Mkuu katika wote waliotoa Comment hakuna hata mmoja amewahi kuwa nayo.
Mimi nanayo. Spea sio tatizo hata kidogo hilo la kwanza.
kuhusu filter inatumia filter number 1 sawana gari za Toyota ambazo zipo za 5,000 - 20,000 ni choice yako
ukitaka "genuine" Nisani 15,000 ambayo hakuna utofauti wowote (perfomance wise).
Engine oil 4litres na 3.5litres transmission fluid kama ilivyo kwa Corrola, GX100, na magari mengine ya Toyota.
Air filter 10,000 hadi 12,000 kama za GX100 (ninayo). ikumbukwa filter na transimission hazibadilishwa mara kwa mara.
Fuel consumption: town trip full A/C 8.2km/litres (sijawahi kujaribu kutembelea bila A/c) highway ama safari ndefu inategemea na uendeshaji mimi huwa ni 11.2km/litre with full A/C(sijawahi kuendesha bila A/C ili kulinda usafi wa ndani wa gari)
X Trail pamoja na ukubwa wake ina A/C kali kama GX100/110, Ina Four Wheel Drive, confortable, taaa zake ni kali (kwa wanaopenda kuendesha usiku), stability njiani ni kama GX100/Gx110/115 kwa waliowahi kuziendesha.
Vitu gali kwenye Xtrail ni Shockups, Taa incase zimeibiwa ama kuvunjika, na plugs moja ni 25,000 ingawa utabadilisha mara moja kwa mwaka.
Kwa ujumla sijawahi kuregreat kununua Nassan Extrail (usiombee ununue Nassan pathfinder ama Terrano huko hakuna rangi utaacha ona).
Bei Show rooms ni kati ya 18 - 24 million inategemea na model NT30, NT31 na mwaka uliotengenezwa, Nissani Xtrail zinautofauti sana karibu ain 5 kwenye taa za mbele na nyuma pamoja na Dash board. soma zaidi kwenye makampuni yanaouza magari kuona utofauti.
ukiagiza mwenyewe unaweza kuipata hadi 15m mpaka usajili.