FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 304
- 236
Inaelezwa kuwa matumizi ya nishati asilia ni kichocheo kikubwa cha maambukizi ya mfumo wa upumuaji (Acute Respiratory Infection) ambayo yanaongoza kusababisha vifo vya watoto walio chini ya miaka 5 ambao wanalazwa hospitalini kutokana na magonjwa mbalimbali ya utotoni hasa katika nchi zinazoendelea.
Mpango wa Taifa wa Kuzuia Maambukizi ya Mfumo wa Upumuaji katika uchunguzi wake uliofanyika katika vituo 14 vya afya unaonyesha kuwa asilimia 10.5 ya watoto waliopelekwa kutibiwa katika vituo hivyo walikuwa na dalili za maambukizi ya mfumo wa upumuaji ambapo asilimia 50 walikuwa watoto walio chini ya umri wa mwaka mmoja.
Watoto walio katika hatari ya Kuambukizwa
Ugonjwa huo una mahusiano ya moja kwa moja na hali ya kipato cha familia, ambapo watoto wanaoishi katika familia masikini wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa ya mfumo wa upumuaji ikizingatiwa kuwa nishati asilia ni chanzo kikubwa cha mwanga na kupikia.
Nyumba nyingi za vijijini zimeezekwa kwa nyasi huku zikiwa na madirisha madogo ambayo hayapitishi hewa kwa urahisi. Vilevile kwa wakazi wa mjini baadhi yao hawazingatii ujenzi wa nyumba zenye mfumo mzuri wa kutolea hewa.
Utafiti huo Chuo Kikuu cha Umea (2011) unafafanua kuwa watoto kutoka familia maskini ambao walikuwa wanakohoa ni asilimia 31.4, familia zenye kipato cha kati ni 28.5% na familia zenye kipato kikubwa ni 21.4%. Pia matokeo yanaonyesha kuwa watoto kutoka familia maskini walikuwa wanakohoa mara 1.7 zaidi ya wale wa familia tajiri.
Inaelezwa kuwa uwezekano wa watoto wanaotoka katika familia masikini kuendelea kusumbuliwa na magonjwa ya mapafu ni mkubwa ikiwa hatua hazitachukuliwa ili kubadilisha mazingira wanayoishi ambayo hayawahakikishii usalama wa afya zao.
Zaidi, soma hapa => Maambukizi ya Mfumo wa upumuaji yanachangia asilimia 10.5 ya watoto wanaotibiwa hospitalini | FikraPevu