VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Sina haja ya kuficha. Kwanza, nimefanikiwa kuhuisha (ku-renew) Cheti changu cha Uwakili baada ya kukisitisha kwa miaka kadhaa. Kilichonivutia hadi kuhuisha cheti changu kwa mwaka huu 2017 ni uchaguzi wa Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) wa mwezi Machi mwaka huu kule Arusha.
Chama hichi cha Mawakili wa Tanganyika kinamhitaji Tundu Lissu kuwa rais wake. Kwa jinsi utawala wa awamu ya tano unavyosema na kufanya, TLS haina chaguo lingine zaidi ya Tundu Lissu kuwa Rais wake.
Lissu ni international figure. Akisema, Mawakili watakuwa wamesema. Lissu hujenga hoja;hutetea wafuasi wake; huthubutu kubuni visivyo vya kihuni; Lissu hutaka heshima kwa Mawakili na wananchi kwa ujumla. Ni Lissu tu.
Najua TLS ina wagombea watano kwenye Urais wa mwaka huu. Najua CCM tuna wagombea wetu wawili kati ta hao: Stolla na Mandari. CHADEMA nao wana wagombea wawili: Lissu na Masha. Lakini, Mawakili wakikutana Arusha huacha kando vyama vyao na kulinda maslahi yao.
Kwa wakati uliopo, Lissu haepukiki. Kwa wakati huu, kumchagua Lissu kuwa Rais Mawakili Tanganyika ni kuleta equilibrium hapa Tanzania. Nitakuwa Arusha kuanzia tarehe 12/3/2017 ili kufanikisha kuchaguliwa kwa Lissu.
Lissu si wa mchezomchezo. Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam