Nishaurini: Nimegundua pesa ninazompa anahonga mwanaume mwingine

kevin strootman

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
1,109
1,840
Mimi ni kijana wa kiume nna miaka 27, kuna msichana nimekutana nae miezi minne iliopita, kiukweli ni mzuri sana pia ni mwanachuo hapa Dar, kiukweli nimemuhudia sana ndani ya miezi hiyo minne.

Nimemnunulia hadi kiwanja Chanika, simu nzuri, pesa za matumizi nampa nyingi tuu nimemwambia boom lake awasaidie wazazi nyumbani kwani aliniambia wako vibaya sana (maskini wa kutupwa)

Sasa juzi nimegundua kumbe pesa ninazompa ana kamwanamme kake nae anakahonga anasoma nako chuo.

Gharama nilizomgharamia nimecalculate ni zaidi ya M8, nikimuulza analeta kiburi anadai kama vipi tuachane.

Je, nifanyaje? Juzi washikaji zangu wamenishauri tuwateke wote tukawatese nje ya mji ikiwezekana tumuue huyo jamaa.

Mnanishauri nini?

Inauma sana
 
Yaani ndani ya miezi mi4 umehonga m8? kwangu naona hii chai.

Kwa mtu mwenye uwezo wa kuhonga m8 hawezi kulalamika hivi...labda kama hauzipati kwa jasho lako unamwibia baba.

Kwa mwezi unahonga 2m kwa siku elfu 67. ??? Hujiulizi kwanini Heslb inawahonga 8500 kwa siku unafikiri board haina akili ???
 
Dah jamani...
Sikupangii hela zako mkuu lakini hizo hela ungetafuta mtu yeyote humu wanaokujaga kuomba msaada wa kazi ama mkopo uwape na Mungu atakubariki.
 
Dah jamani...
Sikupangii hela zako mkuu lakini hizo hela ungetafuta mtu yeyote humu wanaokujaga kuomba msaada wa kazi ama mkopo uwape na Mungu atakubariki.
Ila kwa ushauri kuhusu huyo mwnaamke hakufai au labda kama unataka golddigger as a wife
 
Back
Top Bottom