCCR mageuzi na NLD.

Tanzania mpya inawezekana, lakini ni pale tutakapoweka pembeni maslahi ya vyama na kuweka mbelea maslahi ya watanzania!

ANGALIZO: UKAWA ikivunjika litakuwa pigo kubwa kwa vyama vyote vya upinzani na Demokrasia nchini. Kila chama cha upinzani kitashuka ukilinganisha na nafasi kilichopo sasa. Na CCM itakuwa kwa zaidi ya asilimia 25% ukilinganisha na nafasi yake kwa sasa. NIAMININI!

Imekuwa ni jadi sasa kwa Watanzania kuwa na tatizo la kusahau namna siasa za CCM zilivyo hapa nchini. Mwaka 2005 Rais wa sasa Kupitia C CM Kikwete alionekana kuwa chaguo sahihi na baadhi ya watu na viongozi wa kidini walisema alikuwa ni chaguo la Mungu!

Lakini utendaji wake na hasa katika kushughulikia matatizo ya wananchi ya moja kwa moja haukuwaridhisha wananchi wengi na baadhi wanasema kheri aondoke mapema. Leo naona amekuja Dr. Magufuli
ghafla Watanzania naona wamesahau taabu na suluba zilizosababishwa na uongozi wa chama kile kile cha CCM. Sasa watu wameanza tena kuweka matumaini ya ukombozi mpya wa kiuchumi na tofauti za kitabaka utakaoletwa na Dr.Magufuli.

Ni muhimu tukajiuliza ni njia zipi mpya ambazo Dr.Magufuli atatokea ambazo wenzake hawakuzipitia? Wakati wananchi tukiendelea kupigika ndani ya utawala wa CCM, Dr.Magufuli alikuwa ni sehemu ya uongozi uliotufikisha hapa. CCM ina sera ambazo kwa sasa wanahitaji mfumo mpya wa uongozi na lazima wajifunze wakiwa nje ya uongozi ndipo wanaweza kuelewa haya tunayoyazungumza.

Ni vema watanzania tukawa na fikra za kimapinduzi ili kifanya maamuzi magumu dhidi utawala wa kimazoea na kuingiza utawala wa kisasa unaojali mahitaji na mawazo ya wananchi wa hali ya chini kuliko ilivyo sasa!
 
Wewe jamaa ni wa sisiemu na una mpango wa kutuvuruga kisiasa. Si jambo jema na jepesi Lowasa kupeperusha bendela. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tuejizika, mtu ambaye mwanzoni tulikuwa hatumkubali sasa atakuwa mtamu kwa lipi na tutawaambia nini watanzania juu ya huyu mtu? Lowasa alikuwa mtamu ccm sisi huku atatuharibia.
 
Safi sana USHAURI MZURI.je ukawa wako humu ndani? Fanyieni kazi ushauri huu
 
Hahaha umejitahidi ila ngumu sana kwa vichwa vya kina MBOWE na mitaji yao fuata upepo
 
Nilikuwa naanza kukuelewa ila baada ya kutaja huyo fisadi imebidi nisitishe safari ya kuendelea kusoma
 
Mimi ninamuunga mkono mtoa hoja lakini naomba nikupinge sehemu mbili au moja.

Kwakuwa SISI chadema na CUF ndio tunaonekana kuvutana
Na kwakuwa CUF akipewa akitoa Rais bara akatoa na Zanzibar ni kama Kuiwezesha CUF 100% kuwa ndio CHAMA tawala na wengine watakuwa mapambo tu basi mimi ushauri wangu

MGOMBEA atoke NCCR au NLD

Kwanza tujue kabisa bila kupepesa chini ya Watanzania wanaoangalia mambo juu juu bila uchambuzi wa kina, kwa kiasi fulani uteuzi wa Magufuli umebadili kiasi Upepo huku site/mtaani/uraiani

Hivyo tunahtaji mtu anaeweza toa Upinzani mkali kwa CCM nakuizika kabisa, wazo lako la lowasa naunga mkono, lowasa akija huku, ccm imezikwa milele

Lakn tuondoe uwezekano wa huyo lowasa sisi kama UKAWA lazima tukubali Dr slaa ni mzuri na alikubalika na anakubalika ila hawezi kuwa Chaguo sahihi kum kick out magufuli, nasema hivi kwasababu Dr alipata umaarufu enzi zake bungeni hata alipokuja kugombea uraisi ilikuwa bado yupo hot kwasasa nadhani viatu vile kwa kiasi vimepwaya

Dr pia umri umemtupa, nimesikia mara kadhaa watu hasa wakina mama, na hata leo nimeskia wakisema slaa yule hapana, nadhan mnajua. Katika uchaguzi kuna watu wana deal na mwonekano tu wa mtu kijana/mzee haina ubishi, wengine ile presidential material (mnaoelewa mnanielewa).

Sasa kwasababu hizi ndio naona nafasi ya mtu kama MBATIA, naona nafasi ya mtu kama TUNDU lissu

Hawa wawili wanayofauti sana, lakn kwasasa unaweza jua kuwa mtu kama tundu lissu ukiachia mbali mambo mengine ni gumzo kwa kila mtu ana heat site huku, wengi qanamjua kwasababu ya umaridadi bungeni

Mbatia ana busara, ni mtulivu na presidential material, kwasasa anafahamika kwa kiasi lakn anaweza kuuzwa pia katika kampeni

Nafas tunayo, tusiichezee
 
Nilikuwa naanza kukuelewa ila baada ya kutaja huyo fisadi imebidi nisitishe safari ya kuendelea kusoma
Uvumilivu katika kusikiliza hoja hata kama ni kinzani ni muhimu mkuu Khantwe. Hata hivyo hongera kwa kusoma mpaka ulipofikia.
 
Last edited by a moderator:
Wewe jamaa ni wa sisiemu na una mpango wa kutuvuruga kisiasa. Si jambo jema na jepesi Lowasa kupeperusha bendela. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tuejizika, mtu ambaye mwanzoni tulikuwa hatumkubali sasa atakuwa mtamu kwa lipi na tutawaambia nini watanzania juu ya huyu mtu? Lowasa alikuwa mtamu ccm sisi huku atatuharibia.

Mkuu Still88 unakumbuka kipindi ambacho tuliwaita ndugu zetu kuwa CCM B? Mi nilikuwa mmoja wapo lakini unajua hao hao tuliowaita ndio tulioungana nao kuiapata UKAWA? Unakumbuka jinsi gani wengi wetu tulivyomchukulia Mh. Mbatia? Kuwa muwazi tuu ndugu yangu... Majibu yako yanadhihirisha ukweli wa kauli hii... "Theres no permanent allies or enemies in politics, only permanent interests" Swali ni je? do we have common interest? And what is it in the first place? Km wote interest yetu ni kuubadilisha mfumo uliopo na pia tunajua strength za huu mfumo then utakubali tuu kuwa tunahitaji kuachana na fikra mgando, ubinafsi na ushabiki usioangalia uhalisia! Tutashindwa kabla ya pambano, na sitaki hili litokee!
 
Last edited by a moderator:
Mimi ninamuunga mkono mtoa hoja lakini naomba nikupinge sehemu mbili au moja.

Kwakuwa SISI chadema na CUF ndio tunaonekana kuvutana
Na kwakuwa CUF akipewa akitoa Rais bara akatoa na Zanzibar ni kama Kuiwezesha CUF 100% kuwa ndio CHAMA tawala na wengine watakuwa mapambo tu basi mimi ushauri wangu

MGOMBEA atoke NCCR au NLD

Kwanza tujue kabisa bila kupepesa chini ya Watanzania wanaoangalia mambo juu juu bila uchambuzi wa kina, kwa kiasi fulani uteuzi wa Magufuli umebadili kiasi Upepo huku site/mtaani/uraiani

Hivyo tunahtaji mtu anaeweza toa Upinzani mkali kwa CCM nakuizika kabisa, wazo lako la lowasa naunga mkono, lowasa akija huku, ccm imezikwa milele

Lakn tuondoe uwezekano wa huyo lowasa sisi kama UKAWA lazima tukubali Dr slaa ni mzuri na alikubalika na anakubalika ila hawezi kuwa Chaguo sahihi kum kick out magufuli, nasema hivi kwasababu Dr alipata umaarufu enzi zake bungeni hata alipokuja kugombea uraisi ilikuwa bado yupo hot kwasasa nadhani viatu vile kwa kiasi vimepwaya

Dr pia umri umemtupa, nimesikia mara kadhaa watu hasa wakina mama, na hata leo nimeskia wakisema slaa yule hapana, nadhan mnajua. Katika uchaguzi kuna watu wana deal na mwonekano tu wa mtu kijana/mzee haina ubishi, wengine ile presidential material (mnaoelewa mnanielewa).

Sasa kwasababu hizi ndio naona nafasi ya mtu kama MBATIA, naona nafasi ya mtu kama TUNDU lissu

Hawa wawili wanayofauti sana, lakn kwasasa unaweza jua kuwa mtu kama tundu lissu ukiachia mbali mambo mengine ni gumzo kwa kila mtu ana heat site huku, wengi qanamjua kwasababu ya umaridadi bungeni

Mbatia ana busara, ni mtulivu na presidential material, kwasasa anafahamika kwa kiasi lakn anaweza kuuzwa pia katika kampeni

Nafas tunayo, tusiichezee

Heshima kwako mkuu Dumelang. Hongera kwa mawazo yako mazuri. Nakubali kabisa kwa mgombea huyo kutoka NLD au NCCR km ulivyopendekeza. Hilo litaondoa hiyo dominance ya upande mmoja bt again that candidate has to be EL

Faida kubwa ya EL ni kuwa kwanza adui amegawanyika. EL akitoka ni lazima atoke na not less than 12% of the votes that would supposedly fall to CCM candidate. Hiyo ni advantage kubwa sana kwa UKAWA maana hapo ni kabla ya kuweka kura za UKAWA.
 
Last edited by a moderator:
UKAWA yetu tugawane mbao!
attachment.php
 
Attachments

  • IMG-20150714-WA0000.jpg
    IMG-20150714-WA0000.jpg
    57 KB · Views: 257
duuu,2angalie sana ushauri unaotolewa humu..kwanza mgombea anatakiwa awe anajulikana, pili aliekuwa wa 2 ndo ananafasi ktk uchaguzi.. so anaesema dr hafai ni mwongo na ni kampeni za ccm ili cdm ishindwe. 2mesahau utafiti wa juzijuzi 2, wakwanza alikuwa ni lowasa 2 alkuwa ni dr slaa na watatu sijui.magufuli hana ubavu wa kumshinda slaa asilani
 
Back
Top Bottom