Kuna historia inazungumzwa kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu wa miaka ya 1990 kurudi nyuma walikuwa kama "watchdog" wa serikali. Serikali ilikuwa ikianzisha/kutenda jambo ndivyo sivyo basi wanafunzi hao walikuwa wakianzisha mgomo mzito uliyokuwa ukiitikisa serikali. Akina Samweli Sitta na James Mabatia ni miongoni mwa watu waliopata kashda (kashi kashi) na migomo hiyo.
Mgomo wa mwisho mzito kabisa kufanyika vyuo vikuu ni ule wa Mwaka 1990.
Jeneza la migomo ya vyuo vikuu kwa masuala muhimu katika nchi lilifungwa pale mikopo ya Elimu ya juu ilipoanzishwa. Tangu kuanzishwa kwa mikopo hii kinachotokea vyuo vikuu siyo migomo kwa masuala bali makelele ya kudai posho zao za kujikimu.
Ndiyo maana kwa mfano tatizo kama lile la UDOM limetokea, watoto wenzao hata kama hawasomi degree kama wao, wanafukuzwa na serikali lkn wako kimya wanaendelea na masomo. Hii ni njaa ya tumboni inayopelekea fikra za wanafunzi hawa kuwa pofu na mfu kabisa. Hawagomei masuala (issues) wanagomea njaa. Hii ni hatari.
Tunaambiwa vyuo vikuu ni chemichemi ya fikra huru, lkn sioni tena Uhuru wa fikra miaka hii. Ninaona kundi la vijana wapaka poda na sketi za kubana bila kusahau suruali za mlegezo wakishauriana namna ya kutumia "boom" lao.
Sababu ya pili ni " kuwapa shavu" (kuwapa vyeo) ktk serikali wahadhiri wa vyuo vikuu. Hii nayo imekuwa kansa kwa wasomi hawa. Badala ya kuishi kwa misingi ya taaluma zao wamekuwa wakiishi kwa kujikomba kwa wanasiasa ili wapate shavu.
Wasomi wa zamani walikuwa wakiendesha harakati ktk vyuo vikuu na walikuwa wakitoa nadharia madarasani na kuziweka kwa vitendo kwa kuwahamasisha wanafunzi kupinga jambo/suala fulani. Lkn siku hizi, wapi bwana! Njaa ya vyeo imeua nadharia lukuki zilizojaa vichwani mwa wasomi hawa. Sasa wanaishi kama bibi yangu wa Nakapanya ambaye hakuwahi kufunua kitabu hata kuangalia picha tu.
Masuala muhimu yanakanyagwa na serikali nchi hii lkn wasomi wa vyuo vikuu wapo tu. Kwao muhimu ni njaa zao, siyo njaa ya jamii?
Oops!! Wonders shall never end. Idiots are becoming wiser than elites.