Nisaidieni tofauti ya viza na passport

Nisaidieni tofauti ya viza na passport

prenge

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2015
Posts
219
Reaction score
283
Msaada jamani hiyo viza sijui wanaandika hivyo bwana wee nisaidieni au passport ndio viza kwa kiswahili?
 
Passport kwa Kiswahili ni "pasi ya kusafiria". Hiki ni kitambulisho cha kusafiria ambacho hutolewa na nchi kwa raia wake. Visa ni "ruhusa" ya kuingia katika nchi nyingine. Visa huombwa kutoka na kutolewa na mamlaka za nchi unayotaka kwenda, mara nyingi balozi za hizo nchi. Visa hutaja muda anaokusudia kukaa msafiri pamoja na lengo la safari. Visa hubandikwa katika kitambulisho cha kusafiria (pasi ya kusafiria "passport") cha mhusika.
 
Ili kusafiri nje yq nchi unahitaji kuwa na pasi ya kusafiria. Ili kuingia katika nchi fulani unahitaji kuwa na visa ya nchi husika. Kwa kifupi, passpot inatolewa au ni mali ya nchi yako ya uraia wakati visa inatolewa na nchi unayotaka kuingia.
 
Passport hutolewa na idara ya uhamiaji ya nchi yako na visa hugongwa kwenye passport na ubalozi Wa nchi unayotaka kusafiri kama kibali cha kuingia ktk nchi hiyo
 
Passport kwa Kiswahili ni "pasi ya kusafiria". Hiki ni kitambulisho cha kusafiria ambacho hutolewa na nchi kwa raia wake. Visa ni "ruhusa" ya kuingia katika nchi nyingine. Visa huombwa kutoka na kutolewa na mamlaka za nchi unayotaka kwenda, mara nyingi balozi za hizo nchi. Visa hutaja muda anaokusudia kukaa msafiri pamoja na lengo la safari. Visa hubandikwa katika kitambulisho cha kusafiria (pasi ya kusafiria "passport") cha mhusika.
Asante mkuu....
 
Aiseeeee umetiririka vyema. kwa lugha za wenzetu wanasema, very precised/ well explained.
 
Back
Top Bottom