Peter Agostino
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 105
- 227
Katika blogu ya jifunzeujasiriamali, mara nyingi nimekuwa nikiulizwa swali hili na wasomaji wengi wa mtandao huo wakitaka kujua ni mtaji au mahitaji kiasi gani yanayotosha kuanzisha biashara maalumu mtu anayolenga kuianzisha(their specific business). Na mimi nimeshatoa majibu mara kadhaa kama ilivyokuwa kwa makala hii ya “Mtaji wa kuanzisha biashara ya jumla ya vocha za simu, million 2 inatosha?”
Hata hivyo kuna wasomaji hata baada ya kusoma majibu hayo bado huonyesha kuwa na wasiwasi kwamba labda njia niliyoeleza haitoshi na pengine kuna njia rahisi zaidi au majibu yatakayoweza kutatua shida yao kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Msomaji anapouliza swali kama hili anategemea kukutana na jibu kamili kwamba labda kuanzisha biashara ya kuuza nguo za mitumba unatakiwa uwe na shilingi milioni 2 au milioni tatu au kiasi chochote kile kingine, lakini hilo haliwezekani na siyo kila mtu anayeanzisha biashara fulani basi ataanza na kiasi cha fedha kile kile atakachoanza nacho mtu mwingine. Kuna vigezo vingi vinavyotakiwa kuzingatiwa kikiwemo ukubwa wa biashara, kiasi cha mtaji ulichokuwa nacho, upatikanaji wa mtaji nk.
Kwa hiyo mshauri wa biashara, mtaalamu au kocha wa biashara hawezi kukutajia kiasi kamili cha mahitaji ya biashara yako tuseme katika simu au ndani ya kipindi kifupi tu cha mazungumzo labda tu iwe mlikuwa mmeshazungumza kabla mkafanya matayarisho, ukampa picha halisi ya biashara hiyo kulingana na utafiti uliokwishafanyika.
Kitu pekee ambacho mjasiriamali au mtaalamu anayefanya tathmini ya biashara popote pale kujua mahitaji ya mtaji ni kiasi gani anachopaswa kufanya, ni zoezi la utafiti au upembuzi yakinifu ambao pamoja na mpango wa biashara vinakuwa ndiyo muarobaini wa kubaini biashara fulani inahitaji kiasi gani cha pesa pamoja na masuala mengine yote yanayoihusu biashara hiyo.
Kama kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kinavyoelezea vitu hivi kwa undani, kimsingi siyo zoezi gumu wala linalohitaji utaalamu wa hali ya juu kufanya, ni jukumu ambalo mjasiriamali mwenyewe kama anaweza kupata maelekezo kidogo basi anakuwa na uwezo wa kufanya peke yake bila hata usaidizi kutoka mahali pengine popote.
…………………………………………………………………….............................................
Blogu ya jifunzeujasiriamali, imeandaa SEMINA ya jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara awamu ya tatu ambapo jumapili hii mpaka jumanne tutakuwa tukichanganua biashara ya saluni ya kike iitwayo, ROSE HAIR & BEAUTY SALOON
· Kiingilio ni Tsh. Elfu 10
· Mshiriki atapewa kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali PDF bure.
· Inaendeshwa katika blogu maalumu ya MICHANGANUO na kwA njia ya email.
· Masomo yapo katika post za kawaida za blogu hiyo, mp3 pamoja na PDF.
· Msiriki atapata pia fursa ya kujifunza masomo ya semina za awamu zote 2 zilizopita pamoja na tiketi ya kuingia semina nyingine zote zitakazofuata baada ya hii, zinazohusiana na michanganuo ya biashara.
· Fursa ya kuuliza swali lolote muda wowote kwa mkufunzi wa semina ambaye muda wote yupo online.
Kujiunga na semina, lipa kiingilio chako sh. 10,000/= kupitia namba za simu 0712202244 au 0765553030, jina ni Peter Augustino Tarimo, Tuma pia anuani yako ya emai kwa njia ya meseji (lakini iwe ni ya GMAIL, aina nyingine mfano yahoo nk. haziwezi kusapoti blogu ya masomo).
Baada ya hapo, utatumiwa email yenye baadhi ya masomo pamoja na link ya BLOGU HII YA MASOMO YA SEMINA YA MICHANGANUO.