Niwe Upande Gani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niwe Upande Gani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saharavoice, Jun 19, 2009.

 1. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Baada ya sakata la misamaha ya kodi kwa mashirika ya dini kumalizika kwa serikali kusalimu amri, nimebaki na maswali mengi bila majibu. ukifikiri kwa undani sana utagundua kwamba ni kweli misamaha hii iko abused kwa kiwango cha hali ya juu sana na hapo ndipo tunaona jinsi tunavyopoteza mamilioni ya kodi.

  Wajanja wengi walianzisha na wanaendelea kuanzisha mashirika ya dini kwa ajili ya kufaidi misamaha kama hii na kwa kweli si kwa ajili ya kuwasaidia wananchi bali ni kwa sababu ya kufanya biashara.

  Lakini nimejiuliza maswali mengine pia kwamba: Iwapo mashirika haya yanapata misamaha ya kodi mbona karo za shule za seminari ziko juu sana ukilinganisha na private schools zingine zisizopata misamaha ya aina hii? Mbona baadhi ya hospitali za mashirika ya dini zinatoza viwango vikubwa vya matibabu kuliko private hospitals zingine????. Hivi waliosoma Seminari zamani walilipa karo za kiwango kikubwa kama cha sasa?

  Wakati naendelea kufikiri hivi, najiuliza tena je huko makanisani na misikitini kuna Ufisadi unaendelea? Au Dini zetu zimegeuka za kibiashara badala ya huduma?? wakati naendelea kujiuliza, mimi huyo kiguu na njia nakutana na mheshimiwa Mbunge rafiki yangu, namuuliza maswali yangu kuhusu hili, anakubaliana na mawazo yangu lakini ananiambia mzee ukitaka usipate ubunge tena basi unga mkono serikali katika hili. "mimi hili sichangii" anasisitiza.

  Mwishowe nabaki nimeduwaa, political impact!!!!!!!
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,791
  Likes Received: 83,168
  Trophy Points: 280
  Mimi naamini kabisa huko makanisani na misikitini kumejaa unafiki na ufisadi wa hali juu. Angalia kwa mfano hili la kanisa katoliki kuwaelimisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa kuchagua viongozi muhimu katika uchaguzi ujao wa 2010.

  Mimi naliunga mkono sana hili, lakini kinachonishangaza ni viongozi hao wa dini wamekuwa wanafiki wa kutosema ukweli bila kuficha kwamba uongozi tulionao sasa hivi nchi mwetu hautufai kabisa Watanzania kutokana na ushahidi mwingi uliokuwepo wa mambo mbali mbali kuhusu ufisadi, mikataba isiyo na maslahi ya nchi, kuhusu kutoshughulikiwa kwa mafisadi pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mafisadi mbali mbali wengineo ambao bado wamo ndani ya chama serikali na mashirika yetu ya umma.

  Ningependelea kuona hawa viongozi wa dini wanasema kweli kabisa bila kuficha maana siku zote msema ukweli ni mpenzi wa Mungu na wao kama viongozi wa dini wanahitaji siku zote kuwa wakweli kwa waumini ao bila woga au kificho.

  Ninachotaka waseme ni kwamba Kikwete kama Rais kashindwa kutimiza ahadi zake, kashindwa kupambana na ufisadi kashindwa kuhakikisha mikataba ya rasilimali zetu mbali mbali ikiwemo madini bado inaendelea kutokuwa na maslahi yyoyote kwa nchi yetu, hivyo Watanzania tuna kila sababu ya kuchagua Rais mpya katika uchaguzi wa 2010 bila kujali anatoka dini gani au chama kipi. Pia Wabunge wengi nao ni wasanii hivyo Viongozi wa dini wangelisema hilo kwamba Wabunge kama wawakilishi wa wananchi wameshindwa kazi za na matokeo yake kipindi cha kuanzia 2005 hadi sasa kimeuyumbisha sana nchi yetu kuliko wakati mwingine wowote ule tangu tupate uhuru kutokana na Wabunge kutokuwa makini na siku zote kufuata mstari wa chama hata kama wanaona hakuna maslahi yoyote kwa nchi

  Hayo maswali yako mengine uliyoyauliza nayo yana umuhimu mkubwa sana. Inakuwaje shule za seminari na hospitali zinatoza viwango vya juu sana kuliko shule na hospitali nyingine. Ingekuwa vizuri sana kama ungetuwekea mifano michache ya bei hizo.
   
Loading...