dah, enzi hizoooo, kudadadeki, manzi alinijibu, sikupendi, kwanza huna hadhi ya kuwa na mimi, yaani wewe humvutii mwanmke yoyote, hivi unajua kama wewe ni kituko? muone kwanza sura yake....dah hahaaah nakumbuka nilijihisi tofauti sana na wakati ananijibu hivyo tupo waqwili tuu akinisindikiza katika match kijiji cha pili..nilimuangaliaa kisha nikasema hivi huyu hanijui, hajui hapa tupo wapi nitamfanyizia hapahapa, aah nikapotezea, ilinivuruga sana maana ktk machi huko nilikuwa nikikosa Magoli hovyo na mimi ndio nilikuwa tegemezi kwenye team ya kijiji, kutokana na kasi niliyokuwa nayo...basi hiyo siku ilikuwa mbaya mbaya sana kwangu.alivyokuwa mdwanzi akaja tena home akamsalimia bi mkubwa akauliza nilipo akaja,akaniambia usikasirike bwana mi namaanisha tuu kweli sikupendi ila mtu akikwambia akupendi usimchukie maana huwezi jua..pia nimekuja kukuaga mi narudi shule kampala..nikamjibu fresh tukapiga sana stori usiku huo na kesho yake nikamsindikiza akasepa, mwaka uliofuata nikiwa nishamsahau habari zake hata kichwani hayupo tena, tena katika uwanja uleule, game imeisha namuona mtu huyu apa, vipi wewe umekuja lini? anasema nimekuja saa tisa nikaenda kwenu nikaambiwa uko mpirani nimekuja kukuangalia, nikamwambia nashukuru, vipi masomo akajibu kamaliza ila amekuja mara moja tu hatakaa sana...ki ukweli naweza sema huyu manzi nilimuelewa sana si mimi tuu hati ma blaza na ma faza wa kijiji walikuwa manamtolea macho na wanatamani wamdukue...wakati huo mimi nishakubali kushindwa sina mpango..akaniambia nakupenda sana tukiwa njiani tunarudi home, nilichomjibu mimi ni kwamba apunguze bange labda atakuwa anatumia kali sana, nikamwambia pia mimi niko katika mahusiano na house girl wao maana huyo ndio hadhi yangu tunaendana na kama haamini mimi nakula beki tatu wao akifika kwao akamuulize mama yake mimba ya yule beki tatu ni ya nani.....hahaaaaah nililipiza nikaanza kuonza kuona michozi inatoka, nikamuuliza vipi? tembea twende usije ukabakwa huku maporini twende nyumbani, njia nzima ananiuliza hivi ni kweli? hivi ni kweli? nikamjibu ndio ni kweli yule ndio saiz yangu...hahahaaa eti nikifika tu namfukuza mimi ndio nilimleta pale akuchunge na awe ananiambia taarifa zako leo hii anafanya hivi walah namfukuza na akinibu namchoma hata kisu, mara huyo katimua mbio anakimbilia kwao, nikaona huyu mwehu leo nimemuweza....nikamwacha aende...kufika huko kwao moja kwa moja kamvaa beki tatu, vitasa vya maana, bi mkubwa wake anashangaa huyu binti kapatwa na nini maana ni mpole hata kuua mbu ni shida leo vipi, kajaza watu..bahati nzur hakusema sababu ya kumtembezea kichapo shilawadu wake..ni nimefika home nikaoga wakati natoka nikamuona kaka nje kwao kajiinamia nikampita nikaondoka zangu....usiku kaja dirishani, oya we mdwanzi fungua, nikatoka nikamfungulia kapitiliza mpaka ndani, nikamuuliza vipi akasema fresh nimekuja kukujibu lile ombi lako..ikawa hivyo yaani kila siku ipatikanapo nafasi ni kunjunjana, iwe iwe asubuh, haya iwe mcha ama usiku, mwisho mimba ndi..wote wanafunzi.....ni story ndefu ila iliisha vibaya, kumbukumbu mbaya kwangu ni kwamba wazazi wake walikuwa wajeda kuna siku nilipewa kichapo na MP nikahisi roho ndio inatoka siku hiyo, alipojulikana ana mimba na akagoma kuitoa, tukafukuzwa makwetu, tukaenda kupanga magomeni hapo tena mambo ya masomo ilibidi yasimame na tukaanza kutafuta kazi wote wawili, na bahati kila mtu alipata kazi, mimba ikawa kubwa na hatimae siku za kujifungua zikakaribia, nikatafutwa kimya kimya nikapewa tena kichapo cha maana kama onyo niachane na yule binti, binti ndio alikuwa mtetezi wangu siku zote ila kwa kichapo hiki cha pili ilinibidi sasa niangilie upya hayo mahusiano maana hali ilizidi kuwa mbaya...yule binti alifuatwa na binamu yake pale nyumbani akachukuliwa akarudishwa kwao na yule binamu akaniambia mdogo wangu chukua pesa hii nenda mkoa wowote kaendelee na masomo, nyumbani washajua unapokaa, na mzee ana hasira na wewe...sepa dogo nakwambia kama kaka yako...huo ndio ulikuwa mwanzo wa kutengana na lile jembe..nikaenda mikoa ya kusini huko, nikasoma huko, mpaka nikapoteza na masiliano nae, niliporudi town nikamkuta mtoto tayari ana miaka mi2 na nusu wa kike ila binti ana pete ya uchumba, niliumia sana, hiyo siku nikala sana vitu akanihadithia mambo yalivyokuwa baada ya mimi kuondoka...mpaka kuozeshwa kwa huyo mzungu ambae ndio mumewe mtarajiwa, nikaona kher tuu maana kwa wakati huo mimi ndio nimemaliza shule namiliki suruali tuu..nikaanza mishe mjini kuichukufukua family.we mzee aliposikia ibilisi nimerudi akampeleka canada mama na mtoto, mpaka leo hii, mtoto sasa ana miaka 19 kwa maana si mtoto tena, ni mtu mzima nae ana maisha yake na mtoto mmoja.........hili ndilo lilikuwa bao la mechi ya ufunguzi wa mlolongo mreeeeeeeefu sana huko mbele ktk mahusiano..na mwisho wa siku ni kwamba mimi ni babu kijana pengine kuliko wote humu JF..niliamua kuoa mapema pia sababu sikutaka kurudia kosa