kuongezea kwa majibu ya wadau hapo juu, kama internet yako sio nzuri na speed inapanda na kushuka, kudownload kutakula mb chache na kuangalia online kutakula mb nyingi,
na assume unaangalia video ya dakika 5.
youtube wao wanakuchagulia quality kutokana na speed yako, umeanza kuangalia speed yako ni ndogo umeangalia sekunde 30 na video ime buffer mpaka dakika 2 (hapa ni sawa na umedownload 40% ya video yako), ghafla mtandao wako speed ikaongezeka, youtube watafuta ile uliodownload na kisha wata buffer kwa quality kubwa zaidi, hivyo huu mchezo wa kuchange quality huku unaangalia video na kudelete kile ulicho buff basi utasababisha mb ziende nyingi zaidi kuliko kudownload.
solution yake hii kama unatumia browser utafute extension inayofanya quality iwe fixed.