Njia 13 za kujiweka mwanamke ili mwanaume watamani kukufukuzia

DJ SEPETU

JF-Expert Member
Apr 17, 2017
8,413
12,328
Nimepokea maombi mengi sana kutoka kwa baadhi ya kinadada kwenye pm yangu wakitaka kujua vile wanavyoweza kuvutia zaidi mwanaume Na hatimaye kuweza kupata chaguo bora la mume.
Aidha kuongezeka kwa nyuzi nyingi za wakina dada kutafuta waume pia kumechagiza Mimi kuwaandalia hii mada ambayo kiuhakika itafungua milango ya kuongeza kismati Na kuanza kupoteza muda Na fedha kwa waganga matapeli.

Usijilaumu labda una mkosi ama huna umbo au sura ya kuvutia hapana fuata ushauri wangu Na utaona tofauti kubwa sana.
Twende kazi

1.Namna unavyovaa!
Ukivaa mavazi ya kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wako utaishia kuwapa wale hit and run tu.
Vaa kistaha ila sio kishamba mfano unavaa dela au khanga out.

2.unavyomwangalia mwanaume
Kuna aina mbili za kumuangalia mwanaume!
A.polepole itaonyesha kuwa umevutiwa nae.
B.haraka haraka.hii humpa confidence mwanaume ya kuendelea,ulisha muona jogoo akidonoa mchele ndo hivyo.

3.Mfanyie kazi iwe rahisi
Ni ngumu mwanaume kukuapproach ikiwa kwenye kundi la marafiki zako,unaweza kwenda mahali ambapo atakuwa huru kurusha ndoano.

4.Sehemu mubashara
Kukaa sehemu ambayo mwanaume akikusogerea kila jirani atageuza shingo kujua kinachoelea utachelewa sana,sehemu mujarabu ni kama vile mkahawa,supermarket, au maktaba.

5.mpatie nafasi aongee Na wewe.
Kutopokea hata salamu Na kuwa ktk mood hasi itamkatisha tamaa mwanaume.

6.Tabasamu!
Amini usiamini tabasamu huwezi kuvunja moyo hata Wa mnyongaji.
Jaribu Na utaona utitiri Wa mwanaume.

7.Usiboreke
Kuwa mwanamke kwenye furaha,ndio watu wana shida lakini huna sababu ya kuonyesha kwa mtu asiehusika.

8.Acha ujeuri
Unamkasirikia rafiki yako Na kadharika,unapunguza mvuto kwa mwanaume, hakuna mwanaume atakayemtongoza mtu atakaye mpuuza au mkataa.

9.Usitangamane Na wanaume
Muda wrote ukiwa kwenye group la wanaume unajipotezea bahati.

10.muonyeshe uko interested
Mjulie hali Na kadha Wa kadha.

11.onyesha uanamke wako
Fanya manjonjo mbele yake mfano rudisha nywele nyuma .

12.Mchokore
Pita mbele yake mwangalie machoni wakati unapita mtese kihisia!

13.usilazimishe
Mwanaume atagundua mapema kuwa upo approachable,ukienda sawa kama ni kawaida yako kwa hiyo usilazimishe.
Asante.
 
Ninaamini kila shetani na mbuyu wake, unaweza kuwa changu doa wa corner bar na mkaka akafahamu yote, kama anakupenda atakwambia tu kama uko tayari kuachana na shughuli hii nitakuoa, ukikubali mnapima ngoma na ndoa inafuata. Mapenzi hayana formula mkuu.
 
Sijaelewa unamaanisha nini kwenye kusema sijui MTU akae sehemu ambayo ni rahisi kutongozwa.
Nilichogundua unafundisha mbinu za wanadada kujiuza.
Hatufuati ng'ooo na watakuja wenyew kama imepangwa.
 
Sijaelewa unamaanisha nini kwenye kusema sijui MTU akae sehemu ambayo ni rahisi kutongozwa.
Nilichogundua unafundisha mbinu za wanadada kujiuza.
Hatufuati ng'ooo na watakuja wenyew kama imepangwa.
Soma vizuri ninazungumzia ni namna mtu anaweza tengeneza social environment ya kukutana Na watu anuai,wala sio huo umalaya unaousema hapa.
 
Ninaamini kila shetani na mbuyu wake, unaweza kuwa changu doa wa corner bar na mkaka akafahamu yote, kama anakupenda atakwambia tu kama uko tayari kuachana na shughuli hii nitakuoa, ukikubali mnapima ngoma na ndoa inafuata. Mapenzi hayana formula mkuu.
Hizi ni scene chache sana elfu kwa mmoja,ndio dada poa anaweza kuolewa lakini muoaji atakuwa amelidhika tayari,sijazungumzia ulichoropoka hapa.
 
Hizo ni njia za kujirahisisha tuuu, mwanamke anayejiamini haangaiki na hayo yote sababu kutongozwa huja automatically.
Pindi ukifika 40 Na bado upo single mom, au nungayembe utaelewa nilichosema hapa!!!
 
Huku kufundishana ufuska sasa.
Dada yangu Mimi pia nilijua kuwa kuna watu watatafisiri kama wewe,kiukweli kabisa sivyo Uzi huu unajadili namna mwanamke anavyoweza kuwa approachable,yaani kujenga tabia zitakazo kupa exposure ya kukutana
Na watu Na vile watu watakapokuona kuwa ni mtu social.
 
Pindi ukifika 40 Na bado upo single mom, au nungayembe utaelewa nilichosema hapa!!!
Hahahahaha! Nimeolewa na siwezi msema vibaya ambaye hajaolewa, wala mwanamke ambaye analea watoto peke yake huyo ninamheshimu vibaya mnoooo sababu ni jasiri na ana utu, wangapi wanatoa mimba lakini yeye ameamua kulea mimba hadi mtoto unafikiri ni kazi ndogo?
Nawapenda na ninawaheshimu sana hawa watu.
 
Sasa mbona unaleta mdomo pindi watu wenye nia njema kama Mimi tunapotaka huyu single mother apate msaidizi au ambayo hawajaolewa kama wewe wapate wenzi,be honest
 
Dada yangu Mimi pia nilijua kuwa kuna watu watatafisiri kama wewe,kiukweli kabisa sivyo Uzi huu unajadili namna mwanamke anavyoweza kuwa approachable,yaani kujenga tabia zitakazo kupa exposure ya kukutana
Na watu Na vile watu watakapokuona kuwa ni mtu social.
Utasamehe mkuu.
Yawezekana hukuwa na nia mbaya ila sisi tu tumekujudge vibaya.
Si unajua sisi wanadamu kila unachokifanya kuna watakaosifia na kuna watakaoponda hata kama nia yako sio hiyo wanayoifikiria.
 
Back
Top Bottom