Njaa ni ugonjwa mbaya zaidi kutokea si tu Afrika, ila Tanzania, nimeamini leo

zunya

JF-Expert Member
Sep 2, 2014
1,528
1,064
Njaa ni ugonjwa mbaya zaidi kutokea si tu Afrika, ila Tanzania, nmeamini leo.

Nilifanya jaribio dogo tu nione hali ya mambo inaendaje kwenye njaa, niliamua toka jana nisile, nimeamuka nikanywa chai na chapati mbili mida ya saa tatu ivi asubuhi, nikakaa hadi mida ya saa tano nikaenda sehemu kukaa na washikaji tupige stori mbili tatu.

Ikafika mida ya saa nane kila mtu anaagiza chakula uko mi hata sihangaiki, nimekaa tu napiga story watu wanakula wanamaliza mi sitaki chochote kile, zaidi nilinunua pipi kali ili mdomo usichachuke sana.

Nikarudi nyumbani mida ya saa moja, nikaoga, nikapata kikombe kimoja cha maziwa (artificial) na kuingia kulala, nikaamuka asubuhi huyo kazini bila kupata kitu chochote kile ile asubuhi zaidi ya maji glasi moja tu.

Kufika kazini nimekaa hadi saa nne, njaa inauma vibaya hadi nasikia kizunguzungu, mdomo umechacha sitamani hata kuongea, na nilitoka sina hata hela ya kula uzalendo ukanishinda nikaamua kumpigia swahiba wangu mmoja anitumie walau 20 nile maana hali ilikua mbaya

Njaa mbaya jamani!
 
Sasa bora wewe umeona njaa mbaya halafu unauhakika wa hicho chakula.. hali kama hiyo inakupata na hauna matumaini ya kula mkuu wanasema adui yako muombee njaa
 
Njaa inauma pale unapokuwa hata hujui chakula utakipata lini, yaani una njaa na hauna uhakika wa kula!
Sasa wewe unajishindisha njaa makusudi! halafu unauhakika wa chakula, na unaleta report ya jaribio!
 
Hiyo sio njaa ni hofu njaa inamuuma asiye na uhakika wa kula
 
Kaka ktk maisha ya mwanadamu, tumbo ndo kila kitu, mtu kumiliki kila kitu ni ishara ya kutunza tumbo tuuu.
 
Asikudanganye mtu njaa ni zaidi ya vita. Ila hiyo yakujitakia sio njaa mkuu.
Mi nipo mahali naona watu wanavyogombana ili kila mmoja awe boss, nihatari.
 
Mi nikiwa fiti mfukoni huwa sisikii njaa. Ila tangu mwaka jana nakula kila wakati sababu ya stress. Biashara zikifa nitaitwa mpiga dili
 
Njaa inampata ASIE NA CHAKULA WALA UHAKIKA WA CHAKULA,na omba Mungu usikutane na hiyo hali,waweza kuiba mbele za watu na ukadhani uonekani,kumbe njaa imekukamata.
 
balaa hilo linakutokea na huna uhakika wa kupata chakula kwa jasho lako na tegemezi lako la mwsho ambaye ni mzee FARU J anakwambia "mwafwaa"inauma sana
 
Back
Top Bottom