Kuna dogo mmoja alikuwa anatoka Mkoa anakuja Dar Es Salaam Sasa akamwambia konda.
Dogo: Konda tukifika Chalinze uniambie.
Konda: Sawa.
Gari likatembeaaaa sasa konda akasahau kumwambia dogo walipofika chalinze, wakapapita. Dogo kuona hashituliwi ikabidi amuulize konda.
Dogo: Konda, chalinze Bado!?.
Konda: Ayaaah nimesahau.
Abiria: Weeeee!! mtoto kakwambia tangu anapanda umwambie tukifika chalinze , haya geuzeni gari tumrudishe.
Dereva akageuza gari mpaka chalinze.
Konda: Haya dogo chalinze ndo hii, njoo ushuke.
Dogo: Hapana sishuki, baba alinambia nikifika chalinze ndo Nile maandazi yangu.😂😂😂