Nizar khalfan atemwa vancouver, apata timu mpya.

PingPong

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
926
160
KIUNGO wa Tanzania Nizar Khalfan ametemwa kwenye timu ya Vancouver Whitecaps ya Canada kutokana na kushindwa kuonesha uwezo wa kuridhisha kwa timu hiyo inayocheza ligi ya MLS nchini Marekani.

Uamuzi huo wa Whitecaps kumtema Khalfan ulitangazwa Jumatano, ambapo baada ya kutemwa huko klabu ya Philadelphia Union pia ya nchini humo ilitangaza kumchukua.

Kocha Rennie alisema pamoja na kufikia uamuzi wa kumtema Khalfan, jambo hilo lilikuwa gumu kwao kutokana na kiungo huyo kubadilika na kuimarika kimchezo katika miezi ya mwisho, lakini kulikuwa hakuna budi kufanya hivyo kwa sababu klabu inahitaji mabadiliko.

"Nadhani ni mchezaji mzuri mwenye uwezo na nimefurahi kwamba amepata nafasi ya kuwemo kwenye ligi kwa sababu tulikuwa na mawazo mengine kuhusiana na nafasi yake ," Rennie alisema.

"Kwa jumla wakati huu tunatazama zaidi kuhusiana na kinachozalishwa na tunapenda kasi na mabadiliko kwenye mchezo, lakini pia tunahitaji watu wa kutengeneza nafasi na kupata magoli mengi zaidi na hayo yote yalikuwa masuala magumu hasa katika safu ya kiungo," alisema.

Khalfan, aliifungia bao moja tu timu hiyo na kusaidia kutengeneza mabao mara nne alipoanza mwaka huu vema akitokea kwenye benchi katika mchezo wa tatu wa timu yake ya Whitecaps.

Alitengeneza mabao mawili na kufanya mechi hiyo dhidi ya Kansas City kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 baada ya wao kuwa nyuma, lakini hakuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza na mara nyingi alikuwa akianzia benchi.

Khalfan alifunga bao lake la kwanza baada ya kuanzishwa kwenye kikosi cha kwanza na kocha wa awali Tommy Soehn na ndipo alipofunga bao hilo la pekee kwake katika ligi ya MLS dhidi ya Real Salt Lake. Whitecaps ambayo hivi sasa inanolewa na kocha mpya Martin Rennie.

Hivi karibuni Khalfan alijiondoa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Bara inayoshiriki michuano ya Chalenji kwa maelezo anaenda kushughulikia usajili wake, ambapo sasa amepata timu mpya ya Philadelphia Union.



source: Habarileo
 
Kambi popote tu! Piga soka ndugu!

yeah ni kweli mafanikio anaweza kuyapata popote pale, ila inambidi Nizar akaze msuli zaidi ili mambo yaende fresh maana naona huko kuna competition kubwa sana ya namba, wenzetu wanaotoka kwenye mataifa yaliyo juu kisoka wana nafasi kubwa kuliko sisi.
 
[h=1]Union claim midfielder Khalfan in MLS Waiver Draft[/h] MF joins Philadelphia from Vancouver; Holder, González waived
November 23, 2011

Philadelphia Union Communications





[h=2]Khalfan[/h]
khalfan.jpg










Chester, Pa. (November 23, 2011) – Philadelphia Union announced the club has selected Nizar Khalfan in the MLS Waiver Draft after Vancouver Whitecaps FC released him earlier today. Additionally, the Union have waived goalkeeper Thorne Holder and defender Juan Diego González.
A native of Mtwara, Tanzania, Khalfan appeared in 22 regular season matches in 2011, including nine starts. In 1,066 minutes, the 23-year-old notched a goal and four assists. The midfielder joined Vancouver midway through the 2009 USL First Division season, playing a total 58 games and 3,029 minutes with the Canadian side.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom