Aiyo mchumba siku fichi, ukikosa dole gumba ujue we ni mgumba wa maandishi.
Hasa bila hili dole utaandika vipi, maana ndio dole linalosaidia kushika biki.
Nimetafakari mbali aisee, dole gumba mi nalikubali mazee.
Msiojua maana acheni niwaelezee, dole gumba mliache msilichezee.
Sa skia dole gumba linasabahi, ukiwa mbali dole gumba linatoa hai.
Dole gumba linafanya tunafurahi, na kwenye furaha ndio kunako kutwa uhai.
Mtaani hali tete, bila ili dole lisingekuwepo lile dole la mabeste.
Nacho fahamu hili dole halivai pete, linashika rungu kama huamini kamuulize kipepe.