Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la watu kutoa tiba kwa kuwa wameoteshwa. Napenda kufahamu kama nikiota ndoto nitajuaje kama nimeota au nimeoteshwa? Nikiota labda nimemwoa binti wa jirani yangu nikamweleza je atakubali au kuoteshwa kunatokea kuhusiana na tiba tu?
1. Nijuavyo mimi, kila ndoto inahusu vitu halisi katika maisha ya mtu - yaani, vitu ambavyo huyo mtu anavipenda, havipendi, amevipata, ameshindwa kuvipata, anavitamani avipate, anavichukia, anaviogopa, hana uwezo navyo n.k...
2. Ndoto zinahitaji kuzitufuatilia kwa karibu sana ili kujua ujumbe wake.
3. Baadhi ya ndoto zina 'pattern' fulani - mfano, wanyama (simba, kiboko nk), shimo refu sana, kuzama majini, kuvuka barabara kwa shida sana na kisha kuvuka gari la speed sana kupita, kukabwa shingoni au kuwa katika hali ya hatari na kupiga kelele, kuwaambia rafiki, ndugu wakusubiri wakati unakojoa nk.
4. Ni kweli unaweza kupata ujumbe kuhusu maisha yako kwa kufuatilia ndoto unazoziota. Kwa hiyo, unaweza kugundua kitu fulani katika maisha kwa kufuatilia ndoto - maana zina ujumbe unaohusu maisha ya kila siku ya mtu.