Njegere Ni chakula cha kawaida kabisa kwa watanzania wengi.Njegere huweza tumika kama sehem ya kifungua kinywa,kiungo cha supu ,kiungo cha saladi na hata kama sehem ya mlo mkuu .
Kuna Namna nyingi sana ya kupika na kuandaa njegere.Hii ni moja ya namna ya kuandaa njegere kama sehem ya mlo mkuu. Kwenye pishi hili nimetumia Beef masala kama moja ya kiungo.Ingawa kiungo hiki ni maalum kwa nyama,kinaleta ladha nzuri sana kwenye Njegere.Kumbuka tu,Upishi ni sanaa,ubunifu lazima.Usikariri. Mahitaji Njegere ½ kilo Nyanya 3 kubwa Swaumu ½ kijiko cha chai Beef Masala kijiko 1 cha chai Nyanya ya Kopo vijiko 2 vya chai Maziwa fresh kikombe 1 ½ Karoti Mbili,kata duara Mafuta vijiko 4 vya chakula Chumvi kwa ladha upendayo Njia 1.Chemsha njegere adi ziive,ziwe laini na Maji yakauke. 2.Katika sufuria unga mafuta na kitunguu adi kitunguu kianze kubadilika rangi(usiache kikawa cha brown) ,Ongeza nyanya,nyanya ya kopo,chumvi,swaumu na beef masala.Kaanga adi nyanya na mafuta zitengene ndani ya sufuria. 3.Ongeza njegere na karoti ,kaanga kwa pamoja adi njegere na nyanya zishikane.Ongeza maziwa,chemsha uku unageuza mara kwa mara ili maziwa yasikatike na yasiungulie chini.Chemsha adi upate uzito unaopenda.Tayari kwa kula.
Kama familia inawatoto wadogo basi ongeza kiasi cha maziwa ili upate mchuzi mwingi.watoto wengi hupenda mchuzi wa njegere na si njegere zenyewe.