Nitaoa mwanamke asiye na kazi

Naona mleta mada anajadili jambo gumu, wakati hata kumbe hajaoa....teh

Hapa ni sawa na kuchoma battery ya gari la mafuta lililo anguka...teh
 
Kunywa soda kwa mangi
 

Kwa hiyo unakomaa kuniaminisha kwamba hakuna kabisa wanawake wajane magolikipa waliofanikiwa kulea watoto wao bila msaada wowote kutoka kwa ndugu?

acha kufanya assumptions za ajabu wewe! wapo sana tu tena wengine ni majirani zangu. Kuna father mmoja muislamu alifariki mimi nikiwa bado ni teenager aliacha wajane wawili na wote aliwahi anawahudumia yeye.

Leo hii tunavyoandika hapa watoto aliwaacha wako makazini na walisoma hivyo hivyo kwa shida shida.

Hizo kazi za kukaanga mihogo/maandazi zinazoingiza 10k kwa siku, wapo watu wanaendesha maisha yao kwa hivyo hivyo vipato unavyoiona kwako ni duni. Wanakula,wanavaa na wanasomesha.

Mwanamke yeyote akishajijua kwamba ana mzigo wa watoto hata kama alikuwa ajuhi fuma vitambaa! atajua mpaka bei ya cabbage bustanini ni shilling ngapi ili aweze kufanya biashara.

kwani unafikiri ni kwanini watu huwa wanawasifiaga single mothers humu jamvini?
 
Hayo mambo ya ujentoman ya kupitiana kazini nimemaachia wenye mioyo migumu kama jiwe. Ujentoman wangu mwenye moyo laini kama pamba... nimefanya tu busara ya kumzawadia kaPasso apambane na hali yake... Sipendagi ujinga mimi
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 hahahah hapo umemuweza sasa.
 
Basi sawa kwa kua unaridhia maisha duni ya familia yako kipindi haupo
Umaskini si kitu kizuri
 
Mmmmh! Aisee ndugu una muda gani kwenye ndoa yako? Mbona umeongea vitu vya msingi na vizito namna hii? Mpaka nimekaa kurudirudia kusoma ulichoandika? Maneno yako si ya vijana kama mimi hapa ambao bado tunaparamia wanawake ovyo kwa kuangalia external factors, Hongera sana kwa kupata busara hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…