Nitaifanya CCK kuwa kama Chadema

Nitaifanya CCK kuwa kama Chadema

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
Kuzaliwa kwa Chama Cha Kijamii (CCK) kilichopata usajili wa kudumu Januari 27, mwaka jana, hakukutarajiwa na wengi.
Kwa maana CCK iliyoasisiwa na waliokuwamo ndani ya Chama Cha Jamii (CCJ) kinachotajwa hadi leo, hususani Akitanda, hakikupokewa kwa nguvu kubwa katika kuanzishwa kwake.

Lakini chini ya uenyekiti wa muda wa Constantine Akitanda, CCK ilistawi, ikapata usajili wa muda Julai 23, 2010, hivyo ikawa mwanzo wa kuingia katika siasa za ndani ya Tanzania.

Akihojiwa na safu hii mwishoni mwa wiki iliyopita, Akitanda anasema safari ya kisiasa katika kuifikisha CCK kuwa na usajili wa kudumu, ilikuwa yenye ‘milima na mabonde'.

"Si kazi rahisi kushiriki siasa katika nchi zetu changa, lakini kwa uvumilivu na kujitolea kwa umma, tumefikia hatua hii," anasema.
Akitanda anasema, hadi kufikia sasa, chama hicho kina kauli mbiu ya ‘mabadiliko ni sasa, mabadiliko ni sisi' na kwamba itikadi yake ni uhafidhina wa uchumi wa kijamii.

Kwa mujibu wa Akitanda, itikadi hiyo inayotarajiwa kupitishwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi baadaye mwezi ujao, inahusisha mambo tofauti, ikiwamo kupima matokeo ya kiuchumi kupitia hali na maisha ya raia.

"Hatuwezi kusema uchumi umekuwa kwa kuangalia takwimu za jumla, sisi tunashuka chini na kuangalia huduma za kijamii zikoje, afya, maji, miundombinu na nyingine, zinakidhi na kuboresha maisha ya wananchi," anasema.

MKUTANO WA UCHAGUZI
Akitanda anasema CCK ni chama kinachotambua, kuheshimu na kuzifuata sheria za nchi, hivyo kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Aprili 19, mwaka huu.

Anasema wanachama hai wa CCK wenye sifa, wamepewa fursa ya kuwania nafasi yoyote ya uongozi, huku akijitaja kuwa mmoja wa wagombea nafasi ya Uenyekiti.

Akitanda anasema zipo sababu nyingi zinazomfanya agombee nafasi hiyo, mojawapo ikiwa ni kuendelea kukielekeza kufikia kusudio la kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

"Binafsi bado ni utashi wa kuitumikia CCK na kuipeleka mahali iwe kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)," anasema.
Akitanda, anasema Chadema imepitia nyingi ngumu katika kufikia mafanikio yaliyopo sasa, na kwamba si vibaya kwa vingine vingine kama CCK kujifunza.

"Nimekutana mara kwa mara na Freeman Mbowe (Mwenyekitiwa Chadema) na kuzungumza naye, kwa kweli ametoa ushauri mzuri kwetu ambao hatuwezi kuukataa," anasema.

Akitanda, anasema kushiriki sasa za ndani ni sawa na kujitoa mhanga katikati ya simba wengi.
Anasema hali hiyo inatokana na jinsi watu wenye maslahi binafsi, walivyojikita kwenye vyama vya siasa na serikali, ili kulinda maslahi yao na si ya umma.

"Sasa unaposhiriki siasa, lazima ufichue hila ovu na katika hilo, lazima uwaguse wenye maslahi binafsi, sasa kuingia katika siasa ni sawa kuishi ukiwa umekufa," anasema.

CHANGAMOTO ZA KUASISI CHAMA
Akitanda, anasema zipo changamoto nyingi katika kukianzisha chama kipya cha siasa, kishindane na vyama zaidi ya 17 vilivyo na usajili wa kudumu.

Anasema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa fedha, rasilimali watu na wataalamu wa mambo ya siasa.
"Watanzania hawana utamaduni wa kuvisaidia vyama vya siasa, sasa katika hali kama hiyo inakuwa vigumu kukiendesha chama kama CCK," anasema.

Hata hivyo, Akitanda anasema CCK imefanikiwa kujijengea mtandao wa washirika wa kisiasa na kwamba baada ya uchaguzi wa viongozi, wataunda ‘kikosi kazi' cha kukifikisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa mafanikio.
Anasema kwa vile dhamira ya ukombozi kama ilivyo kwa uongozi wake, haitegemei fedha, hivyo wataendelea kujenga itikadi ikiwa ni msingi wa CCK na kutafsiri dira, mwelekeo na malengo yake.

HALI YA KISIASA NCHINI
Akitanda anasema mazingira yaliyopo nchini hayatoi taswira chanya kwa siasa za ndani, akihusisha kushamiri kwa uovu unaojumuisha kutekwa, kuteswa, kujeruhiwa na kuuawa kwa wasiokuwa na hatia.

"Matukio tunayoyaona sasa yakiwa na taswira hasi kwa nchi hii, ni matokea ya kushindwa kwa watawala,"anasema.

AHIFADHI ‘JAMBO ZITO' MOYONI
Akitanda anasema hivi sasa ana kile alichokiita kuwa ni ‘jambo zito', alilolihifadhi moyoni mwake kuhusu taifa hili.
Anasema kutokana na hali hiyo, anakusudia kulitoa wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa chama hicho, Aprili 19, mwaka huu.
"Nina jambo ambalo kila ninapotafuta uwanja wa kulisema, siupati, limenizidi lakini ninamuomba Mungu aniweke hai hadi siku ya uchaguzi niweze kulitua," anasema.

HUJUMA, FITINA NA MAJUNGU
Akitanda anasema kwa uzoefu katika kushiriki siasa, amebaini kuwapo hujuma, fitina na majungu ndani ya vyama vya siasa.
"Kila kukicha kunakuwa na hujuma mpya, fitina mpya na majungu mapya, inahitaji ujasiri sana katika kukiongoza chama cha siasa," anasema.

Hata hivyo, Akitanda anasema hali hiyo haistahili kuwakatisha tamaa wenye dhamana za uongozi, badala yake kukabiliana nazo hadi kufikia malengo ya kuleta ukombozi unaohitajika nchini.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Bora akaendeshe shamba lake tu au grosari yake. CCK kuwa sawa na Chadema ni ndoto za alinacha
 
Siku hizi bila kuitaja CHADEMA kwenye maelezo yako basi ujue hakuna wakukusikiliza.

Kwa sasa CHADEMA imekuwa bidhaa muhimu sana kisiasa(kama maji katika maisha), yaani Usipoisifia basi utaitukana!!

Haya CCK karibuni, ila mjue pamoja na umakini wote wa CHADEMA, iliwachukua zaidi ya miaka 20 kufikia hapo walipo.
 
Nape atagombea nafasi ipi ktk chama? Au yeye ni automatic vuvuzela leader?
 
Jaribu kuwa UNIQUE PARTY don't COPY other POLITICAL PARTIES... Kwanza anza mikutano ya HADHARA... tukuone
 
ADC, CCJ, CCK, NCCR, CUF, CCM, DC, TLP, PPT, CHEYO kwa ummoja wao hawana ubavu wa kucheza mziki wa CDM kwa sasa...labda wenyewe wavurunde...
 
Back
Top Bottom