Nitakuwa wa mwisho kutoa big up kwa rais kwenye sakata hili la makontena ya mchanga wa dhahabu!!

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,995
2,245
Swali la muhimu la kujiuliza, Je, dakika 5 zilimtosha rais kuielewa report hii kwa kina na kuitolea maamuzi au alipewa kabla akaisoma leo tar 24.5.2017 ni makabidhiano tu?.

Nitakuwa wa mwisho kumpongeza rais au nisimpongeze kabisa kwa sababu zifuatazo:

1. Nilikuwa wa kwanza kumpongeza polepole kwenye ishu ya katiba mpya hususani alipokuwa akisema nafasi za ukuu wa wilaya, mkoa hazina tija na athari za rais kupewa majukumu/maamuzi makubwa! leo hii najisikia aibu machoni pa watu waliokuwa wananisikia nikitoa big up kwake.

2. Huyu prof Muhongo ambaye leo rais anamwona mbaya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania lilishamwona hafai toka muda mrefu ndiyo maana liliazimia kwa pamoja achukuliwe hatua. Hivyo rais kutengua uteuzi wake ni kukiri kosa alilolifanya kwenye uteuzi wake. Kwa hili sina sababu ya msingi ya kusema big up.

3. Nitakapoona mali za mafisadi na wahujumu uchumi na watu wao wa karibu wote zinafilisiwa baada ya kubainika na kosa.

4. Kumtumbua prof Muhongo ni sawa na kufukua makaburi, hivyo marais waliopita/wastaafu kama walihusika katika sakata hili wakachukuliwa hatua kama watuhumiwa wengine. Wengi wanasema katiba hairuhusu! Tujiulize mbona tunavunja katiba kwa mambo ambayo wakati mwingine hayana tija kwanini tusivunje katiba kwa suala la msingi kama hili? Uhusika mmoja wapo wa marais wastaafu ni usiri wa mikataba kama mamikataba yangekuwa wazi mambo mengi yangekuwa wazi.

Mwisho yatupasa kutambua mbele ya Mungu hakuna dhambi kubwa wala ndogo japo tunajifunza dhambi ya kumkashifu roho mtakatifu ndiyo dhambi isiyosameheka. Kwa Mungu hakuna mkubwa wala mdogo kwa maana ya umri, nafasi au kipato!
 
Sure....tutakuwa wengi. Hizi ndo sanaa za ccm tangu uhuru....
Bashite tu anamshinda ila mihemko ya kutaka kuonekana live kusiko na faida yoyote.
Chato international airport ni kwa ajili ya wanyonge?
 
Naomba anayekumbuka orodha ya baraza la mwaziri wakati michanga inaanza kusafirishwa nje.
 
Big up bado sana...Kwani ni Chama gani kilisaini hiyo mikataba?

Kwani Tanzania ya Viwanda Imekuwa?

- Pesa Ya Rambi Rambi
-Fao la Kujitoa
-Mikopo ya Wanafunzi
-Dawa Hospitalini

----Watu Hawashibi Maneno, people want to see positive change on their lives

mfumuko wa bei...Sukari 3000, unga ghali kuliko petroli

Kwani Ni Chama gani waliingia hii Mikataba by the way? Wako wapi?
 
Naungana nawe kwa hoja zako. Ni ujinga na upumbavu kushangilia mambo yenye ukakasi. Kama kwer rais ni mtetez wa wanyonge na anauchungu na maliasili za taifa. Kwanz angeanza yeye kuwa muwaz kweny mikatba, tujue anasaini nin. Pili huwez mtumbua muhongo then jk anakula bata. Huu ni usanii tu
 
Back
Top Bottom