Sir Yahaya
Member
- Nov 6, 2019
- 19
- 49
Njia tano za asili za kuondokana na miguu kuwaka moto
Huu ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi sana na mara nyingi humfamnya mtu mwenye tatizo hilo kushindwa kusinzia japo anahisi kusinzia.
Miguu kuwaka moto ni ugonjwa unaotokea ambapo katika mwili wa binadamu kutakuwa na matatizo kama kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili yani za miguuni hivyo kupoteza uwezo wa utendaji kazi wa neva miguuni, sababu zingine ni kama kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu, kuwa na sumu nyingi mwilini,kurithi au mwili kushindwa kufanya kazi zake vizuri.
Dalili za ugonjwa wa miguu kuwaka moto
Ugonjwa huu una dalili nyingi zikiwemo:
- Kuhisi ganzi,
- kuhisi kuchomwa na kitu chenye ncha Kali miguuni,
- kuhisi miguu kuwa na majimaji kwa ndani,
- joto Kali miguuni,
- kuhisi kama unaungua miguuni,kushindwa kushika au kubeba vitu na maumivu makali.
Vitu/ mambo yanayoweza kupelekea mtu miguu yake kuwaka moto
Kuna mambo mengi sana yakiwemo:
- Uzito mkubwa wa mwili (hii husababisha uti wa mgongo kukaa tofauti na unavyostahili hivyo baadhi ya neva kukandamizwa na uzito wa mwili au misuli hivyo kusababisha miguu kupata maumivu na kufa ganzi.
- Matumizi ya baadhi za dawa zenye kemikali kwa muda mrefu au mara kwa mara mfano dawa za TB, HIV nk.
- Upungufu wa virutubusho mwilini hasa mkusanyiko wa Vitamini B
- Magonjwa ya sukari na Shinikizo la damu , magoti , mzio na fangasi
- Matatizo ya moyo
- Matatizo katika mishipa ya damu
- Ulevi wa kupindukia kwa muda mrefu
Jinsi ya kuepuka ugonjwa wa miguu kuwaka moto
- Kuwa na uzito unaoenda na na kimoja chako
- Fanya mazoezi ya mwili
- Kula chakula kinachokupatia virutubisho mwili hasa VITAMINI B
- Usafi wa viatu, sox na miguu
- Ondoa sumu au kemikali mara kwa mara mwilini
Matibabu:
- Kula vyakula vyenye mkusanyiko wa vitamini B za kutosha
- Fanya mazoezi ya mwili kama kukimbia, Kutembea n.k pia kufanya massaging
- Punguza uzito uliopitiliza
- Tumbukiza miguu katika maji ya vuguvugu yenye chumvi
- Tibu maradhi ya sukari hakikisha sukari ipo sawa
- Ondoa sumu kali mwilini mara kwa mara
- Chua miguu yaki kwa vitu vinavyopunguza maumivu ,vinavyosaidia mzunguko wa damu kuwa Vizuri (paka Asali mbichi, shubiri na limao).