Wana Jamvi, pamoja na uzoefu wangu kwenye mambo ya mahusiano kuna mkasa umenikuta na nashindwa kuutatua.
Kisa kiko hivi...
Nilikuwa na kimchepuko changu kimoja, hiki kimchepuko nilikuwa napiga nacho trip za kikazi allover TZ. Mimi kazi zangu zina involve kisafiri na wife anakazi yake hawezi kusafiri. So mara nyingi nakuwa siko home. Badala ya kuokota okota wanawake kila mara nikaona nitafute mdada ambaye yuko flexible na safari ili nile naye route.
Basi maisha yakaendelea raha mustarehe takribani miezi 8 hivi. Siku moja simu ya mchepuko ikawa inazingua, nikaichukua kupeleka kwa fundi. Fundi nilikuwa nimemwachia password ili aweze ku test akisha tengeneza.
Sasa kumbe baada ya kutengeneza fundi akawa ameondoa password. Nikafika kawasha pale iko poa, akazima nikaweka kwenye bag kwenda nyumbani.
La haula sijui nini kilitokea wife akawa ameiona hii simu kwenye bag. Kumbuka si kawaida yake kabisa ku search kwenye bag langu la kazini. Nafikiri alikuwa anatafuta kalamu. Akaona meseji zangu na dada nyingi tu za kutosha.
Basi ikawa kesi pale, nika appologise kwa muda, akatishia kuondoka nika mshawishi nikamwambia bora mimi ndo niondoke kama hunitaki tena..basi baada ya muda kidogo akanisamehe na tukaendelea vizuri.
Tatizo ni kwamba wakati mwingine akikaa ana badilika na kuanza kulia, haamini kama yule mwanamke nimeachana naye. Haamini kama nimeachana naye ndo shida kubwa. Ukweli ni kwamba nimeachana naye. Je nitawezaje kumhakikishia kuwa nimeachana naye hadi aridhike. Hilo ndo tatizo langu kubwa na naomba mawazo yenu.