Nitapata wapi betri halisi za Samsung hapa Tanzania?

Nitapata wapi betri halisi za Samsung hapa Tanzania?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
6,044
Reaction score
5,920
Wadau, nina visimu viwili vya Samsung: Galaxy S 1, na GT-C3222 ambazo sasa betri zake zimechoka. Nimejaribu kununua betri zake hapa Bongo lkn sikufanikiwa kupata genuine hata kwenye maduka yaliyothibitishwa kuuza simu zao.

Nikaamua kujitosa kununua betri feki nikidhani naweza kutumia japo hata kwa mwaka mmoja, lkn ni maafa. Betri ya GT-C 3222 niliyonunua wiki iliyopita jana imeaga dunia rasmi maana imegoma hata kupokea moto! Betri nyingine ya Galaxy S1 nayo nikiiweka kwenye simu, baada ya saa moja inakuwa imekwisha!

Nimemuomba mpenzi wangu ambaye ameenda ughaibu kwa wenzetu wasioruhusu bidhaa feki za China, ametembelea madukani wakamwambia hawezi kupata hizo betri maana simu zangu zimepita na wakati! Kwa kweli kwa sasa sina bajeti ya kununua simu nayoitaka, lkn pia siziamini sana simu zinazouzwa hapa Tanzania maana sina uwezo wa kuthibitisha ubora wake na naamini watengenezaji wake hutuletea simu za viwango vya chini kufuatana na uwezo wetu wa kiuchumi.

Nimejaribu kutafuta betri za simu tofauti kama Nokia au Tecno lkn nimeambiwa haziingiliani na Samsung ila Tcno na Nokia ndizo zinaingiliana.

Nisaidieni wadau, nitapata wapi betri nzuri kwa ajili ya simu za Samsung?
 
Mmmhhh
Ss naona turudi tu kwenye nokia na mi betri yangu ndo basi tena
S3 min

Mi sielewi hivi ndo kusema hata haya maduka yaliyothibitishwa nako wanauza fake?
 
Back
Top Bottom