Nitamdai vipi hela ndugu yangu?

Kama umeamua kweli ,nenda ukamdai yule jamaaa tens mfungulie mashitaka,yeye atakuja kumdai alimpa pesa,ww hukumpa pesa dada yako mfuate yuleeee mtu wa kwanza
Mshikaji hana kosa. Na sister alivyokubali kwamba ni kweli alipokea iyo hela tulikua wote watatu yaani mimi, sister na mshikaji. Kumsumbua tena na kesi itakua sio poa.
 
Ndugu wanakuwaga na ufala sana, kuna mtu ana laki5 zangu ni mwaka na nusu umeisha sasa anasubiri nimkumbushe. Ila kwa sababu alitumia pesa yako bila ruhusa, tumia aggression kuidai au chkua vitu vyake ukauze ufidie.
Na huwa wanauchuna wakijua ishu itaisha kindugu ndugu.

Inaumiza sana ukifikiria mtu ujawahi kumfanyia ubaya wowote
 
Jitahidi kuishi katika Maisha ya usafi cleanest life style
Acha Pombe
Acha ngono
Acha Kuhifadhi chuki ndani ya moyo wako Wapende watu wote na kuwaombea Amani.

Hakika utafanikiwa zaidi M1.5 ni hela ambayo utaipata Muda sio mrefu.
 
Jitahidi kuishi katika Maisha ya usafi cleanest life style
Acha Pombe
Acha ngono
Acha Kuhifadhi chuki ndani ya moyo wako Wapende watu wote na kuwaombea Amani.

Hakika utafanikiwa zaidi M1.5 ni hela ambayo utaipata Muda sio mrefu.
Hayo yote nayafata mkuu. Hata mimi kila nikifikiria kuwa aggressive naumia sana. M 1.5 is not worth kuweka hatarini undugu tatizo mtaani hali ni ngumu sana. Nime-pretend as if nothing happened lakini nimeshindwa
 
Ni dada yangu wa mama mmoja ila baba tofauti. Namdai milioni 1.5. Mwaka jana Octoba kuna mishe nilifanya jamaa niliefanya nae kazi Disemba mwishoni akaleta hela home milioni 1.5 ila nilikua nimesafiri kwa sababu anamjua sister adogo? Ana mpango wa kufungua saluni, kuna vifaa vyake vya saluni pale home anapoishi mpaka sasa ninachofikiria ni kwenda kuvichukua ivyo vitu wakati hayupo halafu niiuze kufidia hela yangu.
Chief fanya kama ilipotea ipotezee. Hata yeye anataman kama angekuwa nayo akupe. Sasa unaweza kumsababishia akajiuze ili apate hela ya kukulipa. Una afya akili timamu na muda wa kuanza upya hujachelewa. Japo muite muulize kiutaratibu akuambie nini kilitokea aliitumiaje.
 
Ndugu wana lostisha sana... mimi kuna kaka yangu wa damu baba mmoja mama mmoja ila hata akinikopa buku sahiv simpi.

Maana mimi nina udhaifu wa kumuamini mtu, alishanikopa elfu sitini akasema atanipa chap alikuwa amekwama kidogo..

Ni mimi sipendi kumkumbusha mtu deni, sasa akajisahaulisha kwamba namdai, hiyo siku amekuja anataka nimkopo elfu kumi sijui usiku luki imeisha, nikamuambia sina kitu.

Akaniambia fanya hata buku, nikamuambia aisee sina.

Nimeamini ndugu wa kweli ni mzazi wako na kidogo mkeo na watoto... hao wengine ni watu watakuja kuwa na life lao na nyumba zao.

Kuwa makini na ndugu kuliko kitu chochote

Ndgu miyeyusho mzee
 
Ni dada yangu wa mama mmoja ila baba tofauti. Namdai milioni 1.5. Mwaka jana Octoba kuna mishe nilifanya jamaa niliefanya nae kazi Disemba mwishoni akaleta hela home milioni 1.5 ila nilikua nimesafiri kwa sababu anamjua sister akampa ile hela. Sister akaipiga akauchuna. Nilivyorudi mwezi wa kwanza nimefatilia malipo yangu kwa jamaa ndio akaniambia hela alipeleka home.

Kuulizia home sister kasema ni kweli alipokea iyo hela mambo yakaingiliana akaitumia kwaiyo atanirudishia mwezi wa 3. Mwezi wa 3 ukaisha hajalipa nikaulizia akanipiga sound za kujilizaliza tu. Ooh baba angekuwepo angenilipia sijui nini nini.. Mpaka leo hajanilipa chochote na wala sioni kama ana mpango huo. Najua hawezi kulipa kwa mara moja lakini hata kupunguza kidogo kidogo tu hakuna.

Nilijaribu kuwashirikisha wakubwa jibu nililopewa nimeambiwa nimuachie Mungu tu. Kiukweli hela yangu inaniuma sana mbaya zaidi am jobless kila nikikosa mchongo wa kunilinda hata kwa siku moja tu naikumbuka hela yangu. Bora ningekua na kazi ningeipotezea tu iyo hela.

Nitadai vipi hela yangu hata kwa njia aggresive kidogo? Ana mpango wa kufungua saluni, kuna vifaa vyake vya saluni pale home anapoishi mpaka sasa ninachofikiria ni kwenda kuvichukua ivyo vitu wakati hayupo halafu niiuze kufidia hela yangu.
Huo utakuwa ni wizi na atakuwa na kila haki ya kukushitaki na ukakamatika kirahisi tu.
Kama unajua ana mpango huo, mwambie mapema kuwa deni lako lipo pale pale na unatarajia kulipwa, usimpe mazingira ya kuhisi amesamehewa.
 
Yaani ndugu walisema umuachie Mungu bila kumhoji? Zuia vitu vyake hivyo ila usiuze vichukue ukatunze sehemu na anatakiwa ajue kuwa ni wewe umevichukua, hao ndugu watakapokuja na wewe unawaambia wamuachie Mungu
 
Kwa jinsi nilivyomsoma sioni kama ana mpango wa kunilipa ndio maana nafikiria kutumia njia aggressive kidogo, lakini nitafanya kwanza kama ulivyonishauri

Hiyo Njia aggressive muachie afanye aliyempa dadaako Pesa yako.
Wewe hukumkabidhi hizo pesa. Mwenye kosa ni huyo aliyempa dadaako. Alimpa dadaako Kwa ruhusa ya Nani? Kama ulimruhusu Sawa
 
Pole sana.
Vipi unaonaje hali yake kiuchumi? Ni mtu anayemudu kulipa ila hataki tu? Kuna wengine ni sawa na kuidai maiti.
Kama ana uwezo ila hataki, nenda kwa yule mlipaji wako muelezee hali ilivyo, muombe aje kudai kwa kisingizio wewe hutambui kama alimpa dada yako.
 
Mwachie Mungu tu
Mwishowe waanze kukuloga huko kwenu
Ila sista yako ni mnyama,hana utu,kaa naye mbali atakuja kukudhuru siku moja
 
Huyo hata alipopokea hakukuambia, ni mtu wa ovyo huyo usipoteze muda wako, simama jifute vumbi ingia mtaani upambane utapata nyingine, lesson learned
 
Sio mstaarabu Kama bwai mbwai chukua vitu vyake kaweke sehemu mwambie umekopea Kama vipi akagomboe tu maana utakuta iyo hela yako ndio kanunulia ivo vitu vya salooni
 
Back
Top Bottom